Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Download app, jisajili na anza kuweka michango yako humo. Baada ya hapo utahitaji kudownload form yao unajaza particular zako na kuituma kwa email au ende physically ofisini kwao. Maelezo yote haya yapo kwenye website yaoHivi nikitaka kujiunga UTT amis ni lazma niende ofisini kwao?? Na je, mfuko gani una return nzuri?
Download app, jisajili na anza kuweka michango yako humo. Baada ya hapo utahitaji kudownload form yao unajaza particular zako na kuituma kwa email au ende physically ofisini kwao. Maelezo yote haya yapo kwenye website yao
Idadi ya mifuko hadi sasa ni 6:Mkuu kama una maelezo ya hizo scheme ipi ni nzuri zaidi
Je ni mfuko gani mzuri wa kuwekeza UTT AMIS ?Idadi ya mifuko hadi sasa ni 6:
Ukwasi| Jikimu| Wekeza Maisha | Umoja | Hatifungani | Watoto.
1. Sasa unaweza kuuza vipande vyako kwa njia ya menu ya simu, siminvest *150*82#. Nenda eneo wameandika "Kuuza Vipande". Ukomo ni milioni 2 kwa siku.
2. Ukishafanya zoezi la kuuza au kutoa hela basi utatumia ndani ya muda usiozidi siku 3 kupata hela yako katika akaunti ya benki ulojaza wakati unafungua au kukamilisha usajili wako. Ndani ya siku 3 za kazi ni kwa mfuko wa Ukwasi/Liquid Fund huku mifuko mingine ni ndani ya siku 10 za kazi. #Siku za kazi ni J3 hadi Ijumaa#.
3. Unaweza kufungua akaunti yako kwa njia karibu 6 ( kwa njia ya simu *150*82#, Utt amis app, kujaza fomu mtandaoni, CRDB benki au kutembelea ofisi za UTT AMIS ). Kwa njia ya simu na app utaweza kuendelea kununua vipande/kuweka hela ila itakusumbua kutoa endapo hutakamilisha usajili wako.
4. Unaweza kutumia njia mbalimbali kuchangia/kuweka hela yako UTT AMIS. Kuanzia kuweka kwa njia ya benki ( CRDB, NMB, NBC), njia ya benki mtandaoni ( CRDB simbanking, NMB mkononi), mawakala ( CRDB), Utt amis app na mitandao ya simu yote nchini hadi Azam Pesa.
5. Unapoweka pesa yako unaweza kufuatilia salio ndani ya siku 3 za kazi kwa njia hizi: kwa siminvest menu *150*82# ( uliza salio), UTT AMIS app na tatu kuomba statement yako kupitia uwekezaji@uttamis.co.tz
6. Unaweza kufungua akaunti ya mtu mmoja ( individual account) au akaunti ya pamoja ( Joint account) kwa mtu zaidi ya mmoja ( wenza), vikundi, taasisi na asasi mbalimbali
7. Unaruhusiwa kufungua mfuko zaidi ya mmoja kulingana na malengo yako wewe yalivyo. Unaruhusiwa kuwekeza kusikokuwa na ukomo.
8. Unaruhusiwa kurithisha vipande kwa wanufaika wako ulojaza katika fomu ya kujiunga. Vipande ni mali kama mali zingine kama ardhi katika kurithisha au kuwapa wale watu wetu wa karibu.
9. Viambatanisho muhimu unapofungua akaunti ya uwekezaji UTT AMIS. Uwe na baadhi ya hivi vitambulisho: Kadi ya kupigia kura, leseni ya udereva, NIDA, Hati ya kusafiria + passport picha ( blue background)
10. Vipande vya UTT AMIS vinaweza kutumika kama dhamana katika taasisi za kifedha
Haya ni vyema ukafahamu kama ulikuwa hujajua.
Je unapofungua akaunti ya UTT AMIS kuna gharama za awali ?Je ni mfuko gani mzuri wa kuwekeza UTT AMIS ?
Jibu: Mifuko yote mizuri kulingana na lengo anayewekeza anawekeza kwa malengo yepi. Hivyo mwekezaji inabidi ajue lengo lake la uwekezaji ni lipi na hili litampa mwanga wa aina ya mfuko wa kuwekeza.
Kabla hujawekeza pata elimu, jua malengo yako, kipato chako na pengine umri wako. Hivi vitakusaidia kujua wapi uweke hela yako.
Jamaa ni wajanja kweli,, wamejilocate kwenye Majiji tu basi.. Huku mikoani hamna wenye pesa😂Bukoba hawana ofisi
View attachment 3200603
Nakumbuka siku naenda tawi la CRDB kujaza fomu ya kukamilisha USAJILI yule muhudumu alianza kunipanga kuwa niachane na UTT, niingie Kwao (Mama Samia Infrastructure Bond)But siku za nyuma CRDB bank walikuwa wakala wao ila nasikia na wao wameanzisha mfuko kama huo wa UTT so not sure kama wana offer huo uwakala
Hapa umetoa jibu General, kama ilivyo kwenye web yaoJe ni mfuko gani mzuri wa kuwekeza UTT AMIS ?
Jibu: Mifuko yote mizuri kulingana na lengo anayewekeza anawekeza kwa malengo yepi. Hivyo mwekezaji inabidi ajue lengo lake la uwekezaji ni lipi na hili litampa mwanga wa aina ya mfuko wa kuwekeza.
Kabla hujawekeza pata elimu, jua malengo yako, kipato chako na pengine umri wako. Hivi vitakusaidia kujua wapi uweke hela yako.