Nigeria, Ripoti: Mtoto mmoja kati ya watoto wanne siyo wa baba anayedhaniwa

Nigeria, Ripoti: Mtoto mmoja kati ya watoto wanne siyo wa baba anayedhaniwa

wakunyonya

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2024
Posts
994
Reaction score
2,433
!!Wanaume kuna ujumbe wenu hapa...

Ripoti mpya ya Taasisi ya Vinasaba ya Smart DNA iliyo na makao yake nchini Nigeria imefichua kuwa kati ya watoto wanne, mmoja anakuwa sio mtoto halali wa baba anayedhaniwa na hivyo kuchochea kile ambacho wengi sasa wanakielezea kama mgogoro wa uzazi.

Ripoti ya Mwaka 2025 ya Uchunguzi wa DNA inaonyesha kuwa asilimia 25 ya vipimo vilivyofanywa kati ya Julai 2024 na Juni 2025 vilithibitishwa kuwa baba waliodhaniwa hawana uhusiano wa kibayolojia na watoto hao. Maombi mengi ya vipimo vya DNA yaliwasilishwa na wanaume ambao karibu nusu yao walikuwa na umri wa miaka 41 na zaidi.

Jambo la kustaajabisha zaidi ni kwamba, asilimia 64 ya vifungua mimba—hasa wavulana—waligunduliwa kutokuwa na uhusiano wa kibiolojia na waliodhaniwa kuwa baba zao, kiwango kikubwa zaidi kuliko cha watoto waliozaliwa baadaye.
 
Kikubwa mimi ndio naitwa baba na anaitwa kwa jina langu,mengine watajua wenyewe.Mambo mengine mnajitakia presha zisizo na msingi🤣🤣
 
Kikubwa mimi ndio naitwa baba na anaitwa kwa jina langu,mengine watajua wenyewe.Mambo mengine mnajitakia presha zisizo na msingi🤣🤣
Wengine Huwa wanakuja kuambiwa ukweli wakikua hasa mkija kuwa na uhasama na mama mtu mfano diamond
 
Haya bwana ambae unaakili endelea na akili zako.Pengine hata wewe mzee wako alibambikwa(wewe sio mtoto wake pengine) je angekuacha? Na je huyo mzee wako ni zoba? 🤣🤣
Hakuna shaka mzee wangu ndiye baba yangu kinasaba na wanangu ni wangu kinasaba. Haibiwi mtu hapa.
 
Hakuna shaka mzee wangu ndiye baba yangu kinasaba na wanangu ni wangu kinasaba. Haibiwi mtu hapa.
Tupambane kutafuta hela.Haya mambo mengine tuachane nayo kwani hatuwezi kupambana nayo bali yataongeza chuki na kusababisha matukio mabaya ambayo tutakujajutia .(You can never beat nature.)
 
Tupambane kutafuta hela.Haya mambo mengine hatuwezi kupambana nayo bali yataongeza chuki na kusababusha matukio mabaya.(You can never beat nature.)
Utafute hela kwa tabu katika mazingira hatarishi, halafu eti, itumike kulelea mtoto wa dume lingine. Kama ume adopt mtoto sawa, lakini siyo kufanywa bwege.
 
Back
Top Bottom