Shikamoni wakubwa..
Vijana wenzangu mambo vipi..
Wakuu Nina miaka 22 elimu yangu niliishia form 4. Baada ya kumaliza 2022 nimekaa mtaani sana nikaona si vyema nikakaa bila fani yoyote. Mwanzoni mwa mwaka niliamua nipambane nikafanya kazi mbalimbali kama saidia fundi na kufyeka n.k.
Nimefanikiwa kupata 1 million , Je nijifunze kipi kati ya hivyo nilivyoviorodhesha.
Ushauri wakuu
Nilikuwa kwenye hiyo fani/field since 2004 (nilikuwa na ni operator) ila kwa sasa nimebadili niko kwenye field ingine ya kutaftia ugali kwa sasa...
Nikushauri tu....ni hivi....Usije ukaenda kulipa chuo eti ufundishwe Excavator/Bull-Dozer/Wheel-Loader/Grader/Back-Hoe/Drill-Rig,ama Truck...ili wakupe cheti...
Nakutahadharisha utaenda field(kazini ama kwenye test ukiwa bado mweupe kabisa! Hujui chuma yoyote hapo kati ya hizo bali unamiliki vyeti tu!)
Tafuta mahala ambapo Maop/maTX (ama maopareta muitavyo) wanafanya kazi, iwe road(barabarani), ama tumigodi tudogo tudogo...ongea na op mmojawapo tu! Akufue chuma mojawapo kati ya hizo(nikushauri iwe excavator ama grader,
Ama Drill Rig(chuma ya kishua hii mshahara Tembo!) (Operator hot cake duniani kote ni DRILLER TU!)Kuruka na mwewe nje ya nchi kulipwa dorali kwa ma Driller ni kitu cha kawada kabisa!)
Ongea vizuri na opereta wa hiyo mashine,
Note! ( USIMWAMBIE KAMA UNA MILIONI 1 ITAKULA KWAKO)... Maoperator 90% ni walevi!
Mnunulie tungi, Vocha vocha muombe awe anakufua chuma, atakupa session ya masaa kadhaa kila siku, utaendelea kuimaster vizuri mashine ukiwa kazini....
Kadri utakavyozidi kuiva, ndipo op anakuamini kukuachia masaa mengi bosi wake akiwa hayupo ili op huyo apate muda akalewe!
Siku ukienda kwenye test mgodini ama road...UNAKUTA TAYARI UMESHAIVA MDOGO WANGU!
Ukimaliza hayo niliyokuambia, kata leseni, njoo humu niambie brother nimeiva sasa nitangenezee vyeti vya kuombea kazi mgodi wowote, nchini ama nje ya nchi, NITAKUTENGENEZEA FOR FREE!