Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 21,492
- 65,712
Kila la heri MkuuSawa nimekuelewa mkuu.
Kila la heri MkuuSawa nimekuelewa mkuu.
Asante sana.kuna wengine wanajiendekeza tu, , nishawahi kukaa na watu wanaomba mpka dawa ya mswaki nikawa najiuliza hivi hawa mpaka dawa ya mswaki inaisha unakuta haoni au ni makusudi,,, anyway pole Katrina
Tutafute Hela km unapenda wtt alooo😀😀Balaa nakosa picha mimi
Umenikumbusha lake zone nmetoka holiday nikaamua kuchukua house nje ya mji yenye ulitulivu kuna ssta nae kapanga near house ana two children aseee wanaomba hela wale watoto yaaan nilishukuru alivokuja kukosa kodi akahama kinguvuNadhani kuna uzi humu ulikuwa unaelezea kero zinazopatikana katika nyumba za kupanga, mimi kiukweli kero ndogondogo huwa nazitatua mwenyewe ndio maana ule uzi nilikuwa naupitia juu juu tu, ila baada ya kunikuta jambo kwenye hizi nyumba za kupanga ndipo hapo ikabidi niurudie kuusoma ule uzi upya.
Hapa nilipopanga tunaishi wapangaji 3.
1. Mimi.
2. Chumba kingine anaishi kijana mmoja dereva wa gari la mafuta hivo mara nyingi anakuwa nje ya mkoa.
3. Chumba kingine anaishi baba, mama na watoto wake 5 kwenye chumba kimoja na sebule.
Baba akiwa anafanya kazi gereji na mama ni mpika vitumbua.
Sijajua wanalalaje ila mimi naleta kero yangu jamani.
Hii familia imekuwa ni kero kubwa sana kwangu aisee.
Yaani ni wanaomba kuliko unavyodhani.
Hatukatai kama shida ni ya kila mmoja ila ikizidi huwa kero kubwa sana kwa wengine.
Wakiamka tu asubuhi, mama huyo huja kunigongea mlango mara aombe sukari, mara majani ya chai.
Ikifika mchana utasikia umepika nini, naomba kijiko kimoja cha mchuzi nimlishe mwanangu.
Usiku ikifika anakuja mtoto wake mlangoni kwangu na chakula kikavu hata sahani 3 akitaka niwawekee mboga.
Yule baba nadhani anaacha pesa ya matumizi ila sijui ni kwamba haitoshi au sijui kuna nini.
Nikipika mboga au chakula kosa kisinukie, utasikia hodi mlangoni na kibakuli.
Akitoka anawaachia maagizo wanae kuwa wakirudi shule waje kwangu niwape mia mbili mia mbili wakanunue maandazi wakati hajaniachia pesa yoyote.
Yaani wanaomba kila kitu.
Kuanzia asubuhi mpaka jioni
Wakipumzika ni siku 2 ya 3 wako mlangoni kwangu.
Kuna siku nilimuuliza kwani huachiwi pesa ya matumizi.
Akasema anaachiwa ila haitoshi, nikasema si unachoma vitumbua?
Akanijibu matumizi mengi sana ndani kwake hivo nimsaidie tu hivohivo.
Yaani naweza nikawa nimelala au nacheki Tv, nasikia hodi natoka nje nikijua ni mgeni wangu ila nikifungua ni yeye anataka mara kitunguu au nyanya.
Kuna siku niliwahi mwambia kuwa apunguze usumbufu wa kuja kuomba vitu, akapumzika siku 5 tu, ya sita huyu hapa.
Tena sahv anawatuma wanae waje kuniambia kwamba wana njaa niwape chakula
Nina uwezo wa kuhama ila hapa ni jirani na kibaruani kwangu.
Natembea tu na miguu.
Nakaa hapa kuepusha gharama ya safari.
Wazoefu naombeni la kufanya.
Tutafute Hela km unapenda wtt alooo 😀 😀Kabisa.
Yaani chumba na sebule na wako 7.
Sawa sawa mkuu.Maisha ni kusaidiana. Kwahiyo, kama wewe unawasaidia vitu hivyo, tafuta namna ya wao wanavyoweza kukusaidia pia. Mkiwa wote mnasaidiana mambo yanabalance. Kama hakuna kitu chochote wanachoweza kukusaidia, unabakiwa na choices tatu; 1. Hama 2. Satisha kabisa mazoea nao. Lakini kumbuka hao ndio jirani ambao ikitokea dharura ndio wa kuwakimbilia. 3. Kubali kutoa sadaka kadri utakavyojaaliwa. Katika hili jifariji kuwa unafanya kazi ya Mungu. Malipo yake anayajua yeye mwenyewe. Unaposhindwa hautoi, ukiweza unatoa.
Wazungu wskileta uzazi ws mpango tunasema wanataka watuueTutafute Hela alooo
Tafuteni tuwazalie wa kutosha...😃😃😃Tutafute Hela km unapenda wtt alooo😀😀
Sawa, basi endelea kuwasaidia hao watoto hawana hatia. Mungu atakujaalia. Inaonekana ni binti mwenye roho nzuri na unaonekana utakuwa mke na mama bora. Usione ni kero sasa, at least kwa hao watoto.Hapo kwa bold naepuka sana.
Nawasaidia hivohivo tu
Wewe kitu pekee kinachoweza kukusaidia.Nina miaka 2 huu unaelekea mwishoni
Ukiona unaumia ndani usiwasaidie na ukiwasaidia basi chora mstari wa ukomo na wao wajue kabisa huo ukomo sababu kwa historia yetu ya ujamaa msaada unaojirudia hugeuka wajibu na haki kwa anayesaidiwa.Ndio maana nimekuja hapa kuwaomba ushauri wakuu wangu
Ni kero sana aisee.Umenikumbusha lake zone nmetoka holiday nikaamua kuchukua house nje ya mji yenye ulitulivu kuna ssta nae kapanga near house ana two children aseee wanaomba hela wale watoto yaaan nilishukuru alivokuja kukosa kodi akahama kinguvu
Akija TENA fukuuuuuzaaaaaa. Kama una muonea aibu nikodi NIJE NIPIGE KAZI apigwi ahah ILA namchana TU kubebeshana mizigo. Hana nduguSawa mkuu.
Nimekuelewa