Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Kama haikudhuru kitu wala kukupunguzia kitu,wasaidie tu,huwezi kujua maisha ya huko mbeleni,maisha ni safari,


Huenda hao watoto huko mbeleni wakaja kua na maisha bora ukubwani mwao,lazima wataukumbuka tu wema wako,

Wema ni Akiba.
 
Nadhani kuna uzi humu ulikuwa unaelezea kero zinazopatikana katika nyumba za kupanga, mimi kiukweli kero ndogondogo huwa nazitatua mwenyewe ndio maana ule uzi nilikuwa naupitia juu juu tu, ila baada ya kunikuta jambo kwenye hizi nyumba za kupanga ndipo hapo ikabidi niurudie kuusoma ule uzi upya.

Hapa nilipopanga tunaishi wapangaji 3.
1. Mimi.
2. Chumba kingine anaishi kijana mmoja dereva wa gari la mafuta hivo mara nyingi anakuwa nje ya mkoa.
3. Chumba kingine anaishi baba, mama na watoto wake 5 kwenye chumba kimoja na sebule.
Baba akiwa anafanya kazi gereji na mama ni mpika vitumbua.
Sijajua wanalalaje ila mimi naleta kero yangu jamani.

Hii familia imekuwa ni kero kubwa sana kwangu aisee.
Yaani ni wanaomba kuliko unavyodhani.
Hatukatai kama shida ni ya kila mmoja ila ikizidi huwa kero kubwa sana kwa wengine.

Wakiamka tu asubuhi, mama huyo huja kunigongea mlango mara aombe sukari, mara majani ya chai.
Ikifika mchana utasikia umepika nini, naomba kijiko kimoja cha mchuzi nimlishe mwanangu.
Usiku ikifika anakuja mtoto wake mlangoni kwangu na chakula kikavu hata sahani 3 akitaka niwawekee mboga.

Yule baba nadhani anaacha pesa ya matumizi ila sijui ni kwamba haitoshi au sijui kuna nini.

Nikipika mboga au chakula kosa kisinukie, utasikia hodi mlangoni na kibakuli.

Akitoka anawaachia maagizo wanae kuwa wakirudi shule waje kwangu niwape mia mbili mia mbili wakanunue maandazi wakati hajaniachia pesa yoyote.

Yaani wanaomba kila kitu.
Kuanzia asubuhi mpaka jioni
Wakipumzika ni siku 2 ya 3 wako mlangoni kwangu.

Kuna siku nilimuuliza kwani huachiwi pesa ya matumizi.
Akasema anaachiwa ila haitoshi, nikasema si unachoma vitumbua?
Akanijibu matumizi mengi sana ndani kwake hivo nimsaidie tu hivohivo.

Yaani naweza nikawa nimelala au nacheki Tv, nasikia hodi natoka nje nikijua ni mgeni wangu ila nikifungua ni yeye anataka mara kitunguu au nyanya.

Kuna siku niliwahi mwambia kuwa apunguze usumbufu wa kuja kuomba vitu, akapumzika siku 5 tu, ya sita huyu hapa.
Tena sahv anawatuma wanae waje kuniambia kwamba wana njaa niwape chakula


Nina uwezo wa kuhama ila hapa ni jirani na kibaruani kwangu.
Natembea tu na miguu.
Nakaa hapa kuepusha gharama ya safari.

Wazoefu naombeni la kufanya.
Kabira,halafu wana uzazi hao?
 
1000408689.jpeg
 
Siku ukiwapa chakula bahati mbaya watoto matumbo yakaanza kuwauma ndo utajua miaka yote ya msaada si kitu kwao.... maana mpk police utalala siku hyo kwa kesi ya ulitaka kuua watoto wao!!

Mzee wangu aliwahi kuniambia
"Wema usizidi uwezo..."
 
Achaaa roho mbayaa,kama unauwezo wasaidie....hakuna raha na baraka kama kusaidia wenye uhitaji?fanya hivi kama unakiuwezo wanunulie kisado cha nyanya,vitunguu...na tumafuta....afu wambie mtumie hivyo kila mwezi
Wewe huna akili
 
Mimi ni Ke, nishawahi kuwakazia ila najikuta tu nawaonea huruma watoto.
Maana wanakwambia tangu jana usiku walivyokunywa uji na mihogo mpaka mchana huo hawajala
Sasa hilo ni suala la usumbufu wa wawapi wasaidie hao watoto watabeba kaburi lako haya maisha tunapita tu
 
Ni mitihani ya dunia na majaribu pia.
Kama unacho toa tu kama sadaka, na kama huna waambie sina ila usiikalifu nafsi yako.

