Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Apa labda ufungue duka la beer tu uwakala ni pesa ndefu asee ila duka inaweza kutosha japo bdo n ndogo naongea hvyo kwa experience sibahatishi
Mkuu, napendaga sana biashara kama hii ambayo capital haiathiriki kabisa, unakuwa unahesabu net profit tu kwa kiasi chochote tu. Nipe mauzoefu katika eneo hili mkuu, inbox please!!
 
Mkuu me naomba kuuliza hivi ni gharama ngapi inahitajika kupata eneo ndani ya chuo kufanya biashara

NB: eneo la kujenga kama frem[emoji120]
Kwema mkuu, nilichokua namshauri sio kupata fremu Bali ni kufungua chuo. Kwa shilingi million 12 nimemshauri afungue chuo kitakachosajiliwa chini ya nacte. Na kwavile ndio anaanza itambidi akodi jengo ikiwezekana akodi floor moja au mbili katika ghorofa, afanye renovation afanye marketing. Usajili sio tatizo siku hizi wako faster Sana ukiwa umejiandaa kwa jengo na vifaa vidogo vidogo. Kumbuka hiyo 12mil ni kwa ajili ya mwanzoni tu. Ukikamilisha Ada itafanya mambo mengine
 
Hujanielewa mkuu me nauliza labda kwa experience yako kupata eneo ndani ya chuo kufanya biashara kama ni kwa njia ya kujenga frem au kuweka container huwa ni bei gani???.....
 
mimi nawazo la biashara tukikubaliana nakuuzia kwa ela yako inatosha kabisa kuliendeleza mimi ninamambo kibao nayoyafanya kwa sasa alafu wazo tu lipo silifanyi kazi
 
Hujanielewa mkuu me nauliza labda kwa experience yako kupata eneo ndani ya chuo kufanya biashara kama ni kwa njia ya kujenga frem au kuweka container huwa ni bei gani???.....
Ok nimeelewa mkuu, hiyo inategemea na makubaliano kati yako na uongozi wa chuo. Kwa vyuo vya serikali hua kuna utaratibu wa kutoa tender kwa suppliers. Kwa mfano unataka ufungue canteen ili staff na wanafunzi wapate huduma ya chakula, kwa kawaida chuo husika kinatakiwa kutangaza tender na supplier wanaomba tender, bodi ya manunuzi ya chuo itashindanisha suppliers wote ili kuchagua supplier alie bora. Akishapatikana supplier bora kinachofuata ni mikataba kwa ajili ya kuanza kazi. Process hii ni standard procedure, vyuo vingi vya serikali havifati bali wanatoa tender kwa kujuana. Tena wakati mwingine biashara zinazowekwa chuoni zinamilikiwa na watumishi wa vyuo hivyo. Kwa vyuo binafsi ni maelewano tu na uongozi wa chuo husika japo huko pia hali sio tofauti Sana.
 
Mkuu nakushauri hizo pesa uziache bank itakuwa unakula polepole...katika dunia hii hakuna biashara yenye risk free kwamba kama unavyosema wewe always mtaji utakuwa salama ...narudia tena acha kabisa kufanya biashara yoyote endelea kula mshahara tu biashara hutoiweza.
 
Makadilio ya kwenye vyuo vya private uliwah kuckia unisaidie
 
Gharama za viroba vya kuwekea,

Gharama za kukusanyia (kuubeba toka majumbani mwa watu hadi center ya kukusanyia) huo mpunga huko vijijini.

Gharama ya usafirishaji kuuleta mjini.

Gharama za kupakia na kushusha.
 
You are a such best mathematician bro, japo wadau wanasema hesabu za kwenye makaratasi huwa zinatofautiana ukienda kwenye field
Hajaweka :
Gharama za viroba vya kuwekea,

Gharama za kukusanyia (kuubeba toka majumbani mwa watu hadi center ya kukusanyia) huo mpunga huko vijijini.

Gharama ya usafirishaji kuuleta mjini.

Gharama za kupakia na kushusha.

Quote
 
Gharama za viroba vya kuwekea,

Gharama za kukusanyia (kuubeba toka majumbani mwa watu hadi center ya kukusanyia) huo mpunga huko vijijini.

Gharama ya usafirishaji kuuleta mjini.

