Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Mimi ni Ke, nishawahi kuwakazia ila najikuta tu nawaonea huruma watoto.
Maana wanakwambia tangu jana usiku walivyokunywa uji na mihogo mpaka mchana huo hawajala
Amua moja kuwahudumia sababu una huruma au kutowahudumia sababu hutaki kero na si jukumu lake.
 
Dah! Hata kama anachepusha hela as long as watoto wanakuja wana njaa na unaweza kuwasaidia na haikuathiri wasaidie tu na Mungu atakubariki. Siku huna waambie sina. Ila pia kama wengine walivyosema sio mbaya ukamshirikisha mume wake ila akijua mtagombana na anaweza kukuzushia unamtaka mumewe.

Ukiona ni kero sana hama. Watoto watano na maisha haya ni taabu kweli kweli. Pia huyo baba mnunulie box la condom!
 
Mkuu kama unavyowapatia vipo ndani ya uwezo wako na havitakuathiri wapatie tu bila kinyongo wala manung'uniko..kama haviko nje ya uwezo wako waambie huna.
Mungu ana makusudi yale kukuweka hapo pamoja nao
Kuna siku napata na nawapa kidogo.
Ila sasa ndio kama imekuwa mazoea.
Yaani haipiti siku.

Wakisikia brenda linanguruma, wanakuja na vikombe niwawekee juice
 
Mfahamishe mumuwe pengine hajui. Ila wakati mwingine hizo ni silka ya mtu. Wewe hauna silka ya kunyima/kukataa/uchoyo. Ivyo utaweza kusema leo hapana kesho wakurudi utakosa ujasiri wa kukataa. Hiyo ndio silka yako ungekua hauna silka hiyo kitambo ungekua ushakata mrija na wasingerudi tena. Kwa kesi ya watoto wezesha tu ambacho kwako hakitogeuka maumivu.
Ndio, huwa sina uchoyo ninapokuwa nacho ila sasa wakati mwingine mpaka naogopa kupika vikanukia
 
Ila jaman wanaume tutafutee Hela tujenge majumba km unapenda kuwa na wtt wengii🤔🤔maana c poa watoto WA 5 +BB na mm n watu 7 Kwenye chumba na seblee aiseé n nooma mazeee
Kabisa.
Yaani chumba na sebule na wako 7.
 
Maisha ni kusaidiana. Kwahiyo, kama wewe unawasaidia vitu hivyo, tafuta namna ya wao wanavyoweza kukusaidia pia. Mkiwa wote mnasaidiana mambo yanabalance. Kama hakuna kitu chochote wanachoweza kukusaidia, unabakiwa na choices tatu; 1. Hama 2. Satisha kabisa mazoea nao. Lakini kumbuka hao ndio jirani ambao ikitokea dharura ndio wa kuwakimbilia. 3. Kubali kutoa sadaka kadri utakavyojaaliwa. Katika hili jifariji kuwa unafanya kazi ya Mungu. Malipo yake anayajua yeye mwenyewe. Unaposhindwa hautoi, ukiweza unatoa.
 
Kuna siku napata na nawapa kidogo.
Ila sasa ndio kama imekuwa mazoea.
Yaani haipiti siku.

Wakisikia brenda linanguruma, wanakuja na vikombe niwawekee juice
Una miaka mingapi hiyo sehemu?
 
Amua moja kuwahudumia sababu una huruma au kutowahudumia sababu hutaki kero na si jukumu lake.
Ndio maana nimekuja hapa kuwaomba ushauri wakuu wangu
 
Dah! Hata kama anachepusha hela as long as watoto wanakuja wana njaa na unaweza kuwasaidia na haikuathiri wasaidie tu na Mungu atakubariki. Siku huna waambie sina. Ila pia kama wengine walivyosema sio mbaya ukamshirikisha mume wake ila akijua mtagombana na anaweza kukuzushia unamtaka mumewe.

Ukiona ni kero sana hama. Watoto watano na maisha haya ni taabu kweli kweli. Pia huyo baba mnunulie box la condom!
Hapo kwa bold naepuka sana.
Nawasaidia hivohivo tu
 
Back
Top Bottom