Nikikumbuka haya mambo ninakiri kabisa tumetoka mbali na nchi yetu ilikuwa masikini mno

Nikikumbuka haya mambo ninakiri kabisa tumetoka mbali na nchi yetu ilikuwa masikini mno

Wakuu bado hatujafika tunapotaka ila kiukweli kuna hatua tumepiga kwa miaka hii. Haya ni mambo ambayo yalikuwepo ndani tu ya miaka isìyozidi 30.

1. Shule za sekondari zilikuwa chache mno kiasi kwamba kwenye darasa la wanafunzi 60 wanaopata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza labda ni watano tu. Watoto wengi hawakuweza kutimiza ndoto zao kwasababu hiyo. Serikali ilikuwa maskini sana.

2. Nchi ilikuwa na barabara mbovu mno. Barabara za lami zilikuwa za kuhesabu. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 ili ilibidi watu wa kanda ya ziwa waliokuwa wakitokea Arusha na Kilimanjaro wawe wanazungukia Kenya kwenye barabara nzuri badala ya kupitia njia fupi ya Singida. Yalikuwa ni mateso. Sehemu ya kusafiri masaa mawili tulikuwa tunatumia masaa matano hadi sita.

Safari ya Dar - Mtwara ilikuwa funga kazi. Songea - Mbamba Bay nayo ilikuwa safari ya roho mkononi.

3. Miaka ya nyuma ustaarabu ulikuwa mdogo sana hasa kwenye mikusanyiko na vyombo vya usafiri. Ilikuwa kawaida mtu kuvuta sigara kwenye kundi la watu au kwenye basi. Hata customer care zilikuwa za hovyo.

4. Umaskini ulikuwa umekithiri hasa maeneo ya vijijini. Kuvaa nguo zenye viraka ilikuwa jambo la kawaida sana. Siku hizi hiyo hali imepungua. Pia hata yale mambo ya kula pilau hadi kuwe na sikukuu yamepungua. Sasa hivi watu wanafakamia pilau na biriani siku ya kawaida tu.

5. Kulikuwa na taharuki sana kwa mambo yaliyokuwa hayaeleweki... wanyonya damu, popobawa, chunusi na mambo mengine ya kutisha.
Sawa.Ila muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna tija kabisa.
 
Ni kweli umasikini wa mmoja mmoja au wa ujumla ulikuwa wa kutisha mno.

MICHEZO
Jezi za wachezaji zilikuwa zilezile ziliitumika msimu nzima..zilitumika hadi kiwango cha mwisho za kuchakaa kwake.
Na ilikuwa marufuku mchezaji kubadilishana jezi na mchezaji pinzani..

Jezi kuandikwa majina ya wachezaji migongoni ilikuwa ni tukio ghali sana.

ELIMU
Licha ya kukaa chini..madarasa baadhi hayakuwa na sakafu.
Majengo/maboma ya tope.
Halikuwq jambo la kushangaa watoto wakitembea peku kuja shule
NB; KIKWETE mwenyewe Ni victim wa hili..ametusimulia kwny kitabu alichoandika.

Ilikuwa kawaida darasa la 7 lenye watoto 130 kufeli wote (KUTOCHAGULIWA) Wakachaguliwa 4 tu.

MENGINE
Jazeni na nyie...........
 
Imagine hadi miaka ya karibuni TFF walitaka kumuadhibu Nadir Canavaro kwa kubadilishana jezi na mchezaji wa Ivory Coast
 
Chuna ngozi Mbozi Mbeya na Mwanza mpaka Dar washachunwa sana watu ngozi na walikua wanaonyesha mpaka kwenye magazeti

Uliyoandika yote ya kweli sio simulizi za kusadikika chunangozi walikuwepo, nyonyadamu walikuwepo, chunusi wapo, popobawa kawaulize mbagara
Nyonyadamu bado imebakia kuwa fumbo hadi leo.
 
Itakuwa unanufaika na CCM mkuu, sema tu utii ulituponza laiti tungelijua...!
 
Kusini kule watu walikuwa wanavaa magome ya miti,mitumba imekuja kuokoa.
 
Sisi wazee wa zamani tunaona maisha ya miaka 60 nyuma yalikuwa mazuri sana.vyakula vilikuwa vingi na bei ya chini,elimu ilikuwa ya kiwango Cha juu kiasi kwamba mtu aliyefika shule ya upili aliweza kusimamia wizara na mambo yakaenda vizuri tofauti na Sasa,Majengo ya kipindi hicho yalikuwa imara sana na ajira zilikuwa nyingi kutokana na viwanda kuwa vingi ambapo Kwa Sasa vingi vimekufa.Sisi wazee tumekumbuka sana maisha mazuri ya kipindi hicho kabla mchwa wa Sasa hawajaiharibu Nchi yetu
 
Hakuna kitu kama hicho ndugu. Hao wenye shule ya upili ndo walikuja na sera za kijinga hadi viwanda vikafa. Na kama walikuwa vizuri ilikuwaje kwa miaka yote aliyotawala Nyerere kuwe na kilometa za lami zisizozidi 5000 tu? Daraja la mkapa kwenda kusini kalijenga Mkapa. Wazee wa zamani wangekaa tu kimya kulinda heshima zao. Wao ndo waliosaini mikataba ya hovyo sana inayoligharimu taifa hadi leo hii.
 
[/

Hapana mikataba mibovu imeanza baada ya Nyerere kusitaafu.ardhi ikaanza kuuzwa hovyo,mikataba ya madini mibovu kama hii tu ya bandari zetu.kuhusu km Chache ni kutokana ma mapato ya kipindi hicho.kile tulichokipata kiliendana na miradi ya kipindi hicho.ufanisi ulikuwa mkubwa tofauti na sasa.kwa Sasa kiongozi anaona fahari kutembelea v8 ya milion600 kuwatembelea wanakijini ambao hawana huduma muhimu za kijamii.Sisi wazee wa zamani tulifurahia sana maisha hadi tunatamani siku zirudi nyuma miaka 60.
 
Mpaka leo hii bado sijaelewa kama chunusi ni mnyama halisi au kiumbe cha kusadikika tu.
Kuna uwezekano hili neno lilianzishwa kigoma. Watu walikuwa wakipigwa shoti na samaki wa shoti wanasingizia chunusi. Ila huku ziwa nyanza hizo imani zililetwa kutokana na watu wanaodondoka kwenye mkondo mkali mwembamba wa maji. Inamaana kuna mkondo mpana wa maji. Huu haunaga madhara
 
Back
Top Bottom