Nikasema leo niangalie huyu wanaesema Pele alikuaje enzi hizo. Kweli alikuwa nuksi

Sababu babu pele si saiz yao.

Kila mmoja na mtazamo wake. Wewe utasema pele mwingine atakuja na kusema Maradona. Ukweli halisi na utabakia kuwa ukweli. Messi ndiye Mfalme wa wote....kigezo sio kubeba kombe, tunaangalia performance na kuisaidia mataji timu yake. Messi atabakia kuwa juu ya wote.
 
Kuwazungumzia Pelle na Maradona ktk kipengele cha kuwafananisha na kuwatofautisha nani ni zaidi ya mwenzie ni ngumu coz wengi hatujaowaona zaidi uingie google


Ila ni rahisi sana kuwafananisha na kuwatofautisha Messi na CR7 maana hawa tunawaona wakiweka records mbali mbali za dunia pia kuzivunja
 
Nampenda mnoo mfalme messi, ila hajamfikia mfalme pele
 
hakuna bondia kama Ali..anapigana unaona kabisa hela na muda wako unaenda kihalali..achana na ngumi njaa za akina Tyson..Ali anakupiga huku anakutukania mamaako
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Asante kiongozi___but Pele alichomzidi Mfalme ni makombe ya dunia tu ambayo ile ni teamwork.
Sikia mkuu mie siongei kishabiki sababu ni mpenzi mkubwa wa king messi..

Messi anamkaribia pele kwa ukaribu tu, bila hiyana nasema pele kamzidi messi..
Sawa makombe ni team work lakin ujue perfomance ya mmoja mmoja inahusika.

Wewe niambie kitu ambacho messi kabarikiwa pele hakuwa nacho.
 
Kwangu andunje teja hamfikii hata andunje modern..

Maradona na messi mpira wao unafanana kila kitu, ila maradona kazidiwa dribbling ya messi ni nzuri zaidi, messi ni mwepesi kuliko alivyokuwa maradona, messi yuko na speed zaidi. Mengine wako sawa
Humjui Maradona wewe.
 

Ingia youtube umuone mhuni Diego akitandaza soka,, cheki hapa uje na feedback kamanda...

Wafalme original ni wawili tu duniani, waliobakia ni makapi:
KING MESSI10s
KING DIEGO10s


 
Enzi hizo hakukuwa na offside full kuvizia na mabeki walikuwa mashoga shoga
Usisahau kuwa kulikuwa hakuna red card

Usisahau kulikuwa hakuna substitution

Usisahau kulikuwa hakuna penalty za mwisho yaani mkidraw mnarudia mechi kesho yake asbuhi

Ndio hapo pele alichomoza so msitafute pa kujifichia
 
Ingia youtube umuone mhuni Diego akitandaza soka,, cheki hapa uje na feedback kamanda...

Wafalme original ni wawili tu duniani, waliobakia ni makapi:
KING MESSI10s
KING DIEGO10s


Puskas unamuacha wapi mkuu huyo kwangu ndio all time best hana wa kufananishwa naye hapa duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…