Niffer atoa majibu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka akamatwe kwa uchangishaji wa fedha kwa ajali ya maafa Kariakoo

Niffer atoa majibu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka akamatwe kwa uchangishaji wa fedha kwa ajali ya maafa Kariakoo

Niffer ni mjanja sana kwenye mambo ya pesa ndio maana anatajirika haraka haraka

Hela za michango ya wahanga. Zinatumwa kwenye Lipa namba zenye jina lake.

Halafu idadi ya waliotuma pesa haijulikani. Majina yao na kiasi walichotuma hakiwekwi wazi. Yaani Hakuna Auditor

Kwa jinsi wa Tanzania walivyo wajinga. Huyu dada angepata mtaji mkubwa sana wa biashara zake kupitia hiyo michango.

Kwenye page yake ana wafuasi milioni moja na nusu. Imagine wafuasi Laki 5 tu. Wakituma shilingi elfu moja moja kila mmoja.. Niffer anakusanya milioni 500 fasta fasta.

Hapo anapeleka kwa wahanga milioni 200 kisha 300 anazibana.

Hakuna atakaye gundua
Nawewe ni wale wale tu huna hoja kwani kuwa na follows wengi ndio kupata hela hujui kama watanzania wengi ni malimbukeni wa mitandao wanamfollow mtu tu bila sababu
 
Mfanyabiashara maarufu Jennifer Jovin, anayefahamika kama Niffer, ametoa majibu yake baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kumtaja katika hotuba yake ya hadhara akitaka afuatiliwe na kueleza nani aliyempa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia ajali ya kuporomoka kwa gorofa la Kariakoo.

Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

Kupitia majibu yake yaliyojaa shukrani na kueleza nia njema, Niffer amesema:

"Kwanza kabisa, Alhamdulillah, namshukuru sana Allah kwa kunipa nafasi ya kuiona siku ya leo. Kwa kweli, ni jambo kubwa sana kwangu kuona Waziri Mkuu wa nchi yangu ametaja jina langu mbele ya hadhara ya watu mashuhuri. Hii ni ndoto kubwa iliyotimia kwa ulimwengu wa roho."

Niffer ameeleza kuwa nia yake kuu ilikuwa kusaidia wahanga wa ajali hiyo, akisisitiza kuwa hakujua sheria zinazohusiana na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya mafaa kama hayo. Ameeleza:

"Nilikuwa tayari tangu mwanzo kutoa ushirikiano kwa Serikali na jamii kwa ujumla. Niliomba muongozo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza zoezi hili. Ninaamini nia yangu haikuwa mbaya, na kupitia changamoto hii, nimeona umuhimu wa kuwa na taasisi inayotambulika rasmi, Niffer Foundation."

Waziri Mkuu Majaliwa, wakati akizungumza eneo la Kariakoo, alisisitiza kuwa hakuna mtu anayepaswa kuchangisha fedha bila kibali maalum kutoka serikalini na akatoa agizo kwamba Niffer atafutwe ili aeleze ni nani aliyempa mamlaka hiyo.

Soma, Pia: Jeshi la polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo

Baada ya agizo hilo, taarifa zilitolewa kuwa Niffer ameshapatikana na yuko tayari kushirikiana na mamlaka husika.
Mbona kama analalamika
 
Hadi hili sakata lifike mwisho kuna mtu au watu kadhaa watanufaika na lile tako. Ni fursa ya wenye maamuzi kupata utelezi. Niffer anatakiwa kuelewa sio tatizo kucheza na Kasim ila ni hatari mno kucheza na Waziri Mkuu. Mungu amlaze pema hayati EL kwa kusisitiza elimu.
Wanufaike mara ngapi sasa? Wapya au?
 
Kungekuwa na sheria za wazi na zinazojulikana kuhusu fundraising.

Mfano, kuna nchi zinataka mtu anayechangisha awe na foundation na awe anaripoti mapato na matumizi wazi kwa taasisi ya kukusanya kodi na kwa wananchi.

Ni kweli kwamba kutojua sheria si excuse ya kuvunja sheria, lakini pia, sheria isiyojulikana ikivunjwa ni rahisi kwa wananchi kumuonea huruma aliyevunja sheria.

Zaidi, jamii yetu imekaa kuhukumiana zaidi ya kusaidiana. Mtu kama Niffer angeunganishwa tu katika efforts za serikali za kukusanya michango.
Hizo hela angeishia kuzila kama wenzake wanavyokula
Nchi hii kila mtu mwizi mwizi mwizi

Ova
 
Hizo hela angeishia kuzila kama wenzake wanavyokula
Nchi hii kila mtu mwizi mwizi mwizi

Ova
😄😄 ila sisi wabongo kwenye upigaji huwa hatutumii akili. Kuna jamaa alikuwa na club yake ya riadha ambayo ilikuwa ina udhamini mnono toka Marekani. Alikuwa akitumiwa kontena zima 20×20 la raba achilia mbali pesa kibao za kuendeshea club. Yule mtu aliishia kuelekeza pesa kwenye biashara zake huku lengo halisi akilitelekeza. Wamarekani wakaondoa udhamini wao TZ na kuuelekeza Kenya ambapo huko wamefanya makubwa hadi kujenga hospitali.
 
Aise wabongo kwa uwizi tuko vizuri

Ova
 
Jambo limekugusa tafuta wahusika physically au namba zao moja kwa moja utoe swadaka yako lakini hii ya kusema kuna mtu sijui taasisi anachangisha kwa nchi zilizojaa ufisadi na ubadhirifu wala usijisumbue!
 
Niffer ni mjanja sana kwenye mambo ya pesa ndio maana anatajirika haraka haraka

Hela za michango ya wahanga. Zinatumwa kwenye Lipa namba zenye jina lake.

Halafu idadi ya waliotuma pesa haijulikani. Majina yao na kiasi walichotuma hakiwekwi wazi. Yaani Hakuna Auditor

Kwa jinsi wa Tanzania walivyo wajinga. Huyu dada angepata mtaji mkubwa sana wa biashara zake kupitia hiyo michango.

Kwenye page yake ana wafuasi milioni moja na nusu. Imagine wafuasi Laki 5 tu. Wakituma shilingi elfu moja moja kila mmoja.. Niffer anakusanya milioni 500 fasta fasta.

Hapo anapeleka kwa wahanga milioni 200 kisha 300 anazibana.

Hakuna atakaye gundua
Screenshot_20241019_045638.jpg
 
Asilimia kubwa ya watu wanaofanikiwa ni wale wanaojua kusoma mazingira fasta na kugeuza situations ie:tragedies into opportunities.
Kama dogo truly amejiongeza basi kongole nyingi kwake.
 
Back
Top Bottom