Nifanyeje nizoeane na majirani?

🤣🤣🤣🤣🤣
 
Jumuiya ya wazazi au
 
Panga matukio ya kujumuika pamoja kisha uwaalike majirani zako, kitu kama birthday yako au watu wa karibu, wakaribishe kwako muangalie pamoja luninga ili mzoeane, hayo ndio maisha ya wenzetu kule mbele.
Kuangalia luninga pamoja😃😃😃 ya zamani kweli hii sasa hivi ukiwasha TV watu wanawasha simu zao wanaona unawayeyusha tu unakuta Jirani ana Dstv analipa kile cha juu mpaka kurekodi anaona unamyeyusha tu.

Achinje mbuzi aalike majirani aweke na bia kadhaa then wengine wake na bottles zao.
 
Watu pekee ambao wanazoeana na kuelewana kwa haraka ni wanywa pombe,kwani maeneo ya jirani hakuna sehemu ya burudani?
 
Huko hakuna balozi wala mwenyekiti wa mtaa!
 
[emoji817]% sahihi
 
Hamna kagrocery hapo karibu? Au mtaa mzima sio wanywaji......wanywaji huwa wanazoeana fasta sana😆
 
Ni bora kabisa kujitenga. Kadri unavyokuwa mbali na wengi,ndivyo unavyokaa mbali na matatizo. Kadri unavyokuwa na marafiki wengi ndivyo unavyokaribia kupata matatizo mengi
Hiyo ni hatari,usalama wako na familia yako ni muhimu sana,hakuna eneo salama siku hizi, jirani yako ni mtu muhimu kuliko kuogopa kuombwa chumvi.
 
Mchawi siku zote hupenda kujichanganya na watu ili apate misukule kirahisi.Majirani stukeni.
 
Uungwana ni vitendo. Siku za weekend pita kwenye nyumba jitambulishe kwamba wewe ni jirani yao upo nyumba namba Fulani let them know you it will help for the future.
Live with your neighborhood closely they will also help you one unknown day
 
Si ajabu wanazo habari zako zote, wadada wanazoeana haraka sana wao kwa wao.
 
Andaa mkutano wa ujirani mwema, ukimpata mmoja atakusaida namba ya mtu mwingine. Mara nyingi kuna watu wanakuwa na mawazo kama yako lakini kama hayupo wa kulianza inakuwa shida.
Hata kwetu tulianza kwa jinsi hiyo.Sasa hivi karibu majirani wote tunafahamiana.
Tulikutana kwa mtu na kununua soda tukanywa tukazidi kupeana taarifa.
Mpate mmoja mshirikishe naye atakupa jina la mwingine. Andaa ujumbe wa mwaliko pendekeza sehemu ya kukutana.

Wàalike siku moja kwa chakula kama majirani wa karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…