Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

mkuu Namna ya kuagiza huo mzigo wa nguo china
unafuata mnyewe?
Mtaji wa chini kabisa ni Tsh ngapi?
 
Fungua biashara ya m_pesa,tigo pesa, Airtel money, fanya na uwakala wa nmb, Crdb, utafanikiwa Sana ,,,usiajiri mtu Anza kusimamia mwenyewe kuwa makini na matapeli utafanikiwa Sana.
Kwa makadirio ni nini au ni kiasi gani cha mtaji kinahitajika kwa hii biashara? Ukiweka kando gharama za fremu/ofisi/chumba cha kukodi!
 
Karibu kwenye samaki ,unapata zaidi ya m2 hiyo unapata kwa week moja tu
 
Njoo Dodoma fungua min super market, location za hiyo biashara zipo nyingi sana am sure population Dodoma imekuwa kwa kipindi hiki uhitaji wa biashara ya namna hiyo nikubwa sana.
 
Ila tatizo la Kariakoo NI KUPATA HIYO FREMU! Hapo ndiyo ngoma, kwani kwanza ni bei ghali sana na pili hazipatikani kwa urahisi hasa baada ya ule msala wa MOTO! Mambo ndiyo yamezidi kuwa balaa. Sijui kwa wenye uzoefu watujuze!
 
sawa, mshauri project ambayo kila mwezi atapata 2m kwa mtaji wa 12m...karibu
Zipo nyingi ikiwa ni pamoja na kuuza nguo, nguo za aina zote hapo K'koo! Ni suala la kupata the right place na the right contacts za kuupata huo mzigo. Hata ukiuza simu used or refurbished kutoka DUBAI ni pesa tu, ili mradi uwe mahali sahihi au hata hizo spares za magari, ni faida tu ili mradi uwe mahali sahihi at the right time.
 
Chukua tu million 8 chukua simu ndogo ndogo kwa ambazo sio smart phone,chukua na flash na memory then uwe unasambaza kwenye maduka ya kawaida utanishukuru sana.
Hizo simu achukue wapi, Kariakoo au Dubai au Uchina? Na mchanganua wa uwekezaji huu unakuwa vipi, yaani unaingia tu kila duka na kusaka wanunuzi au unakuwa na oda maalum? Mwaga madini.
 
Biashara hizo ndogo ndogo NI ZIPI? Hebu jaribu kuzitaja ili na wengine tupate MAUJUZI.
 
hizi biashara kwa mwezi unapata 2m sio? Jaribu tena kufanya research mkuu, 2m sio pesa ndogo au unazungumzia mauzo tu
 
Mimi nina bakery iko mbezi beach ninahitaji partner...kama uko intrested nicheck 0714882311...whatsapp only
Partner wa kufanya nini? Kuuza au kuoka mikate au cake au kukarabati hizo mashine au nini na unahitaji awe na mtaji gani - pesa, mashine au ujuzi/utaalamu? Hebu funguka
 
Dah I wish ningezipata hizo hela , fanya hivi ajiri mtu au ingia mbeya vijijini hasa mbalizi katika maeneo haya _isuto , ilembo , ilindi na iduwili ni wakulima wa kahawa, nunua kahawa kwa ndoo ya lita ishirini kwa elfu 5000_7000 then nunua mashine ya kuzibangua na pia zikaushe baada ya kuzibangua, uza kwenye viwanda maana wanakuja wenyewe kuchukua ulipo.

Nb. Kukauka ni ndani ya siku mbili mpaka tatu kwa kuwa unakuwa ni msimu wa kiangazi.

Kiwandani ndoo hiyo ya lita 20 inarange kwenye 40000_50000 .

Mahitaji unayotakikana kuwa nayo.

_Eneo la kuanikia na kutunzia kwa mda kabla ya kuuza
_mashine ya kubangua _350000tsh_400000tsh
_maturabai atleast matano( 5)
_ mwenyeji wa kukupitisha kukusanya, pamoja na usafiri wa pikipiki au gar.

Ahsante .
Ushauri tu.

TEKERI.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…