Nyuki Mdogo
JF-Expert Member
- Oct 31, 2021
- 4,134
- 10,644
Milioni 12 njoo uwe broker wa madini. Utatoboa sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuongea ni rahisi, ingia kwenye game sasa.Kuna watu humu jamiiforum wamesinyaa ki mawazo na kwa hakika si rahisi Sana mtu kutoboa endapo akiamini mawazo ya hawa watu. Sjui Lakini
Mimi nilikua nafanya biadhara ya huduma za kifedha kwa mwezi nikawa napata 500k kwa mtaji wa milion 2
Nikawa nauza Simu kwa mtaji wa milion mbili nikawa napata faida ya 500k kwa mwezi.
Haya baba yangu anafanya kazi ya kuuza samaki anapeleka samaki mjini kutoka ziwani, samaki ananunua 700 anauza 1600
Kwa siku analaza mpaka 50 Kama faida.
Kuna jamaa yangu anauza Simu iPhone Simu Moja anapata faida si chini ya 30k na kwa siku anaweza kuuza zaid ya pic moja.
Mchoma chips mtaani kwetu analaza 50 kwa siku Kama faida.
Sjui hawa watu wanao beza 12 milon kuleta faida ya 2milon sjui Kama wapo serious na biashara.
Kuna kitu unapaswa kufaham mtoa mada nikua, biashara unapo ianza usitegemee wateja wa kutosha anza taratibu na kwa mtaji mdogo ila biashara ikianza kuchanganya mpka kufikia mtaji wa hizo milion 12 naiman unaweza pata faida hata zaid ya hizo milion 2
The BEST advice so far.Biashara isiyo umiza kichwa ni mazao wakati wa mavuno..kama umeajiliwa kipindi cha mavuno ongea na boss chukua likizo zama shambani kanunue mazao ya chakula,sogeza mjini weka dawa na kuhifandhi store...yatakulipa,biashara nyingi za kumuachia mtu unaweza kuja kulia tu,labda awe mkeo/mumeo na awe na uchungu sana na hiyo pesa.
Usimpe pesa mtoto wako wala baba yako, labda mama mzazi.
Over
Mchanganuo mzuri lakini ungejaribu kuainisha na changamoto nyingi zilizo mbele yake.Biashara mpya kwa mtaji huo mkubwa is too much risk kama hautasimamia mwenyewe mkuu
Ila kuna option ya kununua mazao ya chakula hasa Mpunga gunia zako za kutosha na kuziweka store na inapofika kipindi cha Masika unafanya kuzikoboa gunia zako na kupata mchele wako swafi tayari kwa kuingiza sokoni kwani kipindi hicho uhitaji wa mchele unakuwa mkubwa sana hapa Dar es Salaam na Zanzibar
Minimum profit calculation
Katika centre nyingi ninazo zifahamu kwa muda huu gunia moja la Mpunga lina range kwenye TSH. 50,000/=
Hivyo basi kwa Pesa uliyonayo yaani TSH. 12,000,000, utaweza kupata gunia zenye debe sita sita 240 za mpunga na kuzihifadhi.
Kipindi ambacho Masika imechanganya hasa mwezi wa kwanza au wa pili, wewe ndo unafanya kukoboa mpunga wako ili upate mchele na gunia 1 la mpunga la debe sita linatoa debe tatu za mchele na debe moja la chenga za mchele
Hivyo basi katika zile gunia 240 unazidisha mara 3 na utapata debe 720 za mchele clear na debe 240 za chenga za mchele
Ukija sokoni debe moja la mchele lina range kwenye 35,000/= kwahyo unazidisha mara debe zako 720 za mchele na utapata kiasi cha TSH. 25,200,000/=, pia debe moja la chenga za mchele ina range kwenye TSH 10,000/= ukizidisha na debe 240 utapata kiasi cha 2,400,000/=
Total itakuwa ni Tsh. 27,600,000/= na ukitoa mtaji wako wa 12,000,000/= utapata net profit ya TSH. 15,600,000/= katika kipindi cha miezi mitano cha kuhifadhi mpunga wako
Ila ukija kutoa gharama za kuhifadhi mpunga na kukoboa haizidi TSH. 5,000,000/=,hivyo bado net profit itabaki kama 10,000,000/= katika miezi mitano yako ya uvumilivu.
Centre zenye mpunga mzuri ni kama zifuatazo Kyela, Kamsamba na kilyatundu, Usangu, Kahama ila kwa Morogoro sizifahamu vizuri
Naomba kuwasilisha na ninakaribisha maswali
Hakuna mkataba wa bodaboda wa miaka miwili ni mwaka au miezi 11, bajaj ndio miaka miwili boss wangu.Kuna hiyo ya boda boda m12 utapata tv's zako 5 unawapa watu mkataba wa miaka 2 kwa siku una elfu5 mwezi una m1.5 kwa mwaka una m18 kwaiyo miaka 2 una m36 boda boda zinachangamoto nyingi sana hayo ni mahesabu tu ya kwenye karatasi ila ukiamua unaweza .....kama unashughuli zingine zinazokuingizia pesa iyo hela baada ya miaka 2 unaweza fanyia kitu cha maana tu au kupata mtaji mkubwa zaidi kwenye project nyingine umekosakosa m25 kabisa
Mkuu embu fafanua vizuri hapa...tupate madini.Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.
