Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
- Thread starter
- #41
soma mathayo 24:13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. na 24:21-22 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.Kanisa ni mali ya Mungu, wala sio mali ya mtu binafsi, hilo ndilo kanisa la kweli. haliji kwa fikra za nini muanzilishi anapenda kiwe au kisiwe, Roho Mtakatifu ndio anatakiwa akuongoze, kama unaye, na kama umeokoka manake usipookoka hauwezi kumpata Roho Mtakatifu, na kwa jinsi ulivyoandika hapa ni wazi wewe haujaokoka na hautampata Roho Mtakatifu hadi uokoke.
kwa kifupi, unaenda kuanzisha cult ya kishetani kabisa, isiyo na misingi ya Neno la Mungu wala Roho Mtakatifu, na ni shetani anakuongoza kwenda kujenga kitu hiki. hautajua haya ninayoyaongea kwasababu ufahamu wako umetekwa na hautaelewa hadi Mungu akufungue akili yako, kama neema hiyo itakukuta kabla haujafa. rudi kwa Mungu, acha kuwa ajenti wa sheteni.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
Kwamjibu wa aya hizo hadi sasa hayupo hata mmoja aliyeokoka!
Nakuomba usiijiite umeokoka la sivyo utakuwa hujui maandiko hata tone ila umekalilishwa na wachungaji njaa.
karibu kwenye kanisa langu ufunguliwe na uijue kweli halisi. Ahsante