Nikiukumbuka Muungano: 14-10-2024: Siwezi kumuenzi Mwalimu Nyerere

Nikiukumbuka Muungano: 14-10-2024: Siwezi kumuenzi Mwalimu Nyerere

Tanganyika haipo kwasababu muungano wetu ulizalisha nchi mbili, Zanzibar na Tanzania, makao makuu yote ya Tanzania yapo huku kwenye Tanganyika ya zamani, mbona Wazanzibar hawalalamiki? ni suala la kukubaliana tu
Wanalalamikaje wakati nchi yao bado inaonekana kwenye Muungano na wanakula matunda ya kuwa ndani ya muungano.

Issue ni kwanini unapotoka huko makao makuu ya muungano ukiwa unaenda Zanzibar unakuwa kama mgeni.? Kwanini wao wanafaidia na kila kipengele cha kimuungano kama nchi ila watanganyika hawafaidiki.?
 
Wanalalamikaje wakati nchi yao bado inaonekana kwenye Muungano na wanakula matunda ya kuwa ndani ya muungano.

Issue ni kwanini unapotoka huko makao makuu ya muungano ukiwa unaenda Zanzibar unakuwa kama mgeni.? Kwanini wao wanafaidia na kila kipengele cha kimuungano kama nchi ila watanganyika hawafaidiki.?
Wazanzibar ni watu wa hovyo sn, wabaguzi na wadini
 
Wanalalamikaje wakati nchi yao bado inaonekana kwenye Muungano na wanakula matunda ya kuwa ndani ya muungano.

Issue ni kwanini unapotoka huko makao makuu ya muungano ukiwa unaenda Zanzibar unakuwa kama mgeni.? Kwanini wao wanafaidia na kila kipengele cha kimuungano kama nchi ila watanganyika hawafaidiki.?
Hizo ni gharama ndogo ndogo za muungano, kila mmoja lazima apoteze kitu
 
Zanzibar hajawai kuwa mnyonyaji, hata wakati wana ungana Tanganyika ilikuwa imara kuliko Zanzibar, kwahiyo Nyerere alifanya muungano akiwa yeye ndio anajiweza kuliko Karume, nakataa unyonyaji hapa
Sahivi tunanyonywa na wazanzibar balaa wamejaa mpk kwenye ngazi za chini VEOs
 
Ninaandika haya kwa hisia za kina kuhusu Muungano wa Tanzania, hasa katika muktadha wa kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere. Kutokana na muktadha wa kisiasa na kijamii wa sasa, ninahisi kuwa siwezi kumuenzi Mwalimu Nyerere bila kuangazia ukweli kuhusu Muungano.

Muungano huu, ambao ulianzishwa kwa matumaini makubwa, sasa umeonekana kuwa na kasoro nyingi na kutoleta faida kwa pande zote mbili.

Mwalimu Nyerere alikusudia kuunganisha watu wa Tanzania ili kuleta umoja na maendeleo. Hata hivyo, muungano huu umekuwa na athari za kiuchumi na kijamii ambazo zinaweza kuonekana kama unyonyaji.

Pande mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar, zinakabiliwa na changamoto nyingi zinazohusiana na usawa wa kisiasa na kiuchumi. Wakati wa kuanzishwa kwa muungano, wengi walikuwa na matarajio ya ushirikiano wa dhati, lakini ukweli ni kwamba kuna hisia za kutengwa na kutokukurubiana baina ya maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika muktadha wa kisasa, Muungano umekosa muono wa pamoja. Huku Zanzibar ikikabiliwa na changamoto za kiuchumi na kisiasa, Tanganyika pia inakumbana na matatizo yake.

Wakati mwingine, inaonekana kana kwamba Muungano unalenga zaidi kuimarisha nguvu za kisiasa za upande mmoja, huku upande mwingine ukihisi kutelekezwa. Hii inafanya watu wengi kujiuliza: Je, Muungano huu ni wa watu wote au ni wa kuburuzwa?

Kukosekana kwa usawa katika ugawaji wa rasilimali na mamlaka ni miongoni mwa sababu zinazomfanya mtu anayejiita muungano kufikiri zaidi juu ya kukataa muungano. Hali hii inahatarisha umoja wa kitaifa na kuleta mifarakano baina ya wananchi. Ni muhimu kwa jamii kuangalia jinsi Muungano unavyoweza kuboresha hali za maisha za watu wa pande zote mbili, badala ya kuwa ni zana ya unyonyaji.

Kila wakati tunapozungumzia Muungano, ni muhimu kukumbuka maono ya Mwalimu Nyerere. Alitaka kuwa na umoja wa kweli. Hata hivyo, ukweli wa sasa unakumbusha kwamba tunaweza kuwa na umoja bila kuwa na muungano unaonyonya. Ni wakati wa kuangalia njia mbadala za kuimarisha ushirikiano kati ya watu wa Zanzibar na Tanganyika bila kuathiri haki na ustawi wa kila upande.

Katika kukabiliana na changamoto hizi, ni muhimu kufungua majadiliano ya wazi kuhusu mustakabali wa Muungano. Watu wanapaswa kushiriki katika maamuzi yanayowahusu, na si tu kusikia kutoka kwa viongozi. Ni lazima kuunda mfumo ambao unawawezesha wananchi wa pande zote mbili kuhisi kwamba wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa nchi yao. Hii itasaidia kuondoa hisia za kutengwa na kuimarisha umoja wa kitaifa.

