Nikiona ajali hii, mengi najifunza

Nikiona ajali hii, mengi najifunza

Nadhani hili ndilo lilikuwa hasa lengo la uzi wako; na mengineyo yote ni mbwembwe tu ndiyo maana kichwa cha uzi na yaliyomo yamepishana; na ama yamelazimishwa lazimishwa tu.

Halafu eti. Mimi nisiye mwislamu naweza kuisoma Qurani bila kudhurika? Kuna ostaadh alishawahi kunitisha kuwa eti Qurani haipaswi kushikwa (achilia mbali kusomwa) na mtu ambaye siyo mwislamu maana madhara yake ni makubwa. Kuna ukweli katika hili? Asante [emoji1545]
Yupo kutoa daaaaawa [emoji1787]

Anatuzuga na habari za Sauli
 
Pana gari ilijifinyanga kama hiyo milima ya Chirundu na wote walitoka salama Mungu ndio mpangaji wa kila kitu hiyo gari inavyoonekana iligongwa kwa nyuma na gari kubwa harafu ikiwa kwenye mwendo ikapinduka pinduka mara kadhaa...
 
photo_5873058260918059656_x.jpg

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Katika ajali hio ambayo tunaambiwa alikuwepo mtoto mdogo lakini amechubuka kidogo sana . MASWALI YA KUJIULIZA
1. Huyu mtoto alipona vipi?
2. Alikaa wapi?
3. Nini kilichomuokoa?
4. Kwanini asife?
Maana hii gari ukiona hakuna sehemu ambayo haijapindana, kwa mazingira ya kawaida ni vigumu kutoka mtoto

Katika Qurani, kuna aya nyingi zinazosema kuhusu nguvu ya neno la Mungu na jinsi anavyoleta matokeo kwa maamuzi yake. Kwa mfano, katika sura ya 2, aya ya 117, inasema:

"Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa mbingu na ardhi na kila kilicho baina yake. Aliposema jambo tu, huwa: ‘Kuwa!’ Na linakuwa."

Aya hii inasisitiza jinsi Mungu anavyokuwa na uwezo wa kutekeleza maamuzi yake kwa nguvu ya neno lake peke yake. Ni mfano wa uweza wa Mungu na jinsi anavyoweza kuunda na kubadilisha mambo kwa matakwa yake.

Qurani inafundisha kwamba kila jambo linalotokea, likiwemo kifo na uhai, linatokana na mapenzi na uamuzi wa Mungu. Kwa mfano, katika sura ya 3, aya ya 145, inasema:

"Hakika kifo kilichoandikiwa ni hakika, na hakika kifo kitakutokea kwa wakati ulioandikwa."
SOMA QURAN UPATE ILIMU

Qurani inaelezewa kama kitabu kisichoshaka kwa sababu ya imani ya Waumini kwamba ni neno la Mungu lililo wazi na lenye ukweli wa kipekee. Katika sura ya 2, aya ya 2, inasema:

"Huu ndio mubini, usiomashaka, uliojaa udhu na uwazi kwa wale wanaomcha Mungu."

Aya hii inasisitiza kuwa Qurani ni kitabu kilicho wazi na kimejaa maelekezo na mwangaza kwa wale wanaoamini. Qurani inaaminiwa kuwa ni muongozo wa kweli na kamili kwa maisha ya kiroho na kimaisha, na hivyo Waumini wanakubaliana kwamba kuna ukweli na hekima ya kipekee ndani yake.
Hapo mtoto alifunga mkanda, baba mtu hajafunga mkanda ndio maana akawahi kuisha.
 
wewe umepaona hapo tu? hukuona picha ya gari? any way
Katika Qur'an, kuna aya ambazo zinaeleza kwamba ujumbe wa Mungu umefikiwa kwa walimwengu wote, na si kwa watu wa kabila au taifa fulani tu. Hii inathibitishwa na aya kama:

  • Sura Al-Anbiya (21:107): "Na hatukukutuma ila kama rehema kwa walimwengu wote."
    Aya hii inasisitiza kwamba Mtume Muhammad (S.A.W.) ametumwa kama rehema kwa watu wote bila kujali taifa au kabila.
  • Sura Al-Hujurat (49:13): "Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke, na tukakufanyeni mataifa na makabila ili mpatane. Hakika aliye bora kwenu mbele ya Allah ni yule mwenye kumcha Allah zaidi. Hakika Allah ni Mjuzi, Mwenye Hekima."
Kuran nacho ni kitabu cha Mungu au uganga! Kuna tofauti kwani.

Naomba msaada.
 
Mtoto alifungwa Belt Baba akasahau ni hicho tu.
 
Sio hao. wakti wa Mtume kulikuwa na makafiri wakubwa walikuwa na akili hizo hizo, lkn siku ya siku ndio wakawa wanapita kuwaambia makafiri waliobaki kuikubali Quran
Na makafiri wenyewe mlioikubali Quran ndiyo nyinyi kima Malaria 2
 
matukio kama haya ya kunusurika yanatumika na wengi kama uthibitisho wa uwepo wa mungu

ni sawa

lakini kwangu naona walakini
Hajiulizi matukio kama school bus kuua watoto kama wote, achilia mbali bodaboda. Huu ni uthibitisho dhaifu kupita kiwango, hajui mimba ngapi hutolewa na zinafanikiwa? Mungu ni zaidi ya hizo bible na Qur'an.
 
