Nikitizama mlima Kitonga naona pale pia tunaweza pata chanzo cha mapato

Kiukweli, nikisema toka moyoni, Watanzania tunatakiwa kupewa elimu ya uzalendo, hilo ndilo lilifanyika hata kwa nchi zilizoendelea hadi zikaendelea. kwamfano, kukubali kuumia kuchangia shilingi alfu moja tu kwa gari inayopita kitonga au senkenke, sio kwa ubaya ila kwa uzalendo wa kuchangia pato la taifa, kama tu wazee wetu walivyokuwa wazalendo wakachangia kodi ya kichwa (ambayo wengi wanailaani lakini ilikuwa muhimu kwa wakati huo), tunaweza kupata pesa zetu wenyewe, tukafanya maendeleo ya haraka. ni kiasi kikubwa sana cha pesa kinaweza kupatikana, imagine magari mangapi yanapita pale kila siku na kila siku tutakuwa tunaingiza shilingingapi? cha muhimu ni kuwaelimisha tu watu wenye akili ngumu wanaokwepa kufanya jambo lolote ili kuendeleza nchi, ambao wanamini tunaweza kupatap pesa toka nje ya nchi, misaada ili kuendeleza nchi.

watu wapo tayari kuhonga pesa malaya hata alfu hamsini, ila kuchangia alfu moja au mbili kujenga nchi wanalalamika, hawajui kama tukijiumiza tukachangia kwenye pato, kwa amaini tu na kiuzalendo tu, tunaweka mazingira mazuri ya kimaendeleo kwa Taifa yatayayotufanya tuishi maisha mazuri baadaye kama Taifa na pia hili litawafanya Watanzania kuwa na uchungu zaidi na nchi yao. ukichangia vya kutosha kwenye nchi yako utakuwa na hasira nzuri kwa wale wanaokula kodi zako, utakuwa na maamuzi murua hata kwenye uchaguzi wa viongozi (general elections), na kila mtu atakuwa kwenye nafasi ya kuiwajibisha nchi. hili ndilo linalotokea ulaya, kule watu wamepigwa makodi sana na hicho ndicho kinachowafanya wawe na sauti kuiwajibisha serikali. hoja hii wanaoweza kuielewa ni wale wenye akili tu, wale sukuma twende hawataielewa. wataona wanaumizwa kwa mchango wa hiari wa buku au hata buku mbili tu kwa ajili ya maendeleo ya taifa lao. kuweni wazaendo. tena watakao katwa pale hata sio masikini, ni wato wenye uwezo wa kumiliki alfu moja (madereva na wamiliki wa magari, hakuna mkulima au masikini atakayepigwa mchango huo moja kwa moja). na wala sio pesa nyingi hiyo.
 
Huu uzi wa ndugu komeo la chuma ndio uzi Bora wa mwezi hapa jf, tunaomba sana mheshiniwa Komeo uendelee kuangalia na milima mingine ili kuongeza mapato ya serikali yetu ya awamu ya sita. Nadhani mh waziri atalufanyia kazi hili, Maendeleo hayana chama
 
Mbona huoni mbali?
Hata wananchi na watalii wote wanaoingia jiji la Dsm, Dodoma, Arusha na Moshi, na wale wanaoingia Mwanza wapigwe kodi Thsh 5,000 kwa kichwa.
Pesa nyingi sana hizo tunaziachia.
 

Wee jamaa mbona umewaza kama mimi[emoji28][emoji28]
Tena barabara ipanuliwe pale iwe hata njia 8 ili kuepusha ajali
 
"Mwenye Meno akicheka, Mwenye Mapengo Huudhika "
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 

..ukiweka barabara au daraja la tozo unatakiwa uwe na barabara mbadala ambayo haina tozo.

..kwa mfano unaweza kuweka tozo ktk daraja la coco beach, halafu wasiotaka kulipa tozo wakawa wanatumia daraja la selander.
 
Hongera kwa PHD.naona UNANIFANYIA kazi haswaaaa
 

Una uwezo mdogo wa kufikiri kama wa Mwigulu
 
Wazo la Road-Toll sio baya wala sio jipya, zilikuwepo wakati mzee Msuya akiwa waziri wa fedha.
Pia zipo South Africa na Zambia pamoja na carbon Tax. Namibia na Tanzania road toll zinalipishwa mipakani kwa magari yenye namba za kigeni.
Kama tunataka Road Toll itabidi iwe kwa barabara zote, vinginevyo hizo sehemu mbaya apewe mkandarasi kwa mfumo wa PPP, ajenge barabara nzuri ya kisasa yenye lane ya kupandia mlima kwa magari makubwa yanayoenda taratibu, akusanye pesa zake kwa mfumo wa road toll.
 
Mimi nilisema kwanini kusiwe na kodi za mchezo kitaifa kila wiki unatoka mkoa mmoja (wananchi wanapewa minoti)[emoji1787]
wazo zuri muheshimiwa spidernyoka nitaunda kijikamati changu kitakachoongozwa na kaka yangu muheshimiwa Kabudi,watakaa kitako wanipe mapendekezo kisha ataniletea mapendekezo ya hicho kijikamati kidogo kitakapomaliza kazi.
 
Siku hizi kila mtu ni mchumi. Mnataka selekale ipate hela bila kuwekeza.
 
Magari madogo yalipie tsh. 1,000, size ya kati tsh. 2,000, mabasi na malori iwe tsh. 5,000.
Yaani watu tunapita ile milima na yale makona mioyo yote inadunda bado unataka kutuongezea Pressure ya kulipia tozo? hebu tuache ....... tunaendelea na tafakari vile tutawanyosha 2025 majimboni kwenu!!!
 
sema bro wako anayo macho kama mbalamwezi iliyokomaa, hv usikute yeye ndo mwenye macho madogo kwenu!!
[emoji23][emoji28]DπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Jicho kama taili la trekta.

haya nimekuelewa muheshimiwa Twilumba ila na wewe ukue sasa,uende ukafanye kazi kama kuna mahala utashindwa sema tutakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…