Nikiangalia comment za vijana wa kitanzania kuhusu maandamano ya Kenya ni kama mnatamani ila mnashindwa nani aanzishe. Msithubutu tuipende nchi yetu

Nikiangalia comment za vijana wa kitanzania kuhusu maandamano ya Kenya ni kama mnatamani ila mnashindwa nani aanzishe. Msithubutu tuipende nchi yetu

Habr wanjf. Ukweli nimekuwa nikufautilia kwa ukaribu siasa na uchumi wa Kenya .pia maono ya watu mbalimbali, kisaikolojia ukisoma comment nyingi inaonesha wazi vijana wengi wameshaanza kujiona wako tofauti na vijana wa nchi jirani au nchi zingine. Hivyo imekuwa kama mfano halisi kwao. Naomba niwasihi vijana msijaribu kumfanya hivyo, Kila mtu ananjia yake ya kufanikiwa wenzetu wamezoea fujo sisi sio wao, tujitafakari. Amani ya nchi yetu ni tunu yetu. Kamwe tusifuate njia potofu kudai haki. Naomba kuwasilisha.
Umeongea point bro
 
Bongo tuna Maisha ya kujitosheleza, mfano unaweza kuwa maskin bado ukawa na hekali za mashamba,unaweza kuwa na maisha magumu bado unaweza ukaishi ndugu na washikaji..tofauti na kenya ni ichi yenye nature ya kibepali long time ago..ukiwa na maisha magumu ni magumu kweli na hamna msaada
 
Wapigania uhuru wengi wa africa walikua na ajenda zao binafsi na sio kuleta maendeleo ya kweli nchini mwao waliwadanganya wafrica wenzao wakatuingiza mkenge tukawafurusha wakoloni matokeo yake wametufikisha apa tulipo sasa.
Kumbuka hatujawafukuza wakoloni kabisa kabisa hasa huyo aitwaye marekani so usilaumu wapigania uhuru
 
Ngoja ni swala la muda.. Vijana wengi wana elimu ya kidato cha 4. Ni elimu tosha yakuanza ku question mambo kadhaa ya serikali na utendaji wake. Hii siyo Tanzania ya giza tena. Wataogopa sasa ila iko siku watachoka
 
Kenya maandamano ya pili hadi watu wazima wamejiunga na vijana kuandamana. Tz hakuna uzoefu wa kuandamana kibabe kama kenya. Mkuu wa mkoa akipiga mkwara asijitokeze mtu kuandamana atakabiliana na polisi, wote wanafyata mkia hakuna wa kuandamana
Arusha Mbeya Mara,Iringa na Mtwara ni potential for mass explotion. Hii mikoa inaweza kuwa chimbuko la maandamano makubwa km Kenya isipoangaliwa. Ni wazoevu wa resistence kitambo.
 
Habr wanjf. Ukweli nimekuwa nikufautilia kwa ukaribu siasa na uchumi wa Kenya .pia maono ya watu mbalimbali, kisaikolojia ukisoma comment nyingi inaonesha wazi vijana wengi wameshaanza kujiona wako tofauti na vijana wa nchi jirani au nchi zingine. Hivyo imekuwa kama mfano halisi kwao. Naomba niwasihi vijana msijaribu kumfanya hivyo, Kila mtu ananjia yake ya kufanikiwa wenzetu wamezoea fujo sisi sio wao, tujitafakari. Amani ya nchi yetu ni tunu yetu. Kamwe tusifuate njia potofu kudai haki. Naomba kuwasilisha.
Wakenya wanaipenda sana nchi yao ndiyo sababu wanakerwa na hujuma wanazozifanya viongozi, wakenya wanataka waujue kila mkopo unaofanywa ni kwa ajili ya nini tofauti na sisi maradi unagharamiwa na pesa za ndani kisha mradi huohuo unakopewa pesa toka nje! Ukweli hatuipendi nchi yetu ndiyo sababu miradi mingi inahujumiwa na kufa tukiacha viongozi wanagawana hiyo miradi, viwanda vingi vimekufa bila sababu na miradi kama Udart imekufa huku tukiichekea kama vile si yetu. Huko Kenya ni vigumu kusikia kiwanda kimefungwa, viwanda vyao vingi vipo toka miaka ya 50 na vipo katika ubora mkubwa, kuna viwanda vya Kenya vilikuwepo hapa tukavibinafsisha na kuviua huku Kenya bado vipo! Tumeua viwanda vyote vya nguo na kugeuza baadhi kuwa vituo vya mabasi, machinjio ya ng'ombe na viwanda vya uponyaji wa akina Mwamposa! Akili gani hiyo! Tanga kulikuwa na viwanda vikubwa hivi sasa hakuna, viwanda vya zana za kilimo tumeviua vyote na mitambo kuuza kama vyuma chakavu!
Unafurahi kuona nchi inakufa huku tukiitazama kwa madai ya kuipenda nchi yetu! Huu ni ujinga uliokithiri.
 
Habr wanjf. Ukweli nimekuwa nikufautilia kwa ukaribu siasa na uchumi wa Kenya .pia maono ya watu mbalimbali, kisaikolojia ukisoma comment nyingi inaonesha wazi vijana wengi wameshaanza kujiona wako tofauti na vijana wa nchi jirani au nchi zingine. Hivyo imekuwa kama mfano halisi kwao. Naomba niwasihi vijana msijaribu kumfanya hivyo, Kila mtu ananjia yake ya kufanikiwa wenzetu wamezoea fujo sisi sio wao, tujitafakari. Amani ya nchi yetu ni tunu yetu. Kamwe tusifuate njia potofu kudai haki. Naomba kuwasilisha.
Amin kwenye miaka 10 ijayo, nchi nyingi za Africa zitakuwa na machafuko.
 
Back
Top Bottom