Nifanyeje niache tabia ya kujitenga na watu?

Nifanyeje niache tabia ya kujitenga na watu?

Sio lazima uwe karibu na watu!

After all unataka kujifunza nini kwa watu ambao asilimia 90 ya mazungumzo yao ni ngono, udaku na porojo!

Lock yourself in a room and watch a good movie or read a book!

Mimi nadhani uko sawa tu na ndio tabia yako hiyo!

Ukikaa na hawa waswahili watakuambukiza uwezo duni wa kufikiri tu. Hakuna lolote utakalojifunza zaidi ya staili za ngono na kupiga domo forodhani.
Acha kumdanganya mwenzio,maisha ya ubinafsi hayana faida yoyote zaidi ya kuufanya ubongo kuwa dormant, elimu ya mtaani ni muhimu sana kwa ustawi kuliko unavyofikilia
 
Hapo hujamshauri kitu. Anatakiwa awe na marafiki wenye hobbies kama zake. Kama anapenda movies atajenga urafiki wa kuangalia movies pamoja, kama ni mpenzi wa magari ajenge urafiki na wanaopenda magari etc.

Itakuwa rahisi kwake kupata marafiki wa aina yake na sio kulazimisha kujenga urafiki na marafikio sio aina yake.

Sent using Cash Money Wings
Hapo kwenye movies mara nyingi hata mimi huwa napenda saana sijui kwanini?
 
Sasa unachat na nani kama rafiki hupendi kuwa naye?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vijiweni hakuna lolote ka maana.Unapokaribishaa watu ndio unakaribisha matatizi,wivu chuki husda nk.Watu shirikiana nao katika matukio muhimu.
Hivi ukienda kijiweni unaongeza nini? Kama kazi zako hazina mahusiano na mikusnyiko huna haja kupoteza muda kukaa kijiweni kusubiri usiku uingie.
Watanzania tunamaisha Fulani ya kupoteza muda.Mtu anatoka shamba/kazini saa sita, anakula,anaoga anaenda kirabuni,mpirani,kijiwe kahawa au baa.Analewa na kuongea huko mpaka usiku.Waafrika Wengi ndio maisha yao na usipiyafuata unaonekana hauko sawa.Wewe umekomboka hongera!!
 
Hapo hujamshauri kitu. Anatakiwa awe na marafiki wenye hobbies kama zake. Kama anapenda movies atajenga urafiki wa kuangalia movies pamoja, kama ni mpenzi wa magari ajenge urafiki na wanaopenda magari etc.

Itakuwa rahisi kwake kupata marafiki wa aina yake na sio kulazimisha kujenga urafiki na marafikio sio aina yake.

Sent using Cash Money Wings
Rafiki yake atakuwa mke atakaemuoa.Watakuwa wanaangalia movie pamoja.Kukaribisha watu nyumbani ni kukaribisha matatizo, binadmu hawaaminiki.Mimi nimebadirika kutoka kuwa na marafiki mpaka kuwa peke yangu Marafiiki ndio maadui.
 
Habari za mida hii wapendwa

Mimi ni wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto wawili. Katika makuzi yangu tokea Primary School nilikuwa naishi kwa style fulani ya kujitenga tenga na wenzangu. Ikafika kipindi wenzangu niliokuwa nikisoma nao shule wakawa wananiita mimi mchawi.

Kwa mfano labda kama kuna kitu shuleni ambacho kinahusisha wingi wa watu mimi lazima nitatoroka shuleni au kama zile group discussions basi mimi lazima nitajitenga. Nilikuwa sipendi kuwa na rafiki kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anapenda kuwa karibu na mimi lakini ilifika mahali hata akija nyumbani kuniuliza nilikuwa namkwepa.

Sasa wadau tatizo limekuwa sugu hadi sasa hivi nimekuwa sina rafiki hata nikisema nijichanganye kwa watu nakuwa sijisikii kujiamini. Kuna muda nasema labda nianze kushabikia mpira lakini sina muda navyo hivyo vitu kwa kifupi hadi saivi sina rafiki hata mmoja.

Kuna wengine nawaona wanaoenda kuwa karibu na mimi lakini nimekuwa mtu wa kujitenga nao. Kwa kifupi nikienda kazini ya huko nayaacha huko huko nikirudi nyumbani napenda kujifungia ghetto kuangalia movies kuchati nikitoka mgahawani narudi tena mbio nyumbani. Bahati nzuri nyumba niliyopanga niko peke yangu yule mama kashanizoea naweza kukaa na watu nakuwa mpenzi msikilizaji tu siongei neno hata moja, wakinisemesha najibu short ama nakuwa mkali.

Naombeni ushauri jamani, kuna muda nawaza hadi nafika mbali. Kwanini nimekuwa mtu wa kujitenga?
Huna HELA ndo maana unaona unajitenga
 
Kuwa na jamaa,usiwe na marafiki.Ukikaribisha rafiki atapiga hata mkeo au mtoto wako wa kike.
 
Asee sinaga Habari Nawatu Nilipo Panga Naweza Kuwa Ndani na wasihisi Kama nipo Sometimes hadi labda niwashe tv

Huwa inaniwia vigumu Sometimes Lkn Naamini kunaninayo epushwa Maana Dunia yasasa Hakuna Usawa Hakuna Upendo Unaweza lazimisha makundi Ili kujifariji Mwisho Wasiku yakawa Faida kwako au Hasara na Kuharibu kilakitu Katika Maisha Yako

Nandio Maana sipendi makundi Bora ku enjoy my own happiness Kwanza Kuna Corona
Sio Vyema kujichanganya changanya ovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unachat na nani kama si rafiki?

Back
Top Bottom