Chuo kwa 12m mkuu? Uko seriously kwelk? Chuo una maaana madrasa ama sunday school?Mkuu habari za majukumu. Nimeona thread ukiuliza ufanye biashara ipi kwa milioni 12. Mimi ningependa kukushauri ufungue chuo. Biashara ya chuo inalipa sana, hivi sass wanafunzi wanaohitimu shule za kata ni wengi Sana, na asilimia kubwa hawapati Nafasi ktk vyuo vya serikali na pia wazazi wengi hawapendi watoto wao waishie kidato cha NNE. Hivyo hii ni fursa kubwa Sana. Binafsi ninafanya kazi Kama afisa masoko katika chuo kimojawapo jijini arusha pia Nina uzoefu katika haya masuala. Kwa hiyo pesa uliyonayo inatosha kabisa kuanzisha chuo bila tatizo lolote. Endapo utapenda kufanya biashara hii tunaweza wasiliana 0717051576
Unapatikana wapi mzeya?Fanya biashara ya kukodisha used scaffolding, uza used planks, plywood, mbao.
Kwasababu ujenzi umeshamiri TZ huu ni wakati muafaka kwa biashara hii
Nitumie ujumbe 00971527369138
Kwa maelezo zaidi
Mkuu, naendelea kutathmini hizi shauri mbali mbali nilizopewa na wadau coz nimetahadhalishwa kutoingia kwa pupa kwenye hizi biashara. Hata hivyo namshukuru Mungu kamtaji kanaendelea kukua, kwa sasa nina 15milion. Nitatoa mrejesho punde nikichagua project ya kuanza nayo.Mkuu Brother James tupe mrejesho
Sawa mkuuMkuu, naendelea kutathmini hizi shauri mbali mbali nilizopewa na wadau coz nimetahadhalishwa kutoingia kwa pupa kwenye hizi biashara. Hata hivyo namshukuru Mungu kamtaji kanaendelea kukua, kwa sasa nina 15milion. Nitatoa mrejesho punde nikichagua project ya kuanza nayo.
Watu tunashindwa kujiuliza wale wenye vimeza vya kuuza mfano matunda wana mtaji wa shilingi ngapi. Yawezekana mtaji wao hauzidi 200,000/=. Lakini je, kwa siku hawaingizi japo 10,000/= kama faida na kwa mwezi 300,000/= hivyo kuendelea kuendesha maisha yao? 12m kama mtu ukiwa serious kwenye uchambuzi wa biashara ya kufanya na kuweka usimamizi imara ni pesa nyingi ambayo inaweza kukuingizia hiyo faida lengwa ya 2m kwa mwezi.Kama mil 12 haiwezi kuleta milioni 2 kwa mwezi ina maaana
Milioni 6 haziwezi kuzalisha milioni 1 kwa mwezi, ina maaana
Milioni 3 haziwezi kuzalisha laki 5 kwa mwezi, ina maana
Milioni1 na nusu haiwezi kuzalisha laki 2 na nusu ina maana
Laki 7 na nusu haiwezi kuzalisha laki 1 na 25elf kwa mwezi!!
Mbonavmimi hainiingii akilini?
Kwa mawazo ya wadau basi biashara hapa Tanzanua hazilipi.
Kwa hio laki 7 na ushee izalishe hamsini kwa mwezi?
Hebu fafanueni vipi mili 12 isizalishe milioni 2 kwa mwezi.
Na biashara za kumpa hizo hela ni ndogo ndogo tu ambazo anapaswa kufanya kama biashara tatu mpaka nne, za mitaji ya kawaida kabisa bila kutumia hiyo 12M yoteWatu tunashindwa kujiuliza wale wenye vimeza vya kuuza mfano matunda wana mtaji wa shilingi ngapi. Yawezekana mtaji wao hauzidi 200,000/=. Lakini je, kwa siku hawaingizi japo 10,000/= kama faida na kwa mwezi 300,000/= hivyo kuendelea kuendesha maisha yao? 12m kama mtu ukiwa serious kwenye uchambuzi wa biashara ya kufanya na kuweka usimamizi imara ni pesa nyingi ambayo inaweza kukuingizia hiyo faida lengwa ya 2m kwa mwezi.
Pia mwulize ni aina gani hiyo ya kuku ambapo ukiwa nao kuku 1,000 kila siku utaokota mayai idadi sawa na kuku waliopo na pia kuku kutaga mayai mawili kwa siku eti kisa tu kala kashiba. Mwisho kuku wa mayai atage kila siku na kwa miaka mitatu mfululizo?! Ni mahesabu yasiyo na uhalisia.Hizo cages za kuku 1000 Kwa milioni 2 zinapatkana wapi na Mimi nazitaka. Maana nnavyojua cages za layers za kuku 96 ni 650,000. Kwahiyo Kwa kuku 1000 awe na cages 11 ambayo ni kama milioni Saba huko.
Kilombero Kuna fursa gani Zaid ya mashamba ya miwa?Njoo kilombero,, Morogoro ufanye utafiti mdogo alafu uangalie biashara gani inakufaa maana uko kuna fursa nyingi Sana,,
But najua adi unapat m12 ushapanga la kufanya all in all njoo kilombero kuna fursa
Kilombero Kuna fursa gani Zaid ya mashamba ya miwa?