Nijuzeni: Costantine Kimanda alikuwa ni mchezaji wa aina gani?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Nimekuwa nikisikia sifa za mchezaji wa zamani wa Yanga, Costantine Kimanda kwamba alikuwa ni mchezaji wa aina yake. Najua humu kuna wakongwe sio mbaya mkatujuza kuhusiana na mchezaji huyu wa kipare aliyetamba miaka ya 90 Jangwani.
 
Nimekuwa nikisikia sifa za mchezaji wa zamani wa Yanga, Costantine Kimanda kwamba alikuwa ni mchezaji wa aina yake. Najua humu kuna wakongwe sio mbaya mkatujuza kuhusiana na mchezaji huyu wa kipare aliyetamba miaka ya 90 Jangwani.
Huyu sio Mpare. Mpare aliyecheza Yanga kwa Mafanikio ni Sekilojo Chambua. Constantine Kimanda ni mchezaji aliyetoka Zaire (Congo DRC) alikuwa akichezea Yanga kabla ya kwenda uarabuni. Ni mmoja kati ya mabeki wazuri sana ila hawezi kumsahau Edward Chumila!
 
Mkuu Kimanda alicheza mechi moja tu ya watani na ilisemekana wachezaji wa Yanga walivuta muamala ambapo Yanga walifungwa 4-1. Katika mchezo huo alifunga goli na alishangaa wenzake kucheza kwa kutojituma hali iliyopelekea yeye pekee ndiyo aruhusiwe kukanyaga makao makuu ya klabu.Ni Madaraka Selemani aliyefunga magoli mawili na George Masatu, kusema hatamsahau marehemu Chumila sio kweli
 
Alicheza mechi mbili, mechi ya kwanza Yanga ilishinda goli 2-0 magoli yote yalifungwa na marehemu James Tungaraza aka Boli Zozo .
 
Alicheza mechi mbili, mechi ya kwanza Yanga ilishinda goli 2-0 magoli yote yalifungwa na marehemu James Tungaraza aka Boli Zozo .
Yes! Hii ilikuwa 1994. Kulikuwa na beki mwingine aliyekuwa anaitwa Ngandu Ramadhan. Hiyo mechi ya 4-1, goli la kwanza la Simba lilifungwa na George Magere Masatu kwa njia ya adhabu, Kimanda akasawazisha approximately distance ileile but at the end of the day, Simba4-1Yanga
 

Constantine Kimanda

Constatine Kimanda alikuwa ni beki wa kati au mkoba wa Yanga na timu ya taifa ya Burundi na sio Congo DRC.

Ilikuwa ni mwaka 1994 alipochezea Yanga ambapo alisajiliwa chini ya uongozi wa katibu mkuu wa wakati ule marehemu George Mpondela.

Alikuwa pamoja na marehemu Method Mogella ambae waliuzwa wote na Mpondela kwenye timu ya uarabuni ya Sharjah FC.

Yanga ya mwaka 1994 ilikuwa ni kali kwelikweli kina Steven Nemes Sekilojo Chambua, Mohamed Hussein au "Mmachinga", Nico Bambaga, Edibily Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo", na Salvatory Edward.

Wengine akina Said Mwamba Kizota, marehemu Salum Kabunda "Ninja", Issa Athuman, Keneth Mkapa, Selemani Mkati, Rifati Said, Sanifu Lazaro, David Mjanja na Mwanamtwa Kihwelu.

Wachezaji wengine walikuwa ni Allly Yusuf "Tigana", Willy Martin, Ngadu Ramadhan, Joseph Lazaro, Willy Mtendamema.

Mwaka 1994 ndipo kulitokea mgogoro mkubwa kwenye klabu hii na kukazaliwa Yanga Asili na Yanga kampuni.

Hivyo Yanga kampuni chini ya Marehemu Mpondela ikaenda kufungwa goli 4-1 na Simba na baaada ya hapo wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wakatimuliwa.

Kimanda ndiye aliefunga goli pekee la Yanga.

Baada ya mgogoro huo kipa Rifat Said alirudi Zanzibar, Edibily Lunyamila akaenda Malindi ya Zanzibar na Saidi Mwamba pamija na Steven Nemes wakahamia Simba.

Ndipo Kocha wa Yanga Tambwe Leya akaamua kusuka kikosi kipya cha Yanga kilichokuwa na wachezaji kama Anwar Awadh, Mzee Abdallah, Silvatus Ibrahim “Polisi”, Maalim Saleh “Romario”, Nonda Shaaban “Papii”, Bakari Malima na Kally Ongala.

Wengine akina Seki Chambua Salvatory Edward na wengine.

Vijana hawa waloitwa Black Stars ndiyo waloiwezesha Yanga kuja kucheza nane bora mwaka 1998 ya klabu bingwa Afrika na baadae mwaka 1999 wakanyakuwa ubingwa wa Afrika Mashariki.


Edibily Lunyamila na Mohamed Hussein.

Kimanda kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Ubelgiji.
 
Kwa Kally Ongala siyo kweli,Ongala kucheza Yanga ya 1999,kabla ya hapo akicheza Abajalo Mnyama mkali wa Sinza.
 
Vuta kumbukizi ya hii mechi

 
MAGOLI YA SIMBA YALIFUNGWA NA MASATU,MADARAKA,CHINA NA DUA BIN SAID.
 
aliyeunda yanga mpya 97-2000 alikuwa kocha mzaire RAUL SHUNGU
 
Nimekuwa nikisikia sifa za mchezaji wa zamani wa Yanga, Costantine Kimanda kwamba alikuwa ni mchezaji wa aina yake. Najua humu kuna wakongwe sio mbaya mkatujuza kuhusiana na mchezaji huyu wa kipare aliyetamba miaka ya 90 Jangwani.
Beki 5 ya Yanga,
Alikua mtu mmoja serious na smart sana,
Ujio wake Yanga ulileta Changamoto kwa Beki 5 ya Simba ya wakati huo, George Magere Masatu (GM).
Changamoto ilikua kwamba nani Beki 5 bora kwa wakati huo.
 
shikamoo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…