Kama unaona ni kero basi tafuta nyumba hayo maeneo karibia na kazi

Ila usiwasahau hao watoto kama utawaona uwe unawatoa kiaina

Kuna kitu unaonyeshwa
 
Nimejifunza usikilize moyo wako ikiwa ni matokeo ya kile ulichofikiria au kukiona utapata furaha ama huzuni, ama hisia zozote,

👉 Ukitoa huku unaumia moyoni ni kazi bure, au unamchamba au kumsimanga ni kazi bure

👉Ikiwa umeamua kuwasaidia wape tuu nyanya au kitunguu hv hv vya jero, au chakula hiki hiki kinatupa kukimbilia chooni, wape chakula hicho roho ama nafsi yako ikiwa Haina kinyongo na mtu....

Familia yetu ni wakulima hasa tuna mashamba ya kutosha japo ya kukodisha,,

Kuna jamii zinapita kuomba ndizi, mahindi wakifika home wanapewa kiroho safi, kama hakuna ni hakuna

Ilitokea hekari zote kipindi fulani mzee aliotesha mahindi sasa wakati wa kupalilia huwa anatumia CHAMBUA bhn,

Ilitokea nn akachukua dawa nyingn hekari zote zilikauka

Matokeo yake,, familia zilizotupa msosii, aseeh ni nyingi, msosi ulikuwa mwingi kama tunavyovuna,,

Nimewah ishi na dogo mmoja alikuwa level ya certificate & dip one kiroho safi sijawahi mtoza hata mia ya kitunguu wala nyanya!!


Nilikuwa nakula standard tuu msosi sikuwa najibana lkn km samaki lazima tule wote, sjui nyama nn,

Lkn Kuna sehemu nilikuja kupigwa njaa, ikatokea tuu nikapata kula sehemu two months,, plus freely kabisa kabisa .......

Hivyo fanya unachoona unaweza


Kikubwa ishi kwenye mipaka,, labda issue za hela,,

Ila mamboga mboga,, maharage ya toka last week umnyime mtu aaaah,, em peana hizo foods madam
 
Nadhani kuna uzi humu ulikuwa unaelezea kero zinazopatikana katika nyumba za kupanga, mimi kiukweli kero ndogondogo huwa nazitatua mwenyewe ndio maana ule uzi nilikuwa naupitia juu juu tu, ila baada ya kunikuta jambo kwenye hizi nyumba za kupanga ndipo hapo ikabidi niurudie kuusoma ule uzi upya.

Hapa nilipopanga tunaishi wapangaji 3.
1. Mimi.
2. Chumba kingine anaishi kijana mmoja dereva wa gari la mafuta hivo mara nyingi anakuwa nje ya mkoa.
3. Chumba kingine anaishi baba, mama na watoto wake 5 kwenye chumba kimoja na sebule.
Baba akiwa anafanya kazi gereji na mama ni mpika vitumbua.
Sijajua wanalalaje ila mimi naleta kero yangu jamani.

Hii familia imekuwa ni kero kubwa sana kwangu aisee.
Yaani ni wanaomba kuliko unavyodhani.
Hatukatai kama shida ni ya kila mmoja ila ikizidi huwa kero kubwa sana kwa wengine.

Wakiamka tu asubuhi, mama huyo huja kunigongea mlango mara aombe sukari, mara majani ya chai.
Ikifika mchana utasikia umepika nini, naomba kijiko kimoja cha mchuzi nimlishe mwanangu.
Usiku ikifika anakuja mtoto wake mlangoni kwangu na chakula kikavu hata sahani 3 akitaka niwawekee mboga.

Yule baba nadhani anaacha pesa ya matumizi ila sijui ni kwamba haitoshi au sijui kuna nini.

Nikipika mboga au chakula kosa kisinukie, utasikia hodi mlangoni na kibakuli.

Akitoka anawaachia maagizo wanae kuwa wakirudi shule waje kwangu niwape mia mbili mia mbili wakanunue maandazi wakati hajaniachia pesa yoyote.

Yaani wanaomba kila kitu.
Kuanzia asubuhi mpaka jioni
Wakipumzika ni siku 2 ya 3 wako mlangoni kwangu.

Kuna siku nilimuuliza kwani huachiwi pesa ya matumizi.
Akasema anaachiwa ila haitoshi, nikasema si unachoma vitumbua?
Akanijibu matumizi mengi sana ndani kwake hivo nimsaidie tu hivohivo.

Yaani naweza nikawa nimelala au nacheki Tv, nasikia hodi natoka nje nikijua ni mgeni wangu ila nikifungua ni yeye anataka mara kitunguu au nyanya.

Kuna siku niliwahi mwambia kuwa apunguze usumbufu wa kuja kuomba vitu, akapumzika siku 5 tu, ya sita huyu hapa.
Tena sahv anawatuma wanae waje kuniambia kwamba wana njaa niwape chakula


Nina uwezo wa kuhama ila hapa ni jirani na kibaruani kwangu.
Natembea tu na miguu.
Nakaa hapa kuepusha gharama ya safari.

Wazoefu naombeni la kufanya.
Hama haraka
 
Back
Top Bottom