Nikifugia samaki kwenye kisima watakubali? Kambale

Nikifugia samaki kwenye kisima watakubali? Kambale

Hii imekaa vyema mkuu

Unawapa chakula gani ?
Na
Ikikupendeza tupe ABC kuhusu huo ufugaji nimetokea kuvutiwa nao🤔
Nilikwenda maonyesho ya 88, nikaona Ruvu JKT wamefuga samaki kwenye tank bandani kwao, nikawauliza kama naweza kufanya hivyo nyumbani kwangu, wakasema inawezekana.
  1. Andaa tank liwe na inlet na outlet kwaajili ya kubadili maji, liweke kwenye eneo lenye hewa ya kutosha
  2. Weka maji yasipungue kina cha mita 1.2 (yasiwe na dawa, kama yana dawa subiri iondoke/evaporate)
  3. Weka udongo laini (wenye rutuba) chini angalau thikness ya sm 15
  4. Weka samadi kiasi ili kubadili rangi ya maji kuwa kijani kupunguza direct sunlight na ni kirutubisho pia
  5. Endelea kuwapa chakula humo, (kile cha kununua ni kizuri zaidi)
  6. Wasiliana na bibi au bwana samaki mara uonapo huna uhakika kwa tatizo lolote ili akushauri vilivyo
 
Mkuu una picha ya ufugaji wako?, aeration ya maji unaifanyaje? ( hali ya maji kupata Oxygen ya kutosha)
Tank linakatwa juu, tafuta tank lililoharibika likate juu kuondoa lile eneo linalofunika
 
Back
Top Bottom