Nikikumbuka haya mambo ninakiri kabisa tumetoka mbali na nchi yetu ilikuwa masikini mno

Sawa.Ila muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna tija kabisa.
 
Ni kweli umasikini wa mmoja mmoja au wa ujumla ulikuwa wa kutisha mno.

MICHEZO
Jezi za wachezaji zilikuwa zilezile ziliitumika msimu nzima..zilitumika hadi kiwango cha mwisho za kuchakaa kwake.
Na ilikuwa marufuku mchezaji kubadilishana jezi na mchezaji pinzani..

Jezi kuandikwa majina ya wachezaji migongoni ilikuwa ni tukio ghali sana.


ELIMU
Licha ya kukaa chini..madarasa baadhi hayakuwa na sakafu.
Majengo/maboma ya tope.
Halikuwq jambo la kushangaa watoto wakitembea peku kuja shule
NB; KIKWETE mwenyewe Ni victim wa hili..ametusimulia kwny kitabu alichoandika.

Ilikuwa kawaida darasa la 7 lenye watoto 130 kufeli wote (KUTOCHAGULIWA) Wakachaguliwa 4 tu.

MENGINE
Jazeni na nyie...........
 
Imagine hadi miaka ya karibuni TFF walitaka kumuadhibu Nadir Canavaro kwa kubadilishana jezi na mchezaji wa Ivory Coast
 
Nyonyadamu bado imebakia kuwa fumbo hadi leo.
 
Itakuwa unanufaika na CCM mkuu, sema tu utii ulituponza laiti tungelijua...!
 
Kusini kule watu walikuwa wanavaa magome ya miti,mitumba imekuja kuokoa.
 
Sisi wazee wa zamani tunaona maisha ya miaka 60 nyuma yalikuwa mazuri sana.vyakula vilikuwa vingi na bei ya chini,elimu ilikuwa ya kiwango Cha juu kiasi kwamba mtu aliyefika shule ya upili aliweza kusimamia wizara na mambo yakaenda vizuri tofauti na Sasa,Majengo ya kipindi hicho yalikuwa imara sana na ajira zilikuwa nyingi kutokana na viwanda kuwa vingi ambapo Kwa Sasa vingi vimekufa.Sisi wazee tumekumbuka sana maisha mazuri ya kipindi hicho kabla mchwa wa Sasa hawajaiharibu Nchi yetu
 
Hakuna kitu kama hicho ndugu. Hao wenye shule ya upili ndo walikuja na sera za kijinga hadi viwanda vikafa. Na kama walikuwa vizuri ilikuwaje kwa miaka yote aliyotawala Nyerere kuwe na kilometa za lami zisizozidi 5000 tu? Daraja la mkapa kwenda kusini kalijenga Mkapa. Wazee wa zamani wangekaa tu kimya kulinda heshima zao. Wao ndo waliosaini mikataba ya hovyo sana inayoligharimu taifa hadi leo hii.
 
 
Mpaka leo hii bado sijaelewa kama chunusi ni mnyama halisi au kiumbe cha kusadikika tu.
Kuna uwezekano hili neno lilianzishwa kigoma. Watu walikuwa wakipigwa shoti na samaki wa shoti wanasingizia chunusi. Ila huku ziwa nyanza hizo imani zililetwa kutokana na watu wanaodondoka kwenye mkondo mkali mwembamba wa maji. Inamaana kuna mkondo mpana wa maji. Huu haunaga madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…