Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Sawa, basi endelea kuwasaidia hao watoto hawana hatia. Mungu atakujaalia. Inaonekana ni binti mwenye roho nzuri na unaonekana utakuwa mke na mama bora. Usione ni kero sasa, at least kwa hao watoto.
Ndio, huwa nina huruma yaani nikogo hivo mkuu.
Watoto hawana hatia
 
Uwongo dhambi Ki ukweli watoto wanatesa sana wazazi ambao hao hao wazazi waliendekeza ngono zao kuwapata hao watoto.. Wazazi wengi wanapata watoto ilihali ni starehe za ngono na sio uhitaji wawatoto

Dunia haina huruma hiii kuzaa zaa bila mpangilio ni changamoto kwa watoto na wazazi
Kabisa yaani
 
Usiache kuwasaidia, wewe wasaidie tu ila kwa uwezo wako. Kwani kitunguu au nyanya moja ni shilingi ngapi jamani mpaka uje kulalamika huku.

Unajua wakati mwingine kuna baraka zinakuja katika maisha yetu kupitia hiyo misaada tunayowapa wenye uhitaji.

Wewe tenga kibajeti kidogo cha 1000 au 2000 kwa wiki yani ukinunua nyanya unaongeza kidogo. Na siku umekwama kabisa unawaambia huna. Ila usiwanyime kama unacho cha ziada. Ile sadaka unayotoa kanisani au msikitini basi usiitoe tena kule kwa sababu tayari utakuwa umeshatoa sadaka yako kwa jirani

Haya maisha huwezi jua kesho yako, hata wao hawapendi kudhalilika, nakuhakikishia ukiwasaidia japo kwa kidogo ipo siku Mungu atakuinua zaidi
 
Ukiona unaumia ndani usiwasaidie na ukiwasaidia basi chora mstari wa ukomo na wao wajue kabisa huo ukomo sababu kwa historia yetu ya ujamaa msaada unaojirudia hugeuka wajibu na haki kwa anayesaidiwa.

Mfano: Huyo jirani akishajua hapo kwako atapata chakula saikolojia yake itamtuma kuelekeza bajeti ya chakula kwenye mambo mengine sababu kinapatikana kwako.
Hapa ni ukweli tupu.
Hatari sana aisee.
Najitahidi ila nitafika ukomo
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Chakula sio kitu Cha kumnyima mtu,
Hakuna aliewai filisika Kwa kugawa chakula
Bro IPO SIKU utampa MTU KITU apatikane adui Yako TU umekwisha ye atawaambia TU unawaibia nyota. Kwishaaaaaaaa ana kaa pembeni
 
Usiache kuwasaidia, wewe wasaidie tu ila kwa uwezo wako. Kwani kitunguu au nyanya moja ni shilingi ngapi jamani mpaka uje kulalamika huku.

Unajua wakati mwingine kuna baraka zinakuja katika maisha yetu kupitia hiyo misaada tunayowapa wenye uhitaji.

Wewe tenga kibajeti kidogo cha 1000 au 2000 kwa wiki yani ukinunua nyanya unaongeza kidogo. Na siku umekwama kabisa unawaambia huna. Ila usiwanyime kama unacho cha ziada. Ile sadaka unayotoa kanisani au msikitini basi usiitoe tena kule kwa sababu tayari utakuwa umeshatoa sadaka yako kwa jirani

Haya maisha huwezi jua kesho yako, hata wao hawapendi kudhalilika, nakuhakikishia ukiwasaidia japo kwa kidogo ipo siku Mungu atakuinua zaidi
Amina.
Sawa sawa na asante sana kwa ushauri wako huu.
Barikiwa sana
 
Sawa nitafanya hivo kabla ya December.
Ila kuna mtoto wake mmoja siku moja aliniambia mie nikihama nimchukue.
Yaani ni huzuni maisha yao
Kila la kheri mkuu, maoni yangu yanaishia hapo kwenye "wewe kuhama"
 
Back
Top Bottom