Suffering ipo kila kona ya dunia hii, hakuna kizuri kinachokuja bila ya kujinyima na kutoka jasho.. Soma historia za mataifa makubwa utakutana na kazi ngumu yenye kuongozwa na nidhamu.
Vyuma kukaza ni kila mahali, pesa ikiwa nyepesi sana kupatikana kuna mahali pana shimo kubwa na linateketeza uchumi mzima.
JPM pesa aliyoibana ilijenga miradi mingi na ya maana kwa uchumi mpana. SGR tuliyolia wakati ikianza kujengwa, inakwenda kuufungua ukanda mzima wa kati, ni juu yangu mimi na wewe kufikiria kuzalisha vitu vyenye soko huko nje kuliko kulialia na kulaumu awamu ya JPM ambaye mwezi March mwaka huu inatimia miaka miwili akiwa amelala kaburini Chato.