Nikiukumbuka Muungano: 14-10-2024: Siwezi kumuenzi Mwalimu Nyerere

Tanganyika haipo kwasababu muungano wetu ulizalisha nchi mbili, Zanzibar na Tanzania, makao makuu yote ya Tanzania yapo huku kwenye Tanganyika ya zamani, mbona Wazanzibar hawalalamiki? ni suala la kukubaliana tu
Wanalalamikaje wakati nchi yao bado inaonekana kwenye Muungano na wanakula matunda ya kuwa ndani ya muungano.

Issue ni kwanini unapotoka huko makao makuu ya muungano ukiwa unaenda Zanzibar unakuwa kama mgeni.? Kwanini wao wanafaidia na kila kipengele cha kimuungano kama nchi ila watanganyika hawafaidiki.?
 
Wazanzibar ni watu wa hovyo sn, wabaguzi na wadini
 
Hizo ni gharama ndogo ndogo za muungano, kila mmoja lazima apoteze kitu
 
Zanzibar hajawai kuwa mnyonyaji, hata wakati wana ungana Tanganyika ilikuwa imara kuliko Zanzibar, kwahiyo Nyerere alifanya muungano akiwa yeye ndio anajiweza kuliko Karume, nakataa unyonyaji hapa
Sahivi tunanyonywa na wazanzibar balaa wamejaa mpk kwenye ngazi za chini VEOs
 
Milele amina
 
Mimi kila nikikumbuka hiki kiswahili chake alikikomalia yeye nachoka kabisa sihitaji kumkumbuka daima

Eti lugha ya taifa nyokolo
 
Huu muungano shida zaidi ipo kwenye mipaka,wakitaka kuuvunja hapo mpaka tutapigana,wazanzibar wanataka bahari yote ya tz wanasema ni yao
 
Mkuu kwani wanaokataa Tanganyika isiwepo ni kina nani??

Je ni wazanzibar au watanganyika??

Wanaokataa kujinasibu na Tanganyika ni kina nani??

Tusiwaonee wazanzibar!! Tuache unafiki!!
 
Watu mnatafutaga tu angle ya kumlaumu Nyerere ili nafsi zenu zifurahi. Ehee, hebu nambie, kitu gani alicho kianzisha Nyerere kinaenziwa leo? Azimio la Arusha? Muungano? Siasa zake za ujamaa na kujitegemea? Nini? CCM? Nitajie kimoja. Muungano aliouasisi Nyerere sio hu tulio nao leo; kila kitu cha Nyerere kwasasa hatukifati, tumeshindwa nini kuufanya muungano ule tuutakao leo? Hebu tuache unafiki, unafiki ni dhambi kubwa kuliko kuua na kuzini. Nimemsikia sheikh mmoja huko YouTube anamlaumu Nyerere eti alipendekeza kilimo cha umwagiliaji, baada ya pendekezo lake hilo, mvua ikagoma kunyesha miaka 3 na mito, visima na maziwa vikakauka, anamlaumu Nyerere kwa kupendekeza kilimo cha umwagiliaji? Look, watu wakiwa na chuki na wewe watakutungia kila aina ya uongo ili uonekane mbaya machoni pa watu. Nyerere ana makosa yake mengi tu kama binadamu but anabakia kua kiongozi bora sana aliyetuunganisha Watanzania. Nchi nyingi za Africa, ni nchi lakini hazina utaifa. Mfano Kenya tu hapo, mtu wa Kericho anaweza kwenda kununua ardhi Ukalenjini? Lugha tu kwao ni tatizo but bongo Mkulya anaweza kutoka Tarime na kwenda kuanzisha maisha Masasi, akaoa mwanamke wa Kimakua na kuishi vizuri tu, Mmakua huyo anaweza kwenda ukweni kwake Tarime pekee yake bila kua na hofu yoyote. Nchi nyingi hazina hicho kitu. Wengi wanao mkosoa Nyerere huaga wanaanza na Chuki Kwanza kwake then ndio wanaanza kutafuta sababu za kumchukia. Narudia, ni nini alicho kianzisha Nyerere na hakijawa modified? Angekua sio Nyerere mama yetu mpendwa Samia angekua rais wa Tanzania/Tanganyika?
 
Kwanza naheshimu mawazo yako na sio lazima kila mtu amuenzi Mwalimu Nyerere kama ilivyo sio kila mtu anamwamini Mungu, wengine wanamwamini shetani.

Kwa vile hoja yako ya kutomuenzi mwalimu ni kuhusu huu Muungano wetu adhimu na adimu, ukitaka tuujadili Muungano, haya basi pokea Rhuksa hii toka kwa huyu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Na baada ya rukhsa hiyo
Leo tarehe 14 October ni siku ya Nyerere Day, tumuenzi kwa kujikumbushe tuliwahi kusema nini, kumhusu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…