Kiukweli, nikisema toka moyoni, Watanzania tunatakiwa kupewa elimu ya uzalendo, hilo ndilo lilifanyika hata kwa nchi zilizoendelea hadi zikaendelea. kwamfano, kukubali kuumia kuchangia shilingi alfu moja tu kwa gari inayopita kitonga au senkenke, sio kwa ubaya ila kwa uzalendo wa kuchangia pato la taifa, kama tu wazee wetu walivyokuwa wazalendo wakachangia kodi ya kichwa (ambayo wengi wanailaani lakini ilikuwa muhimu kwa wakati huo), tunaweza kupata pesa zetu wenyewe, tukafanya maendeleo ya haraka. ni kiasi kikubwa sana cha pesa kinaweza kupatikana, imagine magari mangapi yanapita pale kila siku na kila siku tutakuwa tunaingiza shilingingapi? cha muhimu ni kuwaelimisha tu watu wenye akili ngumu wanaokwepa kufanya jambo lolote ili kuendeleza nchi, ambao wanamini tunaweza kupatap pesa toka nje ya nchi, misaada ili kuendeleza nchi.
watu wapo tayari kuhonga pesa malaya hata alfu hamsini, ila kuchangia alfu moja au mbili kujenga nchi wanalalamika, hawajui kama tukijiumiza tukachangia kwenye pato, kwa amaini tu na kiuzalendo tu, tunaweka mazingira mazuri ya kimaendeleo kwa Taifa yatayayotufanya tuishi maisha mazuri baadaye kama Taifa na pia hili litawafanya Watanzania kuwa na uchungu zaidi na nchi yao. ukichangia vya kutosha kwenye nchi yako utakuwa na hasira nzuri kwa wale wanaokula kodi zako, utakuwa na maamuzi murua hata kwenye uchaguzi wa viongozi (general elections), na kila mtu atakuwa kwenye nafasi ya kuiwajibisha nchi. hili ndilo linalotokea ulaya, kule watu wamepigwa makodi sana na hicho ndicho kinachowafanya wawe na sauti kuiwajibisha serikali. hoja hii wanaoweza kuielewa ni wale wenye akili tu, wale sukuma twende hawataielewa. wataona wanaumizwa kwa mchango wa hiari wa buku au hata buku mbili tu kwa ajili ya maendeleo ya taifa lao. kuweni wazaendo. tena watakao katwa pale hata sio masikini, ni wato wenye uwezo wa kumiliki alfu moja (madereva na wamiliki wa magari, hakuna mkulima au masikini atakayepigwa mchango huo moja kwa moja). na wala sio pesa nyingi hiyo.