Gharama za kupakia na kushusha.
Ila ukija kutoa gharama za kuhifadhi mpunga na kukoboa haizidi TSH. 5,000,000/=,hivyo bado net profit itabaki kama 10,000,000/= katika miezi mitano yako ya uvumilivu

Sexless hiyo 5,000,000/= hapo juu inamaliza kitu, nikitulia nitakupa mchanganuo wa wa hizo gharama zake za kupakia na kushusha
 
Asante mkuu. Nimekusoma. Shukurani kwa ufafanuzi mzuri
 
Umemaliza mtaji (tshs 12,000,000/=) kununua gunia 240 za mpunga . Atapataje hiyo tshs m5/= za kukoboa nk!?
 
Umemaliza mtaji (tshs 12,000,000/=) kununua gunia 240 za mpunga . Atapataje hiyo tshs m5/= za kukoboa nk!?
Mkuu kwenye mchakato wa kukoboa mpunga, kwanza Magunia unaweza kuhifadhi kwenye store ya mwenye mashine kwasababu ana uhakika wa kupata hiyo kazi na hivyo ndio huwa tunafanya.

Kuanzia siku ambayo umehifadhi mpunga wao kwake, huwa kuna wanunuzi wa mchele kutoka nje ya nchi wanafika kwenye hizi mashine kwa lengo la kujipatia mzigo na kwasababu ww umehifadhi pale mpunga wako utapigiwa simu kwamba mnunuzi amepatikana na kama hauupo tayari utasema na utaendelea kusubiri hadi kipindi ambacho unaona upo tayar kukoboa

Mpunga ukisha kobolewa kuna chenga za mchele huwa zinapatikana kwa kila gunia moja la mpunga linatoa debe moja la chenga za mchele na linauzwa minimum ni 15,000 hadi 20,000/= kabisa na wanunuzi wa hizo chenga ni kina mama huwa wapo nje ya mashine kwa ajili ya kuzikusanya hizo chenga na huwa wanaweka oda hata kabla haujaanza kukoboa, kwahyo automatic pesa ya kukobolea huwa inatoka kwenye chenga za mchele

Na kama utakuwa tayari kuuza kwa jumla mchele wako, basi wanunuzi huwa wanafika palepale kwenye zile mashine

Hii biashara pesa huwa inajitengeneza yenyewe ila ukiwa umekaa kwenye kiyoyozi huwezi kuelewa ninachokieleza hapa coz utaona kama napiga hesabu rahisi.
 
Da
Dah... Najaribu kushare link nashindwa.... Ila kuna uzi mmoja hum kuhusu biashara ya mbuzi ni mzuri sana.... Ndo hivi sasa nipo naupambania (ukiwa interested karibu Pm)
🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
mimi nawazo la biashara tukikubaliana nakuuzia kwa ela yako inatosha kabisa kuliendeleza mimi ninamambo kibao nayoyafanya kwa sasa alafu wazo tu lipo silifanyi kazi
kama unahisii hilo wazo litatemesha mkwanja wa uhakika...nami naomba unishirikishe mkuu, nione kama linatekelezeka kwa upande wangu...mimi nipo Zanzibar, kama wazo lako ni useful nipo tayari kulinunua pia km ambavyo umepropose
 
Mkuu kwenye mchanganuo wako wa wa hii biashara ulisema mchele sokoni bei yake unarange kwenye 35000/ kwa debe..hii ni bei ya soko la wapi? Au wanunuzi ndo huwa wanakuja hapo hapo mashineni kuja kuununua kwa bei hiyo?
 
Mkuu kwenye mchanganuo wako wa wa hii biashara ulisema mchele sokoni bei yake unarange kwenye 35000/ kwa debe..hii ni bei ya soko la wapi? Au wanunuzi ndo huwa wanakuja hapo hapo mashineni kuja kuununua kwa bei hiyo?
Yaah mkuu, hiyo ni bei ya kuuzia mashineni ambapo wanunuzi ndio hufika hapo, hasa kwa mpunga kutoka Bonde la kamsamba upo vizuri sana, na watu wengi kwa ukanda ule wanaenda kukobolea Tunduma

Mchele huu ndio kilo yake huwa inafika minimum kwa kilo ni Tsh. 1800/=

Ila kuna wenye uwezo wa kuleta mchele hadi Dar es Salaam hadi Zanzibar hawa ndio wanapata faida kubwa sana

Pia unaweza kufungua store yako kwa ajili ya kuuza mchele wako kidogo kidogo, pia kunakuwa na maharage (mchele hauozi wala maharage haya haribiki kirahisi)

Kwahyo unakuwa una kusanya mpunga wako kwa ajili ya kukoboa na kuuza kwenye store yako mwenyewe ya nafaka

Wali maharage ukishajua ni namna gani hiki ni chakula pendwa basi utajua ni namna gani pesa inapatikana hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…