Constantine Kimanda
Constatine Kimanda alikuwa ni beki wa kati au mkoba wa Yanga na timu ya taifa ya Burundi na sio Congo DRC.
Ilikuwa ni mwaka 1994 alipochezea Yanga ambapo alisajiliwa chini ya uongozi wa katibu mkuu wa wakati ule marehemu George Mpondela.
Alikuwa pamoja na marehemu Method Mogella ambae waliuzwa wote na Mpondela kwenye timu ya uarabuni ya Sharjah FC.
Yanga ya mwaka 1994 ilikuwa ni kali kwelikweli kina Steven Nemes Sekilojo Chambua, Mohamed Hussein au "Mmachinga", Nico Bambaga, Edibily Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo", na Salvatory Edward.
Wengine akina Said Mwamba Kizota, marehemu Salum Kabunda "Ninja", Issa Athuman, Keneth Mkapa, Selemani Mkati, Rifati Said, Sanifu Lazaro, David Mjanja na Mwanamtwa Kihwelu.
Wachezaji wengine walikuwa ni Allly Yusuf "Tigana", Willy Martin, Ngadu Ramadhan, Joseph Lazaro, Willy Mtendamema.
Mwaka 1994 ndipo kulitokea mgogoro mkubwa kwenye klabu hii na kukazaliwa Yanga Asili na Yanga kampuni.
Hivyo Yanga kampuni chini ya Marehemu Mpondela ikaenda kufungwa goli 4-1 na Simba na baaada ya hapo wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wakatimuliwa.
Kimanda ndiye aliefunga goli pekee la Yanga.
Baada ya mgogoro huo kipa Rifat Said alirudi Zanzibar, Edibily Lunyamila akaenda Malindi ya Zanzibar na Saidi Mwamba pamija na Steven Nemes wakahamia Simba.
Ndipo Kocha wa Yanga Tambwe Leya akaamua kusuka kikosi kipya cha Yanga kilichokuwa na wachezaji kama Anwar Awadh, Mzee Abdallah, Silvatus Ibrahim “Polisi”, Maalim Saleh “Romario”, Nonda Shaaban “Papii”, Bakari Malima na Kally Ongala.
Wengine akina Seki Chambua Salvatory Edward na wengine.
Vijana hawa waloitwa Black Stars ndiyo waloiwezesha Yanga kuja kucheza nane bora mwaka 1998 ya klabu bingwa Afrika na baadae mwaka 1999 wakanyakuwa ubingwa wa Afrika Mashariki.
Edibily Lunyamila na Mohamed Hussein.
Kimanda kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Ubelgiji.