Niiteni Mara (uchungu)

Niiteni Mara (uchungu)

Mimi nilizaliwa miaka ya 90, ni mtoto wa 3 kwenye familia ya watoto 5.
Katika hatua za ukuaji, nilionyesha tabia za tofauti na wenzangu. Mama alisema nilikuwa sieleweki kama nna furaha au nimekasirika. Wala sikuonyesha kufurahia vitu kama toys au kucheza na watoto wengine.
Lakini nikaendelea kukua, nilivyokuwa na miaka 5 nikaanza nursery baadae nikaanza la kwanza. Shule pia walimu hawakunielewa – waliniona mkorofi, napenda kukasirika, wengine wakasema mjeuri na mengine mengi.
Niliadhibiwa, nikasemwa lakini sikuwaelewa na sikubadilika. Ila kwenye mitihani, nilifaulu sana. Maisha ya shule hayakuwa marahisi kwangu. Nilivyokuwa darasa la 4, nikaanza kuanguka, nikapelekwa hospital nikapimwa kisha nikapewa dawa za kifafa.
Nilivyoanza kuumwa nilikaa nyumbani muda mrefu, nilivyorudi shule walimu waliambiwa kwamba bado ile hali ya kuanguka haijaisha hivyo wakawa wameacha kunisemasema na kunipiga.
Ila walimu walivyoacha kunisema haikunisaidia sana, kwasababu nyumbani wazazi walitengana mwaka mmoja kabla sijaanza kuumwa. Basi mama akawa na uchungu , akawa anamalizia hasira zake kwangu. Ukiangusha hata kijiko hapo ndani anatoa maneno makaliii! Kwahiyo akawa ananibully, ananiambia wewe mjinga tu hutafika mbali!
Mungu alijalia nikamaliza la saba, nikaenda boarding school. (Nilienda na dawa zangu) .Nilishukuru kwenda sehemu mpya nikitumaini huko ntakaa kwa raha. Lakini nilivyofika mambo yakawa vilevile. Nikaambiwa mimi mjeuriii , najibu watu vibaya, lakini pia nikaanza kusikia watu wanaambiana huyu wa ajabu, nk. Zile changamoto za primary zikarudi.
Maisha yalikuwa magumu sana, kuna wakati nikiwa kama form 3 hivi nikawa nataka kujiua lakini nikashindwa.
Siku zikasogea nikamaliza form 4,nikaenda a level baadae chuo.
Nilivyomaliza chuo, nikawa nafanya kazi. Nikajakupata Depression kubwa nikawa sina hamu ya kuishi sina nguvu hata ya kuamka kitandani. Nikawa nikitoka kazini nikiona magari pale kwenye foleni natamani nijirushe. Nilivyoona ile hali haishi nikaacha kazi nikawa tu niko nyumbani. Basi mama alivyojua nimeacha kazi akaanza kunisemaa, kwamba nachagua kazi wakati sina lolote. Baba yeye alikuwa supportive.
Baada ya muda mrefu nikawa sawa, nikapata kazi nyingine kwenye NGO ya watu wa marekani . Nilivyokaa na wale wazungu ndio mmoja wao akahisi nna usonji, nilivyofanyiwa vipimo ikawa confirmed. Baadae ile kazi pia nilikuja kuacha
Nimeandika hivi kwasababu natamani watu waelewe madhara ya kumwambiaa mtu kuwa wewe ni wa ajabu/mjinga/zoba na mengine yanayofanana na hayo yana madhara makubwa. Unamsababishia mtu kutojiamini , stress na depression.
Lakini pia, wazazi ambao umejaliwa watoto zaidi ya mmoja, jifunze kuwa fair sio kukaa unapendelea wale unaoona wana potential kubwa.
Ruth 1:20
Unahitaji damu ya Yesu ikuponye, mtumainie Kristo naye hatokuacha atasimama nawe.🙏🏿
 
Jirani ninapoishi kuna mtoto binti miaka 6 ana vishiria vyote vya usonji.

Nilivyosoma uzi wako nimewaza huenda na yeye akapitia kama uliyopitia sababu ya uelewa mdogo wa jamii juu ya usonji.
 
Pole ndugu , kuna aina fulan ya maisha ya maisha yako jinsi ulivyo eleza haina tofauti na mimi.
Angalizo na ushauri wako hapo mwishoni lizingatiwe mno .
 
