Ni genetics kwa asilimia chache sana. Sababu kama ni kweli genetics zingekuwa ndio zina-determine intelligence ya kiumbe kwa 100%. Then it means kuna familia na vizazi ambavyo ni wajinga milele. Kitu ambacho ni kinyume na sheria kuu ya nature, Development and specific adaptability to certain environments. So usiwasikilize waliosema Genetics kama kichocheo kikuu cha akilia za binadamu.
Bali kwa kiasi kikubwa intelligence ya binadamu inachochewa na Malezi na Mazingira. Hivyo kumlea mtoto kwa kukuza curiosity yake ya utoto na kumjibu kila swali lake na kumsukuma ili aendelee kuwa hivyo ni njia mojawapo. Badala ya kumfokea kwa kumuona msumbufu. Kwani kufanya hivyo kutam-discourage na kudumaza uwezo wake milele. Ukilinganisha watoto huona wazazi wao kama miungu na kuamini kila walisemalo.
Hapo utaupa nafasi ubongo wake kukua kwa haraka, wanaita brain-plasticity na ku-strengthen neurotransmitters. Hivyo kuzidisha ufikiri na kasi yake, ikiwemo kuongezeka kwa curiosity. Hapo lazima apasue masomo ya darasani ambayo kwa wakati huo wa miaka 6-7 yatakuwa chini yake sababu tayari ubongo umekomaa kupitiliza. Ni kama vile wewe upewe maswali ya 5+5. Vilevile kumfunza lugha za kigeni kama English au Kifaransa zinasaidia kukuza uwezo wake wa kufikiri na kusolve vitu.
Kama kweli unataka kukuza an absolute thinking machine basi, kwenye kipengele cha mazingira itabidi uwe strickt kupitiliza. Ikiwemo kuangalia marafiki anaocheza nao kila siku ni watoto wa aina gani kutoka familia gani ya watu wa aina gani ili kutomchanganya wako na wao na kupelekea kudumaa kwa ufikiri, curiosity, utambuzi na brain-plasticity inayochochewa na new informations.
Hapo bado hujachelewa kama bado ni wadogo. Kujibu maswali, kujifunza na udadisi isiwe shule tu. Bali maisha yao ya kila siku.
Vilevile fimbo hazisaidii kitu bali hubomoa tu kwa kumpa mtoto uoga na kumuaminisha yeye hawezi kufanya ulichomwambia kwani njia pekee ni kuelewa. Kitu ambacho sio kweli, sababu mara nyingi mzazi na mwalimu ndio wenye makosa yanayosababisha mtoto kutokuelewa.
Na vilevile mazoea ya mzazi na mtoto. Kama mwanao unamlea kama mbwa kazi yako ni kumpa chakula na kumkaririsha kanuni za hisabati. Basi usitegemee huyo mtoto kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri.
Kukaa nae muda mwingi, kucheza nae, kuongea nae kama mtu mzima, na kuwa na mazoea naye kama rafiki ndiyo njia pekee ya kujua akili ya kweli ya mtoto na kujua utaikuza vipi. Matter of fact, watoto wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na ufaulu mkubwa darasani, wengi ndivyo walivyolelewa hivyo. Otherwise ni kazi bure.
Dogo langu anapasua 100% kwenye kila mtihani bila hata kutumia nguvu. Na hata mimi nilikuwa nafaulu mitihani bila hata ya kusoma na kukesha usiku kucha kama wale mabaharia wa mabeseni.
Simply sababu uwezo wa kufikiri na uwezo wa kusolve makubwa ulikuwa mkubwa, hivyo viswali vya mitihani ni kama kumuuliza mtu mzima 1+1.
Kuna thread niliandika a few years back inahusu why Africa haina maendeleo, nenda kaicheck. Nimeelezea baadhi ya haya mambo.