Idadi ya mifuko hadi sasa ni 6:
Ukwasi| Jikimu| Wekeza Maisha | Umoja | Hatifungani | Watoto.
1. Sasa unaweza kuuza vipande vyako kwa njia ya menu ya simu, siminvest *150*82#. Nenda eneo wameandika "Kuuza Vipande". Ukomo ni milioni 2 kwa siku.
2. Ukishafanya zoezi la kuuza au kutoa hela basi utatumia ndani ya muda usiozidi siku 3 kupata hela yako katika akaunti ya benki ulojaza wakati unafungua au kukamilisha usajili wako. Ndani ya siku 3 za kazi ni kwa mfuko wa Ukwasi/Liquid Fund huku mifuko mingine ni ndani ya siku 10 za kazi. #Siku za kazi ni J3 hadi Ijumaa#.
3. Unaweza kufungua akaunti yako kwa njia karibu 6 ( kwa njia ya simu *150*82#, Utt amis app, kujaza fomu mtandaoni, CRDB benki au kutembelea ofisi za UTT AMIS ). Kwa njia ya simu na app utaweza kuendelea kununua vipande/kuweka hela ila itakusumbua kutoa endapo hutakamilisha usajili wako.
4. Unaweza kutumia njia mbalimbali kuchangia/kuweka hela yako UTT AMIS. Kuanzia kuweka kwa njia ya benki ( CRDB, NMB, NBC), njia ya benki mtandaoni ( CRDB simbanking, NMB mkononi), mawakala ( CRDB), Utt amis app na mitandao ya simu yote nchini hadi Azam Pesa.
5. Unapoweka pesa yako unaweza kufuatilia salio ndani ya siku 3 za kazi kwa njia hizi: kwa siminvest menu *150*82# ( uliza salio), UTT AMIS app na tatu kuomba statement yako kupitia
uwekezaji@uttamis.co.tz
6. Unaweza kufungua akaunti ya mtu mmoja ( individual account) au akaunti ya pamoja ( Joint account) kwa mtu zaidi ya mmoja ( wenza), vikundi, taasisi na asasi mbalimbali
7. Unaruhusiwa kufungua mfuko zaidi ya mmoja kulingana na malengo yako wewe yalivyo. Unaruhusiwa kuwekeza kusikokuwa na ukomo.
8. Unaruhusiwa kurithisha vipande kwa wanufaika wako ulojaza katika fomu ya kujiunga. Vipande ni mali kama mali zingine kama ardhi katika kurithisha au kuwapa wale watu wetu wa karibu.
9. Viambatanisho muhimu unapofungua akaunti ya uwekezaji UTT AMIS. Uwe na baadhi ya hivi vitambulisho: Kadi ya kupigia kura, leseni ya udereva, NIDA, Hati ya kusafiria + passport picha ( blue background)
10. Vipande vya UTT AMIS vinaweza kutumika kama dhamana katika taasisi za kifedha
Haya ni vyema ukafahamu kama ulikuwa hujajua.