Niffer: Nilianza na mtaji wa elfu 40, sasa hivi nashika hadi milioni 150

Mlimbwende kunako kiwanda cha Utangazaji, Mjasiriamali na mwanamitandao maarufu Bongo, Niffer Jovin, maarufu kama "Niffer" amefunguka namna alivyohaha kujitafuta hadi kufikia mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo.

Niffer ambaye ametimiza miaka 24 mwaka huu, amesema safari yake ya kuutwaa utajiri haikuwa rahisi kama watu wanavyodhani, amesema yeye ni miongoni mwa watu waliotokea katika familia za kimasikini ambazo asubuhi unalazimika kula maembe badala ya kunywa chai, mrembo huyo amesema amewahi kwenda shule bila viatu, amewahi kupigwa kisa tu kukosa sabuni ya kufulia sare zake za shule, lakini pia alikuwa akimuona mama yake namna alivyokuwa anawahangaikia ili wapate chochote kitu na wakati mwingine alikosa kabisa, amesema hiyo ndiyo ilimpa chachu ya kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba ili asipite walimopita familia yake.

Kama ulikuwa unadhani mtaji wa duka kubwa la Niffer "Niffer Outfitstore" lilianza na mtaji wa mamilioni kadhaa unajidanganya, mpambaji huyo amesema hakuanza na mtaji wa milioni, laki moja wala elfu 50, amesema alianza na elfu 40 pekee na haijamchukua muda mrefu tayari amekuwa tajiri kwa mtaji huo mdogo wa nyanya chungu na vitunguu.

Siri kubwa ya mafanikio ya Mwanaharakati huyo wa maisha amesema ni kuwa na nidhamu na pesa, kuwa na marafiki wa kukujenga, kumuomba Mungu huku ukifanya kazi, kwani yeye wakati anajitafuta alikuwa anafanya biashara hadi saa nane, saa tisa za usiku wa manane. Muhaya huyo wa Bukoba amesema watu wanamshangaa kwa kuwa na duka kubwa akiwa na miaka 24 kwasababu hawajui namna alivyopambana kwa bidii kuyasaka mafanikio.

Amemalizia kwa kuwashauri wasichana wenye umri mdogo na wanawake ambao umri umeenda na bado wanahaha kutafuta maisha kwamba wafanye kazi kwa bidii, waache kubwabwaja mitandaoni kufatilia maisha ya watu na badala yake wautumie huo muda wauze hata pilipiii mbuzi watafika alipofika yeye.
Haya mahesabu ya 40k mpaka milioni 150 yamekaaje kibiashara?
Tena mtu akiwa na umri mdogo hivyo 24 years!?
Tusitaniane bhanaa hapa kuna mengine ya kando yalifanyika.
 
Niffer Mall .

Nilichoona amehamia sehemu nyingine pakubwa zaidi.

Yeye mwenyewe ndio alisema kwamba TRA wamemzingua hivyo anafunga kwa muda.

Ndio maana wasanii wakiwa na shida wakiongea watu hawatochukulia serious kwasababui issue nyingi wanazoongea ni kutafuta trending/kiki.

All in all ,nachoona hapo watu wakubwa wamejoin naye nyuma ya pazia na kumtanguliza Niffer(wamepata share) hivyo kumuongezea msingi kama walivyofanya kwa Dayamondi aka Zombie.
Uko sahihi 100%. Wakubwa wengi wana hela nyingi za kifisadi ambazo zinawapa wakati mgumu sana jinsi ya kuzitumia kwasababu wakikaa nazo pia ni hatari. Niffer akitulia anaenda kuwa mwanamke tajiri sana katika umri mdogo. Tusishangae hata hilo jengo akalinunua miaka michache ijayo.
 
Mlimbwende kunako kiwanda cha Utangazaji, Mjasiriamali na mwanamitandao maarufu Bongo, Niffer Jovin, maarufu kama "Niffer" amefunguka namna alivyohaha kujitafuta hadi kufikia mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo.

