Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Mkuu acha nikwambie kitu kimoja uwasaidie na wengine watakaokuja kukuomba ushauri siku 1 huko mbeleni.

Fahamu biashara ni mchezo wa bahati na sibu,huku hamnaga constant profit hata siku 1 kwahiyo usidanganywe wala usipumbazwe na watu watakao kwambia biashara flani ina uhakika wa kiasi flani per day..per month,nk.

Hata kama biashara inaweza kukupa faida ya 2m per month fahamu sio miezi yote utalamba 2m,kwa biashara hyo hyo utapata siku hyo 2m yako, kuna mwezi utapat 3m,kuna miezi itafululiza hata mi 3 Utapata 50k per month, usishangae Huo ndio ukweli.

kwa hiyo kama ushajua ipo miezi utakayosugua benchi na biashara ni ile ile,mtaji ni ule ule, Anzia kuwaza kuanzia hapo sasa... unapowaza biashara ya kufanya usiishie kwenye mafaida ya kila mwezi,mafaida ya kila siku yatakufanya UPOTEZE uje ulie ukose wakukupa pole

ukishajua kuna miezi itaongozana hupati 2m na mtaji umewekeza 12m ninachokushauri ni uachane na biashara 1 kubwaaa na ufungue biashara nyingi ndogo ndogo.

Natamani tu ufahamu 2m ni sawa na uhakika wa faida 70k per day,sasa kama n hvyo kuna biashara nyingi sana za kukupa 50k to 70k za mitaji isiyozidi 2m.

Kwa hiyo ukiwa na 12m unaweza fungua biashara zaidi ya 4 zitakazokupa only 30k, just 30k x 4 = 120k per day ukizdsha 120k x 30 = 3,600,000

Nimekwambia biashara haina constant profit so ktk hiyo 3.6 kwa sababu hiyo ni total ya biashara 4 wewe utakua na uhakika wa kutoyumba hata kama biashara 1 haitokupa 30k zingine zitakupa,biashara hii ikigoma ile kule inakupa.. miezi ya shetani ikifika wenzako wakiwa wanalalamika biashara mbaya.

wewe kwako itakua ni tofauti,biashara yako itakua mbaya kwa namna ya faida kupungua ila si kukosa faida kwahyo kama ulikua ukipata 3.6m sasa hv utakua unapata 2m (ile target yakooooo) or utacheza 2.5,2,2,nk nk,nk

kwanini utakua na uhakika?!

Kwasababu hujawekeza kwenye biashara 1,umewekeza kwenye biashara nyingi ndogo ndogo ambapo uhakika wa faida ni mkubwa kuliko hasara, LAKINI ukitia 12m YOTE kwenye biashara yyte utakayoshauriwa au utakayoiafiki ina pesa,fahamu kwamba zipo siku zitakuja utakua na majuto makubwa kuliko mwanaume aliegundua anagongewa mke wake.

My POINT...

Split that capital into pieces... fungua biashara tofauti bado hauna kitu mkuu,12m is nothing anytime inapeperuka hiyo inabaki story ulishkaga 12m, usiwaze mavitu makubwa makubwa bado wewe n mjasiriamali mduchu sana sana sana,jishushe anzia huku down Halafu utaona namna utavyotusua.

ukiwa na malengo nina uhakika ndani ya mwaka 1 ukiweza fanya kama ninavyotamani ufanye kwa mtaji HUO ukifunga mwaka wa miezi 12,wasipokuita freemason watasema ulienda kuloga.

ila ukienda kama ninavyohisi unataka kwenda,mimi sikuombei mabaya ila nataka ufahamu utakua na safari ndefu sana kufikia ndoto zako.. Fupisha hiyo safari pita shortcut ili uzifikie ndoto zako angali kijana na una nguvu,angali ulimi wako una feel taste ya fanta orange...

Salute
 
Mil 12 tu unatengeneza uhakika wa 2M per month?
Huo mchongo ukitiki nitag mzee baba,maana kuna kiamount kipo tu nachakata nikitupe wapi kichwa kinakosa jawabu.
 
Ninatamani kukushauri wazo fulani,ila ni wacha nisome mawazo ya wakuu kwanza
 
Mkuu kabla ya kupata hizo besa, wewe ulikuwa umepanga kufanya nini?

Halafu hizo hela bado zipo? dah toka Septemba 3!!! 😆😆 maana maisha yenyewe ndio haya haya.
 
Mkuu kabla ya kupata hizo besa, wewe ulikuwa umepanga kufanya nini?

