Nijiandae vipi kuingia Miaka 30?

Umri ni kama kupokea vikwazo vya kiuchumi.Hauwezi kuhisi sasa nina miaka kadhaa na ukasema umri wangu ule pale nauona unapita.Au uleee umeingia mwilini.Au ukaguna ..."duh"...nimekuwa mzito umri umeongezeka.
Jitahidi tu kuwa na juhudi ya kujitunza,kula vizuri kwa kiwango stahili,mazoezi,kufanya kazi halali kwa bidii na tija na kumchaji Mungu.
 
Shukrani sana Kaka Mkubwa,
Umenipa Muongozo makini sana.
 
Well hata mimi sijaacha kuangalia katuni.

Nashauri njoo ukae wiki mbili na mimi ujifunze kwa vitendo.
 
Weeeh!
Queen kasema nina Ngozi nzuri mimi napingaje sasa [emoji4]

Shukrani sana My Queen.
 
Niliingia kwangu nikiwa 35, ilikua ni ndogo lakini ilinisaidia kujiendeleza nikiwa na peace of mind. Ninategemea kuhamia nyumba kubwa zaidi miaka mitatu ijayo.
Safi sanaaa,
Kuna dili lilitiki nikapata Pesa ndefu, nikanunua Nyumba haraka kabla ya kuzitumbua wakati huo nilikua na miaka 26 lakini sasa nimeanza kujenga nyumba ya Ndoto yangu, taratibu bila presha hadi siku itakapoisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…