Mtoto ana umbo dogo nivigumu kufikiwa na mgongano wa ajari........
Upo sahihi. Nilitaka kuuliza umri wa huyo mtoto.

Ni kawaida kabisa kwa watoto wadogo mara nyingi ambao hata hawawezi kutembea kukuta wamenusurika kwenye ajali kubwa.
 
RIP.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, ajali isingewezekana kuwapo popote.

Kuwapo kwa ajali ni ushahidi huyo Mungu hayupo.
Na hata kama yupo hawezi kukubali kufanywa kuwa bidhaa ya kuuzwa hovyo hovyo kama anavyofanywa kuwa na hizi dini.
 
Nadhani hili ndilo lilikuwa hasa lengo la uzi wako; na mengineyo yote ni mbwembwe tu ndiyo maana kichwa cha uzi na yaliyomo yamepishana; na ama yamelazimishwa lazimishwa tu.

Halafu eti. Mimi nisiye mwislamu naweza kuisoma Qurani bila kudhurika? Kuna ostaadh alishawahi kunitisha kuwa eti Qurani haipaswi kushikwa (achilia mbali kusomwa) na mtu ambaye siyo mwislamu maana madhara yake ni makubwa. Kuna ukweli katika hili? Asante 🙏🏿
Mikwara tuu
 
Juzi juzi tu like 2 weeks, kulitokea ajali ya bajaji kugongwa na gari IST dereva na abiria wake walifariki, wamepishana kama masaa mawili tu. Kwenye bajaji kulikuwepo mtoto wa kike wa huyo dereva wa bajaji ana miaka 4....kapona hajaumia!
Ila saa nyingine tunatakiwa tugawqne majukumu. Wapo madereva wazuri tu kazibyao ni kuendesha tajir tafuta dereva akuendeshe mpakq yendako unlike basi
 
Sauli ni kama kuku alidonoa maindi ya kuishia mwaka huu!!?? Maaana inafikirisha sana ni kama alijua hawezi toboa mwaka huu ndo maana akauza polo zake kwa katarama na hakutaka kureplace zingine yani kwa ufupi hakuwa serious na biashara yake tena ya mabasi wakati ndo yalikuwa kwenye peak
 
photo_5873058260918059656_x.jpg

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Katika ajali hio ambayo tunaambiwa alikuwepo mtoto mdogo lakini amechubuka kidogo sana . MASWALI YA KUJIULIZA
1. Huyu mtoto alipona vipi?
2. Alikaa wapi?
3. Nini kilichomuokoa?
4. Kwanini asife?
Maana hii gari ukiona hakuna sehemu ambayo haijapindana, kwa mazingira ya kawaida ni vigumu kutoka mtoto

Katika Qurani, kuna aya nyingi zinazosema kuhusu nguvu ya neno la Mungu na jinsi anavyoleta matokeo kwa maamuzi yake. Kwa mfano, katika sura ya 2, aya ya 117, inasema:

"Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa mbingu na ardhi na kila kilicho baina yake. Aliposema jambo tu, huwa: ‘Kuwa!’ Na linakuwa."

Aya hii inasisitiza jinsi Mungu anavyokuwa na uwezo wa kutekeleza maamuzi yake kwa nguvu ya neno lake peke yake. Ni mfano wa uweza wa Mungu na jinsi anavyoweza kuunda na kubadilisha mambo kwa matakwa yake.

Qurani inafundisha kwamba kila jambo linalotokea, likiwemo kifo na uhai, linatokana na mapenzi na uamuzi wa Mungu. Kwa mfano, katika sura ya 3, aya ya 145, inasema:

"Hakika kifo kilichoandikiwa ni hakika, na hakika kifo kitakutokea kwa wakati ulioandikwa."
SOMA QURAN UPATE ILIMU

Qurani inaelezewa kama kitabu kisichoshaka kwa sababu ya imani ya Waumini kwamba ni neno la Mungu lililo wazi na lenye ukweli wa kipekee. Katika sura ya 2, aya ya 2, inasema:

"Huu ndio mubini, usiomashaka, uliojaa udhu na uwazi kwa wale wanaomcha Mungu."

Aya hii inasisitiza kuwa Qurani ni kitabu kilicho wazi na kimejaa maelekezo na mwangaza kwa wale wanaoamini. Qurani inaaminiwa kuwa ni muongozo wa kweli na kamili kwa maisha ya kiroho na kimaisha, na hivyo Waumini wanakubaliana kwamba kuna ukweli na hekima ya kipekee ndani yake.
Mungu ndie hakimu wa maisha yetu.Hutuvuna wakati anaotaka.
Jina lake lihimidiwe.
Poleni Ndg,Jamaa,Waliopoteza mpendwa wao.
Mungu awe mfariji wenu.
Amin.
 
We umeona mtoto tu,kuna ajali mbaya zaidi ya hiyo kwenye gari kukiwa na trey za mayai na halikuvunjika hata moja.
 
Back
Top Bottom