Niite Mara, kwa sababu Mwenywezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
Huo ni mtari wa biblia Ruth 1:20
Nimesoma hio sura ya kwanza ya Ruth , kwa jinsi huyo mama alivyo pitia kadhia ile sijui kwa nini mleta mada ameamua kutumia hii kama kichwa cha mada yake.

Ukitazama kwa jicho lingine unaweza kuona ndani ya mleta mada kuna hali isiyo rahisi.
Imenifikirisha sana.
 
Mimi nilizaliwa miaka ya 90, ni mtoto wa 3 kwenye familia ya watoto 5.
Katika hatua za ukuaji, nilionyesha tabia za tofauti na wenzangu. Mama alisema nilikuwa sieleweki kama nna furaha au nimekasirika. Wala sikuonyesha kufurahia vitu kama toys au kucheza na watoto wengine.
Lakini nikaendelea kukua, nilivyokuwa na miaka 5 nikaanza nursery baadae nikaanza la kwanza. Shule pia walimu hawakunielewa – waliniona mkorofi, napenda kukasirika, wengine wakasema mjeuri na mengine mengi.
Niliadhibiwa, nikasemwa lakini sikuwaelewa na sikubadilika. Ila kwenye mitihani, nilifaulu sana. Maisha ya shule hayakuwa marahisi kwangu. Nilivyokuwa darasa la 4, nikaanza kuanguka, nikapelekwa hospital nikapimwa kisha nikapewa dawa za kifafa.
Nilivyoanza kuumwa nilikaa nyumbani muda mrefu, nilivyorudi shule walimu waliambiwa kwamba bado ile hali ya kuanguka haijaisha hivyo wakawa wameacha kunisemasema na kunipiga.
Ila walimu walivyoacha kunisema haikunisaidia sana, kwasababu nyumbani wazazi walitengana mwaka mmoja kabla sijaanza kuumwa. Basi mama akawa na uchungu , akawa anamalizia hasira zake kwangu. Ukiangusha hata kijiko hapo ndani anatoa maneno makaliii! Kwahiyo akawa ananibully, ananiambia wewe mjinga tu hutafika mbali!
Mungu alijalia nikamaliza la saba, nikaenda boarding school. (Nilienda na dawa zangu) .Nilishukuru kwenda sehemu mpya nikitumaini huko ntakaa kwa raha. Lakini nilivyofika mambo yakawa vilevile. Nikaambiwa mimi mjeuriii , najibu watu vibaya, lakini pia nikaanza kusikia watu wanaambiana huyu wa ajabu, nk. Zile changamoto za primary zikarudi.
Maisha yalikuwa magumu sana, kuna wakati nikiwa kama form 3 hivi nikawa nataka kujiua lakini nikashindwa.
Siku zikasogea nikamaliza form 4,nikaenda a level baadae chuo.
Nilivyomaliza chuo, nikawa nafanya kazi. Nikajakupata Depression kubwa nikawa sina hamu ya kuishi sina nguvu hata ya kuamka kitandani. Nikawa nikitoka kazini nikiona magari pale kwenye foleni natamani nijirushe. Nilivyoona ile hali haishi nikaacha kazi nikawa tu niko nyumbani. Basi mama alivyojua nimeacha kazi akaanza kunisemaa, kwamba nachagua kazi wakati sina lolote. Baba yeye alikuwa supportive.
Baada ya muda mrefu nikawa sawa, nikapata kazi nyingine kwenye NGO ya watu wa marekani . Nilivyokaa na wale wazungu ndio mmoja wao akahisi nna usonji, nilivyofanyiwa vipimo ikawa confirmed. Baadae ile kazi pia nilikuja kuacha
Nimeandika hivi kwasababu natamani watu waelewe madhara ya kumwambiaa mtu kuwa wewe ni wa ajabu/mjinga/zoba na mengine yanayofanana na hayo yana madhara makubwa. Unamsababishia mtu kutojiamini , stress na depression.
Lakini pia, wazazi ambao umejaliwa watoto zaidi ya mmoja, jifunze kuwa fair sio kukaa unapendelea wale unaoona wana potential kubwa.
Ruth 1:20
Pole......
 
Back
Top Bottom