Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Kuongea ni rahisi, ingia kwenye game sasa.
 
The BEST advice so far.
 
Mchanganuo mzuri lakini ungejaribu kuainisha na changamoto nyingi zilizo mbele yake.
Maana ukiangalia juu juu inavutia ila mpaka kufikia kuipata hiyo faida ya 10M, shughuli pevu, na huenda asiipate.
Moja ya changamoto kubwa ni kuuziwa pumba badala ya mpunga, matokeo yake hizo gunia 240, akaambulia 200 au pungufu ya hapo.
 
Hardware biashara nzuri toka nje ya mji... kunako anza makazi fungua duka la vifaa vya umeme na ujenzi.
 
Hakuna mkataba wa bodaboda wa miaka miwili ni mwaka au miezi 11, bajaj ndio miaka miwili boss wangu.
 
Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.
Mkuu embu fafanua vizuri hapa...tupate madini.
 
Chuo kwa 12m mkuu? Uko seriously kwelk? Chuo una maaana madrasa ama sunday school?
 
Fanya biashara ya kukodisha used scaffolding, uza used planks, plywood, mbao.
Kwasababu ujenzi umeshamiri TZ huu ni wakati muafaka kwa biashara hii
Nitumie ujumbe 00971527369138
Kwa maelezo zaidi
 
Tengeneza na. Uza Used computers zinapatika kwa bei rahisi

Wasiliana nami.
00971527369138
 
Fanya biashara ya kukodisha used scaffolding, uza used planks, plywood, mbao.
Kwasababu ujenzi umeshamiri TZ huu ni wakati muafaka kwa biashara hii
Nitumie ujumbe 00971527369138
Kwa maelezo zaidi
Unapatikana wapi mzeya?
 
Mkuu Brother James tupe mrejesho
Mkuu, naendelea kutathmini hizi shauri mbali mbali nilizopewa na wadau coz nimetahadhalishwa kutoingia kwa pupa kwenye hizi biashara. Hata hivyo namshukuru Mungu kamtaji kanaendelea kukua, kwa sasa nina 15milion. Nitatoa mrejesho punde nikichagua project ya kuanza nayo.
 
Sawa mkuu
 
Watu tunashindwa kujiuliza wale wenye vimeza vya kuuza mfano matunda wana mtaji wa shilingi ngapi. Yawezekana mtaji wao hauzidi 200,000/=. Lakini je, kwa siku hawaingizi japo 10,000/= kama faida na kwa mwezi 300,000/= hivyo kuendelea kuendesha maisha yao? 12m kama mtu ukiwa serious kwenye uchambuzi wa biashara ya kufanya na kuweka usimamizi imara ni pesa nyingi ambayo inaweza kukuingizia hiyo faida lengwa ya 2m kwa mwezi.
 
Na biashara za kumpa hizo hela ni ndogo ndogo tu ambazo anapaswa kufanya kama biashara tatu mpaka nne, za mitaji ya kawaida kabisa bila kutumia hiyo 12M yote

Shida watu wengi ni wa maofisni hawajui biashara, Kwa sababu biashara ni tabia ya mtu ya kila siku na si kuuliza afanye nini
 
Hizo cages za kuku 1000 Kwa milioni 2 zinapatkana wapi na Mimi nazitaka. Maana nnavyojua cages za layers za kuku 96 ni 650,000. Kwahiyo Kwa kuku 1000 awe na cages 11 ambayo ni kama milioni Saba huko.
Pia mwulize ni aina gani hiyo ya kuku ambapo ukiwa nao kuku 1,000 kila siku utaokota mayai idadi sawa na kuku waliopo na pia kuku kutaga mayai mawili kwa siku eti kisa tu kala kashiba. Mwisho kuku wa mayai atage kila siku na kwa miaka mitatu mfululizo?! Ni mahesabu yasiyo na uhalisia.
 
Njoo kilombero,, Morogoro ufanye utafiti mdogo alafu uangalie biashara gani inakufaa maana uko kuna fursa nyingi Sana,,

But najua adi unapat m12 ushapanga la kufanya all in all njoo kilombero kuna fursa
Kilombero Kuna fursa gani Zaid ya mashamba ya miwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…