Wakuu bado hatujafika tunapotaka ila kiukweli kuna hatua tumepiga kwa miaka hii. Haya ni mambo ambayo yalikuwepo ndani tu ya miaka isìyozidi 30.
1. Shule za sekondari zilikuwa chache mno kiasi kwamba kwenye darasa la wanafunzi 60 wanaopata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza labda ni watano tu. Watoto wengi hawakuweza kutimiza ndoto zao kwasababu hiyo. Serikali ilikuwa maskini sana.
2. Nchi ilikuwa na barabara mbovu mno. Barabara za lami zilikuwa za kuhesabu. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 ili ilibidi watu wa kanda ya ziwa waliokuwa wakitokea Arusha na Kilimanjaro wawe wanazungukia Kenya kwenye barabara nzuri badala ya kupitia njia fupi ya Singida. Yalikuwa ni mateso. Sehemu ya kusafiri masaa mawili tulikuwa tunatumia masaa matano hadi sita.
Safari ya Dar - Mtwara ilikuwa funga kazi. Songea - Mbamba Bay nayo ilikuwa safari ya roho mkononi.
3. Miaka ya nyuma ustaarabu ulikuwa mdogo sana hasa kwenye mikusanyiko na vyombo vya usafiri. Ilikuwa kawaida mtu kuvuta sigara kwenye kundi la watu au kwenye basi. Hata customer care zilikuwa za hovyo.
4. Umaskini ulikuwa umekithiri hasa maeneo ya vijijini. Kuvaa nguo zenye viraka ilikuwa jambo la kawaida sana. Siku hizi hiyo hali imepungua. Pia hata yale mambo ya kula pilau hadi kuwe na sikukuu yamepungua. Sasa hivi watu wanafakamia pilau na biriani siku ya kawaida tu.
5. Kulikuwa na taharuki sana kwa mambo yaliyokuwa hayaeleweki... wanyonya damu, popobawa, chunusi na mambo mengine ya kutisha.