Kwa kumalizia, nadhani ni muhimu kufahamu kwamba kumuenzi Mwalimu Nyerere si tu suala la kuadhimisha legacy yake, bali pia ni jukumu letu kutafuta ukweli na haki katika Muungano wetu. Siwezi kumuenzi Mwalimu Nyerere bila kuangazia ukweli kuhusu Muungano huu, ambao umeonekana kuwa ni chanzo cha mgawanyiko badala ya umoja.

Ni wakati wa kuzungumza waziwazi kuhusu changamoto za Muungano na kuangalia njia bora zaidi za kuendeleza umoja wa kitaifa.
Milele amina
 
Mimi kila nikikumbuka hiki kiswahili chake alikikomalia yeye nachoka kabisa sihitaji kumkumbuka daima

Eti lugha ya taifa nyokolo
 
Huu muungano shida zaidi ipo kwenye mipaka,wakitaka kuuvunja hapo mpaka tutapigana,wazanzibar wanataka bahari yote ya tz wanasema ni yao
 
Wanalalamikaje wakati nchi yao bado inaonekana kwenye Muungano na wanakula matunda ya kuwa ndani ya muungano.

Issue ni kwanini unapotoka huko makao makuu ya muungano ukiwa unaenda Zanzibar unakuwa kama mgeni.? Kwanini wao wanafaidia na kila kipengele cha kimuungano kama nchi ila watanganyika hawafaidiki.?
Mkuu kwani wanaokataa Tanganyika isiwepo ni kina nani??

Je ni wazanzibar au watanganyika??

Wanaokataa kujinasibu na Tanganyika ni kina nani??

Tusiwaonee wazanzibar!! Tuache unafiki!!
 
Watu mnatafutaga tu angle ya kumlaumu Nyerere ili nafsi zenu zifurahi. Ehee, hebu nambie, kitu gani alicho kianzisha Nyerere kinaenziwa leo? Azimio la Arusha? Muungano? Siasa zake za ujamaa na kujitegemea? Nini? CCM? Nitajie kimoja. Muungano aliouasisi Nyerere sio hu tulio nao leo; kila kitu cha Nyerere kwasasa hatukifati, tumeshindwa nini kuufanya muungano ule tuutakao leo? Hebu tuache unafiki, unafiki ni dhambi kubwa kuliko kuua na kuzini. Nimemsikia sheikh mmoja huko YouTube anamlaumu Nyerere eti alipendekeza kilimo cha umwagiliaji, baada ya pendekezo lake hilo, mvua ikagoma kunyesha miaka 3 na mito, visima na maziwa vikakauka, anamlaumu Nyerere kwa kupendekeza kilimo cha umwagiliaji? Look, watu wakiwa na chuki na wewe watakutungia kila aina ya uongo ili uonekane mbaya machoni pa watu. Nyerere ana makosa yake mengi tu kama binadamu but anabakia kua kiongozi bora sana aliyetuunganisha Watanzania. Nchi nyingi za Africa, ni nchi lakini hazina utaifa. Mfano Kenya tu hapo, mtu wa Kericho anaweza kwenda kununua ardhi Ukalenjini? Lugha tu kwao ni tatizo but bongo Mkulya anaweza kutoka Tarime na kwenda kuanzisha maisha Masasi, akaoa mwanamke wa Kimakua na kuishi vizuri tu, Mmakua huyo anaweza kwenda ukweni kwake Tarime pekee yake bila kua na hofu yoyote. Nchi nyingi hazina hicho kitu. Wengi wanao mkosoa Nyerere huaga wanaanza na Chuki Kwanza kwake then ndio wanaanza kutafuta sababu za kumchukia. Narudia, ni nini alicho kianzisha Nyerere na hakijawa modified? Angekua sio Nyerere mama yetu mpendwa Samia angekua rais wa Tanzania/Tanganyika?
 
Ninaandika haya kwa hisia za kina kuhusu Muungano wa Tanzania, hasa katika muktadha wa kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere. Kutokana na muktadha wa kisiasa na kijamii wa sasa, ninahisi kuwa siwezi kumuenzi.

nadhani ni muhimu kufahamu kwamba kumuenzi Mwalimu Nyerere si tu suala la kuadhimisha legacy yake, bali pia ni jukumu letu kutafuta ukweli na haki katika Muungano wetu. Siwezi kumuenzi Mwalimu Nyerere bila kuangazia ukweli kuhusu Muungano huu, ambao umeonekana kuwa ni chanzo cha mgawanyiko badala ya umoja.

Ni wakati wa kuzungumza waziwazi kuhusu changamoto za Muungano na kuangalia njia bora zaidi za kuendeleza umoja wa kitaifa.
Kwanza naheshimu mawazo yako na sio lazima kila mtu amuenzi Mwalimu Nyerere kama ilivyo sio kila mtu anamwamini Mungu, wengine wanamwamini shetani.

Kwa vile hoja yako ya kutomuenzi mwalimu ni kuhusu huu Muungano wetu adhimu na adimu, ukitaka tuujadili Muungano, haya basi pokea Rhuksa hii toka kwa huyu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Na baada ya rukhsa hiyo
Leo tarehe 14 October ni siku ya Nyerere Day, tumuenzi kwa kujikumbushe tuliwahi kusema nini, kumhusu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Back
Top Bottom