Mkuu kuna kulima na kupanda. Watanzania wengi wanapanda mahindi sina haja ya kukuwekea picha. Zunguka mashambani ujionee ukulima uliopitwa na wakati.
Nakwambia wakulima wangelima kisasa umasikini TZ tungeisha uaga.
Kuna mwalimu wa mkenya ambae amewekeza kulima kilimo cha kisasa HUVUNA GUNIA 35 KWA HEKA 1.
Njoo kwetu je wakulima wetu wanafikisha hata gunia 20 kwa heka ? Wakijitahidi 15.
Nimejifunza formula za huyo mkenya, analima tofauti na sisi.
Kwa hio usirudie kusema eti kila mtu anajua kulima mahindi sema kila mtu anajua kupanda mahindi. Kupanda ni simple tu, unachimba shimo unaweka mbegu unasubiri mavuno, hao ndio wakulima wa TZ.