Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Vipi kuhusu usalama wa huyu mdudu? Maana najua kutokana na nature yake itabidi ufugie nje ya mji. Hayo mabanda itabidi uwe unafunga mageti? Au itabidi uajili suma jkt walinde? Muongozo wako mkuu. Ahsante
 
Biashara nyepesi na yenye hela nyepesi ni hiyo ya kuweka mpunga store.


Ongea vzr na huyo wa kuweka mazao store ukitulia vzr ukaweka 10M tu kama umefeli kbs lazima upate 8M within 6-7 months
 
Acha uongo
 
Umetisha mkuu nikiokota hela ntakufata unipe ushauri hizo biashara ndogondogo ni zipi
 
Pumbavu
 
Yaniii bro ukianza na mil 8 tu unabeba mazaga ya kutosha huko dubai balaaa yaniii
Sasa kaka hyo mil8 unayosema, nauli kwenda na kurudi toka dubai ni mil2.5, kukaa kule labda siku4 inabid uwe na mil 1.5, yani kutembea, pa kulala na chakula
Apo unabaki na mil4, usafirishaji bandalin, tuseme ni mil1 kusafirisha mizigo, sasa apo kweli hako kamzigo katakuletea faida kweli
 
Hujaweka gharama za usafirishaji ndugu, kwa hi
Yo idadi ya mchele usafirishaji ni kama mil5, na bado kwa bei hyo ya 19400 kwa kilo, yaani 35000 kwa debe maana yake ni bei ya madukani na bei ya kuuzia katika thirdy party buyer, ko kuna bei ya kuuzia wauzaji, kitu ambayo wewe ndiye,inakuaga chini zaidi
Ungekuwa umeifanya ungefaham haya
 
Ww hauna kitubkama hicho maana kule watu wanachukua apartment kwa kuchangia na hazifiki hyo gharama unasema ww pili kama unaenda kwa ajili ya kufata mzigo unafanya jambo moja tuuu kama unaenda kwa ajili ya kula bata sawa watu wanaenda na mil 5 na wanarudi na mzigo wa kutosha tuuuu pia wanasafirisha na agent simple tuuu mzee baba uliza vizuri alafu ndo uanze kuwatisha wanaotaka kutoboa life

Over

@@stoplight
 
Ni vizuri ku aim high, ila Brother kwenye biashara kuna concept ya prudence inayosema do not overestimate the amount of revenues recognized or underestimate the amount of expenses.
Maana umetaka upate net profit kubwa sana.
 
Ni vizuri ku aim high, ila Brother kwenye biashara kuna concept ya prudence inayosema do not overestimate the amount of revenues recognized or underestimate the amount of expenses.
Maana umetaka upate net profit kubwa sana.
Umezungumza vema. Twende kwenye uhalisi sasa, hivi investment ya 14milioni kwa sasa mtu ategemee kuzalisha faida ya kiasi gani kila mwezi. Ikiwezekana tutajie hizo projects zinazoweza kuzalisha hayo makadirio yako ya faida kwa mwezi au share with us projects ulizowahi kuzifanya versus faida zake. Hata kama faida itaonekana baada ya mwaka, au miaka 2, kokotoa utuambie hiyo pesa bila kupepesa macho unadhani ina uwezo wa kuzalisha faida kiasi gani kwa kila mwezi.
 
Biashara nyepesi na yenye hela nyepesi ni hiyo ya kuweka mpunga store.


Ongea vzr na huyo wa kuweka mazao store ukitulia vzr ukaweka 10M tu kama umefeli kbs lazima upate 8M within 6-7 months
Mpunga unaujua vizuri au unausikia tu, mpunga ukikatika vizuri unaweza tamani kufa hasara yake.
 
Kambaku, wapo wanao ingiza zaidi ya hiyo, bado tu hunaziona fursa, kila project ina expectations zake. Tuwasubiri wadau watupe mawazo. Usisahau pia kuwa mtaji wa mil. 12 sio kidogo
Kwann usiende kufanya hizo hizo wanazofanya wenzio wanapata faida zaidi ya milion 2 kwa mwez
 
Mkuu wacha kumpotosha kijana. Mimi ninafanya biashara hii kwa muda Sasa, hesabu ulizompatia hapa ni hesabu za biashara ya PDF. Kwanza kabisa hakuna gunia la mpunga la Debe 6 linalo toa Debe 3 za mchele na Debe moja la chenga hakuna. Ukweli ni kwamba gunia moja la Debe 7 la mpunga mzuri Sana hutoa wastani wa Debe 3 tu za mchele. Unapo panga kufanya biashara hii Kuna gharama zake na inategemea unanunulia wapi Mfano kwa bondevla Ziwa Rukwa maeneo ya Kamsamba na Kilyamatundu ni kama ifuatavyo;
1. Gunia la Debe 7 =50,000
2.Gharama ya anaye kununulia @ gunia 2000
3 Gharama ya kupima ni maelewano wastani ni 500 @ gunia
4.Mfuko wa Debe 7=1000
5.Gharama za kibali Cha ununuzi wa mazao 50,000
6. Kupakia na kushusha @ gunia 1000
7. Usafiri kutoka kijijini mpk store 7000@ gunia
8. Ushuru wa halmashauri ni 2000@gunia
9.Kuhifadhi gunia moja ni 1000
10. Kukoboa gunia moja la debe7 ni 4200
11.Gharama ya anayeingiza mpunga kwenye kinu ni 300 @ gunia
12. Na kama zimehifadhiwa mbali na kinu kilipo Kuna Gharama ya 500 @ gunia kusogeza.
Hii ni kwa ufupi tu wa biashara ya kukunua na kuchakata mpunga kuwa Mchele.
 
Duh
 
Hapa ndo nachanganyikiwa kabisaa juu ya biashara gani itanifaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…