Nikinywa Pombe Silewi, je ni tatizo la kiafya au ni faida?

Nikinywa Pombe Silewi, je ni tatizo la kiafya au ni faida?

wazirib28

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
460
Reaction score
275
Wakuu... mara kadhaa huwa napitia matatizo fulan na huwa natamani hata kulewa ili angalau niyasahau kwa muda mfupi. Lakini sijui ni tatizo au ni faida... kila nikinywa pombe kiasi chochote kile lakini silewi. Kuna siku nilikunywa konyagi mbili lkn sikulewa hata kidogo. Wataalamu wa haya masuala naomba mnisaidie kujua kama hili ni tatizo kiafya au ni faida kiafya. Nawasilisha.
 
kunywa konyagi nne halafu uje na mrejesho kama hujalewa kuna watu watajiuzulu.
Mkuu kuzidisha aina nyingine za vilevi huwa vinaua. Ila kiukweli nimejaribu kutumia pombe za aina nyingi lakini sijawahi kulewa.
 
Ule bapa 3 usilewe au ulikuwa inakunywa visichana 2 tu ukasema konyagi mbili piga bapa 2 uone kama hata wewe ujajisahau.
Ndugu... mimi silewi kabisa. Na nimerithi toka kwa baba yangu. Naye ana tatizo kama hilo.
 
Njoo siku nikueleweshe mana ukinywa mwenyewe huelewi
 
Uliona wapi mlevi akakiri amelewa ????
Kwasababu hata nikiwa na wenzangu tunakunywa pamoja basi mimi ndo nitakuwa salama na kuanza kuwasaidia wenzangu. Huwa nipo fresh tu. Lakini pia watu huwa wananishangaa sana kwasababu huwa wananiona nikiwa nakunywa lakini hawaoni nikiwa nimelewa.
 
Acha utani wewe. Usiombe ukutane na mimi alafu usilewe. Nakwambiaje hujakunywa pombe bado. Pombe haziongopi hata uweje
 
Jamani watu mnadhani natania lakini huo ni ukweli na naomba kama kuna daktari mjuzi wa hayo mambo aje ayaelezee
 
Kama Kunywa Bia imeshindikana kulewa Hebu Kanywe Gongo uangalie Matokeo Yatakuja Vipi..
 
Kama Kunywa Bia imeshindikana kulewa Hebu Kanywe Gongo uangalie Matokeo Yatakuja Vipi..
Gongo tumenyweshwa sana na mama utotoni kama dawa ya minyoo (ila kipindi hiki hatengenezi). Sijawahi kulewa
 
Back
Top Bottom