Jilipue weka ka party alika majirani wote wale na wanywe kana kwamba una birthday
Majiran wa kishua huwapati kwa staili hiyo, hiyo staili unaweza itumia kama umezungukwa na middle class au hawa wa uchumibwa chini kabisa.
Njia rahisi ni kuruhusu wao wakujue kidogo then mengine yatajiset yenyewe,fanya haya kwa wiki tatu then utaona mabadiliko
1-embu tafuta sababu yeyote ya kujuana na mjumbe au mwenyekiti wa mtaa, una weza enda kwake kuomba hata barua ya udhamini unataka kufungua account bank nk... Hakikisha hicho kigezo unakitumia kuonana naye hata mara nne kabla tatizo halijakamilika mazima. Tayar yeye atakua ufunguo wa kukutambulisha wewe kwa wengine bila hata kuomba promo(hii ni kawaida yetu wa tz) jitahid kuwa polite as much as you can, kumbuka ushakaa mwaka bila mawasiliano nao so kuna namna wanakudefine mpaka sasa. Usione maget ukadhan wao hawajuani, wewe ndio huwajuiiiii
2-Siku za weekend asubui toka nje ya geti lako fanya fanya usafi, wakiwa wanapita kutoka kwao lazima watakusalimia na wewe utatumia fursa hiyo kuwajua, ukiwa polite kwa mmoja uka mu empress utashangaa wengine wakikusalia kwa furaha utadhan mnajuana(hapo ndio utajua kuwa wao huwa wanawasiliana)
3-Shiriki matukio ya kijamii taratibu,onesha kuwa nao.Usifanye kwa sifa na usiwe chini ya kiwango... Hutajuta kuwa karibu nao maana watu wa maget hakunaga usumbufu mkubwa hata kama mkijuana maana hukobsio uswazi...
Nb:
Usidharau majirani hata kama si level yako, tafuta namna bora ya kuishi nao pasipo kuharibu kile unachodhan ni sahihi kwako.
Nilishawai ona mtu kapata majanga na akaja kusaidiwa na majirani aliokuwa akiwatukana kupitia kipaza sauti siku moja baada ya sherehe. Yaan kwenye sherehe aliyokuwa nayonalitumia muziki ulebuliokodiwa kupeleka ujumbe kwa majirani waache unafki na kuwasema kwa maneno mabovu kabisa yasiyo na staha lakini keshobyake nyumba ilishika moto na majiran waliamua kuzima moto ule hukubwakiambizana kuwa tumsamehe ilikua pombe. But walichukizwa sana na maneno yake
Tuishi kwa akili na majirani zetu