Halafu hizo hela bado zipo? dah toka Septemba 3!!! [emoji38][emoji38] maana maisha yenyewe ndio haya haya.
Ni akiba tu ambayo na jiwekea ili nifanye biashara yenye tija (productive business) pesa ipo boss wangu na kwa sasa zimeongezeka, zimefika 13mil. Wewe nisaidie tu kunishauri cha kufanya mkuu
 
Mkuu habari za majukumu. Nimeona thread ukiuliza ufanye biashara ipi kwa milioni 12. Mimi ningependa kukushauri ufungue chuo. Biashara ya chuo inalipa sana, hivi sass wanafunzi wanaohitimu shule za kata ni wengi Sana, na asilimia kubwa hawapati Nafasi ktk vyuo vya serikali na pia wazazi wengi hawapendi watoto wao waishie kidato cha NNE. Hivyo hii ni fursa kubwa Sana. Binafsi ninafanya kazi Kama afisa masoko katika chuo kimojawapo jijini arusha pia Nina uzoefu katika haya masuala. Kwa hiyo pesa uliyonayo inatosha kabisa kuanzisha chuo bila tatizo lolote. Endapo utapenda kufanya biashara hii tunaweza wasiliana 0717051576
Mkuu me naomba kuuliza hivi ni gharama ngapi inahitajika kupata eneo ndani ya chuo kufanya biashara

NB: eneo la kujenga kama frem[emoji120]
 
Mkuu, lengo ni 2mil. au zaidi kwa mwezi. Chukulia hii kama sehemu ya kigezo cha biashara utakayonishauri
Mkuu njoo tufanye forex kwa mtaji wako wa $5000 ambayo ni sawa na M13 hatuwezi kukosa faida ya $2500 per each months ambazo ni sawa na M5,mm Nina skills wewe una mtaji njoo tushirikiane maana mm nafanya forex lakn kwa mtaji kdg sana lakn napata faida nzuri tu ..itakuwaje kama nikianza kutrade na $5000 account...karibu sana!
 
Biashara mpya kwa mtaji huo mkubwa is too much risk kama hautasimamia mwenyewe mkuu

Ila kuna option ya kununua mazao ya chakula hasa Mpunga gunia zako za kutosha na kuziweka store na inapofika kipindi cha Masika unafanya kuzikoboa gunia zako na kupata mchele wako swafi tayari kwa kuingiza sokoni kwani kipindi hicho uhitaji wa mchele unakuwa mkubwa sana hapa Dar es Salaam na Zanzibar

Minimum profit calculation

Katika centre nyingi ninazo zifahamu kwa muda huu gunia moja la Mpunga lina range kwenye TSH. 50,000/=
Hivyo basi kwa Pesa uliyonayo yaani TSH. 12,000,000, utaweza kupata gunia zenye debe sita sita 240 za mpunga na kuzihifadhi.

Kipindi ambacho Masika imechanganya hasa mwezi wa kwanza au wa pili, wewe ndo unafanya kukoboa mpunga wako ili upate mchele na gunia 1 la mpunga la debe sita linatoa debe tatu za mchele na debe moja la chenga za mchele

Hivyo basi katika zile gunia 240 unazidisha mara 3 na utapata debe 720 za mchele clear na debe 240 za chenga za mchele

Ukija sokoni debe moja la mchele lina range kwenye 35,000/= kwahyo unazidisha mara debe zako 720 za mchele na utapata kiasi cha TSH. 25,200,000/=, pia debe moja la chenga za mchele ina range kwenye TSH 10,000/= ukizidisha na debe 240 utapata kiasi cha 2,400,000/=

Total itakuwa ni Tsh. 27,600,000/= na ukitoa mtaji wako wa 12,000,000/= utapata net profit ya TSH. 15,600,000/= katika kipindi cha miezi mitano cha kuhifadhi mpunga wako

Ila ukija kutoa gharama za kuhifadhi mpunga na kukoboa haizidi TSH. 5,000,000/=,hivyo bado net profit itabaki kama 10,000,000/= katika miezi mitano yako ya uvumilivu.

Centre zenye mpunga mzuri ni kama zifuatazo Kyela, Kamsamba na kilyatundu, Usangu, Kahama ila kwa Morogoro sizifahamu vizuri

Naomba kuwasilisha na ninakaribisha maswali
Hii biashara ni tamu sana kwa mm mtu niliye karibu na Kenya yani utashika pesa mpaka unuke helaa
 
Salaam Alleykhum,

Wadau kwa kutumia uzoefu wenu, nishaurini nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa million 12 nilionao ili kila mwisho wa mwezi at least nipate Net profit ya milioni mbili.

Nipo tayari kufanya biashara ktk mkoa wowote Tanzania au hata kama ni importation business kama mtaji unatosha nipo tayari.

Nipeni ushauri ili nami nitoboe.
Fungua duka la dawa kijijini
 
Itabidi nikutafute unipe shule kwanza coz forex business kibongo bongo inaonekana ni biashara ya bahati nasibu, yaani badala ya kukosa faida inasemekana forex unaweza kupoteza mpaka mtaji wote. Wengi tumezoea biashara yenye mtaji fixed then unaingiza faida au unakosa faida ila mtaji always unakuwa salama.
hahaha ngoja upigwe kwanza akili ikae sawa.
 
Back
Top Bottom