Nihudhurie usaili upi kati ya hizi mbili?

Nihudhurie usaili upi kati ya hizi mbili?

Status
Not open for further replies.

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Wakuu kwema?

Tarehe 27 mwezi huu nimeitwa interview mbili kama ifuatavyo;
Saa 2 kamili asubuhi natakiwa kuwa Iringa University mkoani Iringa kufanya usaili wa kuandika ya nafasi ya Uhasibu, muajiri akiwa Iringa University mwenyewe. Nafasi zinazogombaniwa hapa ni 2 kati ya watahiniwa 24 tulioitwa.

Halafu siku hiyo hiyo tarehe 27 saa 1 kamili asubuhi, natakiwa kuwa jijini Dodoma katika Chuo Kikuu cha UDOM kufanya usaili wa nafasi ya Auditor ii, muajiri akiwa ni NAOT. Nafasi zinazogombaniwa hapa ni 37 kati ya watahiniwa 5000+ tulioitwa kwenye huu usaili.

So niko njia panda hapa, niende wapi wakuu? Nafasi zote mbili nazipenda kwa usawa.
 
Hao iringa university sikushauri hata kuwafikiria.wana njaa balaa,wanategemea ada za wanafunzi kulipa mishahara,imagine sasa hivi tunavyozungumza tangu mwezi wa 8 mpaka leo hawajalipwa mishahara yao.
Wana maisha magumu mno kwa kifupi.
Ingekua ni RUCO au SAUT ningekushauri uende ila iringa university sikushauri aisee.
 
Hili nalo neno ngoja nisimame hapa
 
Mkuu, kwenye soko la ajira tulilonalo kwa sasa Tanzania, jibu liko wazi, kupata ndio ujanja zaidi kisha inafuata umepata nini.

Kwa kuongezea, ajira sio mzazi, zinabadilishika.

Naamini umeelewa nimeshauri uchague kipi.
 
Ungeshauri tu pasipokuuliza swali lako la kejeli ningekuelewa.
Duh hii siyo kejeli mkuu, hebu soma vzr utaelew. Why tunapenda lugha laini laini tu ruhusu kielew even kwa ugumu aliokupa. Mie nmemwelewa haswaa
 
Duh hii siyo kejeli mkuu, hebu soma vzr utaelew. Why tunapenda lugha laini laini tu ruhusu kielew even kwa ugumu aliokupa. Mie nmemwelewa haswaa
Haya ,yaishe.
 
Nenda Iringa University naona number of vacancies na number of Candidates at least reasonable compared to Utumishi , Go try your luck
 
Angalia wapi karibu kwenda swala la nauli na malazi na probability ya kupata kutokana na namba ya candidates .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom