Nifanyeje nizoeane na majirani?

Jirani yangu alikuwa mchangamfu sana kabla sijahamia na vitu alinihifadhia yeye na vingine naazima vya ujenzi, tena akisisitiza 'hamia hivyohivyo jirani mbona poa tu?' Nimehamia kawa kauzu na ikitokea tumekutana kwa bahati ananiwekea ukuta kwa kila niliyeanza kuzoeana naye, mara huyu mnafiki huyu mbaya nk nk. I'm baffled.
 

Umetoka Huko uswahilini ...baada ya mwaka umemiss Ugomvi na vijembe siooo Acha uswahiliiiii....Ishi maisha yako acha mazoeeeaaaaaa
 

Au Iko Hivi Wee siku ya Jpili Toka UCHI mchana kweupeee mpaka Yumba ya Nne Huku unaimba wimbo wa Zuchu Yumba Ndogo Kwa sautiii.....


#Tukio la kuwakutanishaaa#
 
Kwenye familia nyingi unakuta Wazazi hawafahamiani lakini watoto wanafahamiana na majirani mpaka majina yao, unaweza kuta wewe huwafahamu lakini mfanyakazi anawajua wote

ikiwa wewe ulifika hapo na ukawakuta wengine ni vyema kwenda japo kusalimia, ni kufahamiana tu ila kusijenge mazoea makubwa kwani kufahamiana kunatosha.
 
Kama wewe ni Muislam basi jitahidi sana swala za jamaa zisikupite na ikiwa mtu wakutoka asubuhi kurudi jioni bc jitahidi swala ya asubuhi na ishai jamaa.hapo utawajua watu wote na pia utajenga nao ukaribu.
 
Vikao vya mtaa?
Hivyo sijawahi kuvisikia huku uswahilini kwetu
 
Jilipue weka ka party alika majirani wote wale na wanywe kana kwamba una birthday
Majiran wa kishua huwapati kwa staili hiyo, hiyo staili unaweza itumia kama umezungukwa na middle class au hawa wa uchumibwa chini kabisa.

Njia rahisi ni kuruhusu wao wakujue kidogo then mengine yatajiset yenyewe,fanya haya kwa wiki tatu then utaona mabadiliko

1-embu tafuta sababu yeyote ya kujuana na mjumbe au mwenyekiti wa mtaa, una weza enda kwake kuomba hata barua ya udhamini unataka kufungua account bank nk... Hakikisha hicho kigezo unakitumia kuonana naye hata mara nne kabla tatizo halijakamilika mazima. Tayar yeye atakua ufunguo wa kukutambulisha wewe kwa wengine bila hata kuomba promo(hii ni kawaida yetu wa tz) jitahid kuwa polite as much as you can, kumbuka ushakaa mwaka bila mawasiliano nao so kuna namna wanakudefine mpaka sasa. Usione maget ukadhan wao hawajuani, wewe ndio huwajuiiiii


2-Siku za weekend asubui toka nje ya geti lako fanya fanya usafi, wakiwa wanapita kutoka kwao lazima watakusalimia na wewe utatumia fursa hiyo kuwajua, ukiwa polite kwa mmoja uka mu empress utashangaa wengine wakikusalia kwa furaha utadhan mnajuana(hapo ndio utajua kuwa wao huwa wanawasiliana)

3-Shiriki matukio ya kijamii taratibu,onesha kuwa nao.Usifanye kwa sifa na usiwe chini ya kiwango... Hutajuta kuwa karibu nao maana watu wa maget hakunaga usumbufu mkubwa hata kama mkijuana maana hukobsio uswazi...



Nb:
Usidharau majirani hata kama si level yako, tafuta namna bora ya kuishi nao pasipo kuharibu kile unachodhan ni sahihi kwako.
Nilishawai ona mtu kapata majanga na akaja kusaidiwa na majirani aliokuwa akiwatukana kupitia kipaza sauti siku moja baada ya sherehe. Yaan kwenye sherehe aliyokuwa nayonalitumia muziki ulebuliokodiwa kupeleka ujumbe kwa majirani waache unafki na kuwasema kwa maneno mabovu kabisa yasiyo na staha lakini keshobyake nyumba ilishika moto na majiran waliamua kuzima moto ule hukubwakiambizana kuwa tumsamehe ilikua pombe. But walichukizwa sana na maneno yake

Tuishi kwa akili na majirani zetu
 

Daah.. huyo muuza duka alizingua kinomaa yaani ulitakiwa baadae umfate ukampe makavu. Vipi kama icho kitu ulichoenda kuulizia wewe kisingekua ni cha home? Mfano ukute una nyumba ndogo ndio umepeleka huko halafu wife anaambiwa mbona mumeo ameshanunua?? 🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Ningekuwa na hizo mambo ningemfata kumchana,ila sina hizo mambo.

Nyumba ndogo yangu ni kuoa tu na nikiona wife lazima ajueπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mnakwama wapi bingwa? πŸ˜‚ πŸ˜‚ hakuna balozi au hata M/Kiti wa mtaa hapo karibu?
Ila kwakuwa wote ni watu mnatoka asubuhi mnarudi jioni kila mtu ndani ya gari ni very simple tu fanya hivi
Kupitia balozi/M kiti wa mtaa unaweza kuandaaa ka-tafrija hapo kwako wakaalikwa najua hawawezi kataa
Hpo mtapata kujuana na kudumisha ujirani mwema. Ni wazo zuri sana kukaa na majirani vyema ni nzuri hii. Ili kusudi kesho ukipata kichwa cha mtu getini kwako usihisiwe kwa lolote baya
 
Achana na mambo ya ujirani mwema, binadamu siyo watu...
 
Nilikua na hari kama yako mda fulani, ila sikuu kuu ya iddi moja nilivaa kanzu na kofia kuenda kuswali tulienda kwa muguu na familia mskitini sio mbali sana wakati wakurudi wengi majilani nilikutana nao, waka nisalimia ustadhi assalamu alykum kumbe wewe ni mwenzetu, nikawa naitikiya.
Uislamu ni raha tangia siku hiyo nimepata majilani na ndg wengi wa kweli wanakuja na mimi naenda kwao na siku ya j2 tunakutana, kupiga stori za hapa na pale, watu wanatafuta majilani wanao endena nao usilazimishe.
 
Wanunulie wanao wa kiume mpira itafanya kuzoeana na watoto wa jiran na ndio mwanzo wa wazaz kufahamiana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…