Nifatilie toka shambani kilimo cha mahindi, maharage na alizeti hatua kwa hatua

Msimu huu wa kilimo ntakua natoa maelezo ya kitaalamu na picha live toka shambani kwa vitendo kuanzia kuaandaa shamba, kuchagua mbegu, kupanda, kuzuia wadudu na magonjwa, mbolea, kupalilia hadi kuvuna endelea kunifatilia.
Hayo mazao yanalimwa nchi nzima, kuna baadhi ya maeneo unakuta mtoto wa darasa la 3 ana shamba lake la mahindi na kafuata kanuni zote,ukiona hadi leo kuna mtu hajui mahindi yanalimwa vipi na yanatunzwa vipi huyo sio mkulima ni wale wakulima wa mwendo kasi wako kwenye AC wanalima kimawazo
 
Mkuu kuna kulima na kupanda. Watanzania wengi wanapanda mahindi sina haja ya kukuwekea picha. Zunguka mashambani ujionee ukulima uliopitwa na wakati.
Nakwambia wakulima wangelima kisasa umasikini TZ tungeisha uaga.
Kuna mwalimu wa mkenya ambae amewekeza kulima kilimo cha kisasa HUVUNA GUNIA 35 KWA HEKA 1.
Njoo kwetu je wakulima wetu wanafikisha hata gunia 20 kwa heka ? Wakijitahidi 15.
Nimejifunza formula za huyo mkenya, analima tofauti na sisi.
Kwa hio usirudie kusema eti kila mtu anajua kulima mahindi sema kila mtu anajua kupanda mahindi. Kupanda ni simple tu, unachimba shimo unaweka mbegu unasubiri mavuno, hao ndio wakulima wa TZ.
 
Ile dawa ya wadudu wanaotoboa majani ya wadudu inaitwaje? Inawekwa muda gani baada ya kuotesha?
Ekari moja inatumia kiasi gani na bei yake ikoje?
 
Tupe somo la kupata hizo gunia 35 mkuu.
 
Tupe somo la kupata hizo gunia 35 mkuu.
Mkuu mpaka ntakapo lifanya practically nikifailu nitadocument na video na kuwauzia.
Lakini unaweza ukatafut tu njia yako try and error mpaka ukapata fomula yako.
Tatizo mnakuwa hampo serious, nimewahi weka link kwenye uzi mmoja humu.
This year nimefeli kwenda shambani, njia ya mkenya inahitaji maandaizi makubwa ya samadi, na ukiisha lima mara moja mpaka miaka mitatu ipite we ni kupanda tu, kwa hio ni kilimo kisicho na gharama.
Ntaanza maandalizi mwezi wa 5 na kudocument kila kitu hadi sauti za ndege.
Kwa hio vuta subira, siwezi kukupa utajiri kabla mimi sijaupata.
 
Jamani km kawaida nimerudi tena kutoa mrejesho live kutoka shambani. Hiyo ni Tembo 719,nimeipanda tarehe 12-12-2023. Pia sehemu ingine kwa mbali kidogo nimepanda DK 777 na Panar 691.Lengo la kupanda mbegu zote 3 ni kutaka kujifunza uzuri na mapungufu ya kila mbegu. Nmepanga pia kupanda maharage humo humo shambani( intercroping) baada ya sikukuu. Karibuni kwa maswali,au maoni.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Wakuu natoa mrejesho km kawaida. Hapa ndipo yalipofikia mahindi,nilipandia samadi tu bila mbolea yoyote. Wiki ijayo naweka mbolea ya CAN shughuli inakua imeisha. Picha ya kwanza ni jinsi mahindi yalivyokuwa wiki ya pili toka kuota. Na hizo picha zingine ndo yalivyo sasa.Mungu ni mwema

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Safi mkuu
 
Msimu huu wa kilimo ntakua natoa maelezo ya kitaalamu na picha live toka shambani kwa vitendo kuanzia kuaandaa shamba, kuchagua mbegu, kupanda, kuzuia wadudu na magonjwa, mbolea, kupalilia hadi kuvuna endelea kunifatilia.
Safi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…