TANZIA Nigeria: Sis Osinachi Nwachukwu aliyeshirikishwa wimbo wa ‘Ekwueme’ afariki dunia

Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sis Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo wake “Ekwueme” amefariki dunia.

Osinachi alishirikishwa na Prospa Ochimana katika wimbo huo, amefikwa na mauti jioni ya Aprili 8, 2022, hii baada ya kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takriban miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo.

Baadhi yake nyimbo ni pamoja na “Nara Ekele” akiwa na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis,Abuja), “Ekwueme” akiwa na Prospa Ochimana na nyinginezo.
Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.

Source: Dailypost

Mungu amlaze mahali anapostahili
 
Tunwomba waziri anayekusika na mambo ya sanaa na burudani aiwakilishe nchi yetu 🇹🇿 Kwenye mazishi. Wimbo wake umeliwaza kuburudisha na kuleta hisia za ki Mungu miongoni mwa watanzania
 
Inavyosemekana sio kansa iliyomuua bali kipigo kutoka kwa mumewe alimpiga kifuani akawa kwenye life support mpaka umauti unamkuta. Katika ndoa yake amepitia vipigo na unyanyasaji toka kwa mumewe. Account za baadhi ya wanaijeria wamefunguka mengi ambayo tulikuwa hatujui
 
Duuuh ...account zipi hizo za wapopo nikasome mkuu
 
This
IMG-20220410-WA0003.jpg
 
Inavyosemekana sio kansa iliyomuua bali kipigo kutoka kwa mumewe alimpiga kifuani akawa kwenye life support mpaka umauti unamkuta. Katika ndoa yake amepitia vipigo na unyanyasaji toka kwa mumewe. Account za baadhi ya wanaijeria wamefunguka mengi ambayo tulikuwa hatujui
Aisee amepitia abuse za hatari sana, haya makanisa na msemo wa “watu watasema nini “yatawamaliza wanawake..
Mmewe amekamatwa, I hope justice will be served( ila ni africa, we can only hope)
 
Back
Top Bottom