Mkuu acha nikwambie kitu kimoja uwasaidie na wengine watakaokuja kukuomba ushauri siku 1 huko mbeleni.
Fahamu biashara ni mchezo wa bahati na sibu,huku hamnaga constant profit hata siku 1 kwahiyo usidanganywe wala usipumbazwe na watu watakao kwambia biashara flani ina uhakika wa kiasi flani per day..per month,nk.
Hata kama biashara inaweza kukupa faida ya 2m per month fahamu sio miezi yote utalamba 2m,kwa biashara hyo hyo utapata siku hyo 2m yako, kuna mwezi utapat 3m,kuna miezi itafululiza hata mi 3 Utapata 50k per month, usishangae Huo ndio ukweli.
kwa hiyo kama ushajua ipo miezi utakayosugua benchi na biashara ni ile ile,mtaji ni ule ule, Anzia kuwaza kuanzia hapo sasa... unapowaza biashara ya kufanya usiishie kwenye mafaida ya kila mwezi,mafaida ya kila siku yatakufanya UPOTEZE uje ulie ukose wakukupa pole
ukishajua kuna miezi itaongozana hupati 2m na mtaji umewekeza 12m ninachokushauri ni uachane na biashara 1 kubwaaa na ufungue biashara nyingi ndogo ndogo.
Natamani tu ufahamu 2m ni sawa na uhakika wa faida 70k per day,sasa kama n hvyo kuna biashara nyingi sana za kukupa 50k to 70k za mitaji isiyozidi 2m.
Kwa hiyo ukiwa na 12m unaweza fungua biashara zaidi ya 4 zitakazokupa only 30k, just 30k x 4 = 120k per day ukizdsha 120k x 30 = 3,600,000
Nimekwambia biashara haina constant profit so ktk hiyo 3.6 kwa sababu hiyo ni total ya biashara 4 wewe utakua na uhakika wa kutoyumba hata kama biashara 1 haitokupa 30k zingine zitakupa,biashara hii ikigoma ile kule inakupa.. miezi ya shetani ikifika wenzako wakiwa wanalalamika biashara mbaya.
wewe kwako itakua ni tofauti,biashara yako itakua mbaya kwa namna ya faida kupungua ila si kukosa faida kwahyo kama ulikua ukipata 3.6m sasa hv utakua unapata 2m (ile target yakooooo) or utacheza 2.5,2,2,nk nk,nk
kwanini utakua na uhakika?!
Kwasababu hujawekeza kwenye biashara 1,umewekeza kwenye biashara nyingi ndogo ndogo ambapo uhakika wa faida ni mkubwa kuliko hasara, LAKINI ukitia 12m YOTE kwenye biashara yyte utakayoshauriwa au utakayoiafiki ina pesa,fahamu kwamba zipo siku zitakuja utakua na majuto makubwa kuliko mwanaume aliegundua anagongewa mke wake.
My POINT...
Split that capital into pieces... fungua biashara tofauti bado hauna kitu mkuu,12m is nothing anytime inapeperuka hiyo inabaki story ulishkaga 12m, usiwaze mavitu makubwa makubwa bado wewe n mjasiriamali mduchu sana sana sana,jishushe anzia huku down Halafu utaona namna utavyotusua.
ukiwa na malengo nina uhakika ndani ya mwaka 1 ukiweza fanya kama ninavyotamani ufanye kwa mtaji HUO ukifunga mwaka wa miezi 12,wasipokuita freemason watasema ulienda kuloga.
ila ukienda kama ninavyohisi unataka kwenda,mimi sikuombei mabaya ila nataka ufahamu utakua na safari ndefu sana kufikia ndoto zako.. Fupisha hiyo safari pita shortcut ili uzifikie ndoto zako angali kijana na una nguvu,angali ulimi wako una feel taste ya fanta orange...