Niffer ambaye ametimiza miaka 24 mwaka huu, amesema safari yake ya kuutwaa utajiri haikuwa rahisi kama watu wanavyodhani, amesema yeye ni miongoni mwa watu waliotokea katika familia za kimasikini ambazo asubuhi unalazimika kula maembe badala ya kunywa chai, mrembo huyo amesema amewahi kwenda shule bila viatu, amewahi kupigwa kisa tu kukosa sabuni ya kufulia sare zake za shule, lakini pia alikuwa akimuona mama yake namna alivyokuwa anawahangaikia ili wapate chochote kitu na wakati mwingine alikosa kabisa, amesema hiyo ndiyo ilimpa chachu ya kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba ili asipite walimopita familia yake.

Kama ulikuwa unadhani mtaji wa duka kubwa la Niffer "Niffer Outfitstore" lilianza na mtaji wa mamilioni kadhaa unajidanganya, mpambaji huyo amesema hakuanza na mtaji wa milioni, laki moja wala elfu 50, amesema alianza na elfu 40 pekee na haijamchukua muda mrefu tayari amekuwa tajiri kwa mtaji huo mdogo wa nyanya chungu na vitunguu.

Siri kubwa ya mafanikio ya Mwanaharakati huyo wa maisha amesema ni kuwa na nidhamu na pesa, kuwa na marafiki wa kukujenga, kumuomba Mungu huku ukifanya kazi, kwani yeye wakati anajitafuta alikuwa anafanya biashara hadi saa nane, saa tisa za usiku wa manane. Muhaya huyo wa Bukoba amesema watu wanamshangaa kwa kuwa na duka kubwa akiwa na miaka 24 kwasababu hawajui namna alivyopambana kwa bidii kuyasaka mafanikio.

Amemalizia kwa kuwashauri wasichana wenye umri mdogo na wanawake ambao umri umeenda na bado wanahaha kutafuta maisha kwamba wafanye kazi kwa bidii, waache kubwabwaja mitandaoni kufatilia maisha ya watu na badala yake wautumie huo muda wauze hata pilipiii mbuzi watafika alipofika yeye.
Safi sana Dr Niffa
 
Hata mimi nilianza na mtaji wa elfu 50 nikawa nanunua majeneza used ya wizi nayapaka rangi nauza upya lakini sasa hivi mradi umekuwa mkubwa kiasi kwamba nimekuwa msambazaji mkubwa wa majeneza ndani na nje ya nchi!
Pamoja na kwamba sikumaliza hata shule ya msingi niliishia darasa la nne nikafeli (sikuwa na akili)
Lakini leo hii kampuni yangu imeajiri wasomi
🤣🤣🤣 Hauuzi na Sanda Used mkuu?
 
Biashara ukiwa na juhudi lazima ufanikiwe, wanaolalamika biashara ngumu hao wazembe.

Me nilikuwa tu na wazo la biashara, sikuwa hata na mia lakini nikaweka juhudi hatimaye namiliki biashara kadhaa za mamilioni hapa mjini.
Depal Carleen Darlin shosti yenu anatumia id gani mbona kaadimika sana humu?
 
Ulimi unaponza kichwa. Ukimya nao unasaidia ana attract attention itakayomsumbua!
 
Biashara ukiwa na juhudi lazima ufanikiwe, wanaolalamika biashara ngumu hao wazembe.

Me nilikuwa tu na wazo la biashara, sikuwa hata na mia lakini nikaweka juhudi hatimaye namiliki biashara kadhaa za mamilioni hapa mjini.
Bro kam mungu amekupa shukuru kwa imani yko ila usisem watu wazembe kuna watu wanapamban sna.so kufanikiwa sio ujanja wko pia sio kwamba wew ukifanya sna kazi ila time yko ilikuwa imefika we mshukuru mungu kwa apo ulipo usione wasio fanikiwa ni wazembe bro unakosema
 
Uzi umefufuka simu kakabidhi kwa ukaguzi, ila nifer anajiamini sana sijui nani anampa hiyo jeuri ata kama pesa ipo.
 
Back
Top Bottom