Kinengunengu
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 1,716
- 4,375
Hakuna kitu kama hiko kuwa ukizaliea tu umeandikwa kwenye kitabu cha kuzimu. Huyo Ibilisi hajaumba kiumbe chochote na hawezi kuwa mahali pote kwa wakati mmoja ili ajue nani kazamiwa kwa wakati gani.Inatafakarisha sana, Kwa hiyo mtu akizaliwa tu automatically unakua umeandikwa kwenye kitabu cha kuzimu?????,🤔
Haya shetani alikua malaika mkuu wa sifa huko mbinguni, Hivi hiyo roho ya uasi ya kujiinua kutaka kumzidi Mungu ilitoka wapi???? hapo kabla hiaikuepo??
Kinachotokea, Yeye aliyekuumba anakujua na ameandika jina lako kwenye kitabu cha uzima wa Milele cha mwana kondoo. Biblia inaeleza wazi mbinguni kuna vitabu viwili. Kitabu cha Uzima na kitabu cha hukumu. Kitabu cha Uzima huandikwa kila mwanadamu azaliwapo ila atendapo dhambi na kumuasi Mungu hufutwa kwenye kitabu cha Uzima na kuandikwa kwenye kitabu cha hukumu.
Kwa kuwa mwanadamu amepewa neema ya upatanisho kama ambavyo Kristo alikuja katika mwili na kutupatanisha naye kwa mwili wake. Ndivyo wanadamu tumepewa huduma ya upatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Pale tumuombeapo mtu sala ya toba ndio tunampatanisha na Mungu wake na tunamuomba Mungu afute jina lake kwenye kitabu cha hukumu na aliandika kwenye kitabu cha Uzima wa Milele. Vitabu hivi vitatumika kwenye siku ile ya kukutania njia panda. Wale watendao uovu watafufuliwa kwanza kwa ajili ya hukumu na wema kwa ajili ya Uzima wa Milele.
Ndugu yangu mpendwa, Baba, kaka,Mama, Dada na mwana JF mwenzangu. Wapi pa kuishi katika umilele wako huandaliwa sasa ukiwa hai. Ni vyema.sasa uchague wapi utakapoishi katika umilele wako. Kumbuka kuwa, kesho yako ji fumbo ila umilele wako umekaribia.