Nikishatofautiana na WIFE, Michepuko naiona kama takataka

Shikilia hapo hapo, Kama ulishindwa kuomba msamaha mwanzoni kausha kabisa, Ila mfanyie suprise yoyote ya zawadi atafurahi naimani unajua anapenda nini, ukijishusha kwasasa utaharibu kilakitu.
Hiki ndicho kinawaponza vijana! Kushupaza shingo mwamba haisaidii ni kuendelea kuumizana tu! Hilo la kumtoa out lina mashiko sana.
 
Sasa kwa taarifa yako broh hii kitu huwa inakera ila ulikosea wewe mwenyewe mpaka kumshikilia bango na kesi kufika kwa wazazi.

Kwa mwanaume mstaarabu akikosea, daima hukiri kosa na mwanamke mstaarabu hivyo hivyo uhimili makasiriko nakukemea majanga yasitokee.

Wewe mwenyewe umeharibu, kiri kosa lako kwa wazazi, eleza scenario nzima na wife wako awepo huku ukiomba msamaha.
 
Niko calm ndo maana najishusha,kuwai kurudi nyumbani ila wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa inategemea kwa kiasi gani upo tayari kujishusha na kutatua changamoto iliyopo kwa mafinikio ya muda mrefu. Uzuri ni kwamba we mwenyewe unajua ulipoenda mrama, lakini kuyafukia machungu ya mwengine kwa vijizawadi au attention kunafukia tu machungu ya sasa lakini mwisho wa siku hayo machungu yakikua sana lazima mtu atafute pa kuyatolea na mara nyingi inakua "maji yakishamwagika hayazoleki" mkajikuta mnafikishana pabaya zaidi.
.
Chukulia huu mfano, upo na boss wako na wewe msaidizi wake, katika biashara/ kazi mkawa mnataka kufanya jambo la maendeleo lakini kila ukimpa boss mawazo yako hayatilii maanani (hili sio jambo baya mana akifanikiwa atakua ameshinda vizuri, kuwa na wazo lako na kulisimamia ni jambo jema) alafu baadae wazo lake likafeli na mambo yakawa vibaya ofisini vyuma vikakaza, sasa katika kutafuta suluhisho mkabishana na boss alafu kwa bahati mbaya ukasema "sema we boss huna akili, mbinafsi sana" na hayo maneno 'huna akili' yakaingia akilini mwa boss na akakumind na kukutishia kukufukuza kazi kwa kuwa anajua kabisa huna chanzo kingine cha kipato hivyo utaomba tu msamaha, kisha akanisemea kwa bodi ya wafanyakazi na wewe ukaonekana mbaya, na mbaya zaidi, ukaonekana ndio uliyesababisha hasara na chanzo cha ugomvi.

Na wewe kwa kuwa hapo ndo sehemu yako ya kupata tonge ukajishusha ili mambo yasiwe mengi ukaomba msamaha na kwa juu juu ikaonekana mambo yameisha ila ndani mwako kuna chuki inakua imejitengeneza na inakutafuna kila ukifikiria kwamba yote hayo kasababisha boss alafu we ndo unatembea na fedheha kila iitwapo leo. Alafu ghafla boss anakuja anakupa vizawadi na anakuambia atakupandisha mshahara wakati hata hamjawahi kukaa kuongea kuhusu kilichotokea wala hujawahi kuyatoa yako ya moyoni, je, utamchukuliaje?
.
Utatuzi.
Kama ukiwa tayari kuyamaliza kwa ajili ya furaha ya muda mrefu, usianze na vizawadi na attention, hivyo viwe kama vikolombwezo tu, cha kufanya mkae muongee.
Kwenye kuongea huko wewe nafasi yako ni moja tu, Kuuliza Maswali zaidi ya kujitetea. Mfanye aongee ili ujue kiundani nini kinamkwaza zaidi apo ndo utajua unatatuaje tatizo lililopo, wanawake wanatatua matatizo yao kwa kuongea.
Na mkiongea vizuri kesho unaweza kutuletea stori za kitandani humu haha.
Lakini mpe sharti kwamba aongee kwa utulivu, kama anapayuka payuka kwa utulivu mwambie, leo nilikua nina mudi ya kukusikiliza wife lakini umenikata stimu so, ukiwa kwenye hali ya utulivu ndo tutaongea. Kisha mwache mpe muda.
Think Long Term Brother, Good Luck.
 
100 % very true,Amani/Furaha huwa inaanzia nyumban then mambo mengine ya njee ndo yanaendelea vizur hii ni kwa Kila kitu including uchepukaji.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Hiki ndicho kinawaponza vijana! Kushupaza shingo mwamba haisaidii ni kuendelea kuumizana tu! Hilo la kumtoa out lina mashiko sana.
Kama alishindwa mwanzo iweje afanye mwisho, alienda Hadi kwa wazazi na ikaonekana mwanamke ndio anakosa iweje ajishushe? ukisimamia msimamo simama kweli kweli,
 
Yes huwa napenda uongelee mkeo sio mchepuko kila uchao.

Fanya hivi;
Chagua siku uwahi nyumbani.
Mtoe out mahali tulivu sana.
Mpatie chakula na kinywaji bora akipendacho.

Baada ya maakuli na mkiendelea kunywa.
Hebu ongea naye taratibu huku ukiwa umemlaza kifuani.
Msifie sana na mkumbushe nyakati za furaha na mwisho muombe msamaha na umwahidi kuwa utakuwa unazingatia ushauri wake.

Ninaamini atalegea na kukusamehe na ukiona amelegeza mpeleke hotelini mmalizane kabisa mrudi home mkiwa mmekula na kukulana kabisa
 
Mhm madini tupu, akifuata huu ushauri ndoa imepona
 
Depoond ww ni aliwatani ila kwa ili umeniangusha sana mwamba
 
Kuna namna yangu kuomba radhi,
Ila kuomba straight nilishindwa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Hapo kwny kukiri kipengele sn mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushaur mwanana kabisa huu,
Sio Siri nmepata maarifa mapya hapa[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu ya out imekaa POA sn,
Japo Ratiba imenibana ila Ntaifanyia kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…