Nikiwa kama mzazi namuunga mkono Inspector Haroun (Babu) kumtembezea kipigo mtoto wake baada ya kumkuta studio

Nikiwa kama mzazi namuunga mkono Inspector Haroun (Babu) kumtembezea kipigo mtoto wake baada ya kumkuta studio

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Inspector Haroun (Babu) amemtembezea kipigo mtoto wake akidai kwamba mtoto amempeleka chuo ila anashangaa kumkuta studio

1736981631187.png

Yupo sahihi kwasababu uchungu wapesa anayolipa chuo tunaujua tunaolipia ada. Mzazi au mlezi unaweza kutimiza wajibu mtoto aende kusoma shule za serikali bure lakini utaanza kusomesha akifika chuo bila mkopo, vyuo vinagharimu mamilioni, Gharama za kumsomesha mtoto chuoni zipo juu sana, Pocket money, ada, laptop, hostel, n.k. kwa mwaka inafikia mpaka milioni 4.

Nikweli kama nchi tuna tatizo la ajira lakini katika wahitimu 100 wa vyuoni, kwa makadirio 40 wanaweza kuajiriwa ama kujiajiri kwa elimu zao, kwenye Muziki katika wasanii 100 ni watatu wanaweza kufanikiwa tena hao unachanganya na wale wanaotoa wimbo moja na kupotea mazima.

Nakumbuka enzi hizo nikiwa sekondari mpaka chuo kuna washikaji waliojaribu kuingia kwenye muziki wameharibu sana future zao. wapo waliothubutu kutumia ada kulipia studio mpaka Leo hawana ishu za maana muziki uliwakataa,

Muziki wa Tanzania hata ukifanikiwa kutoboa ni ngumu kumaintain zaidi ya miaka kumi, Kuna wasanii wengi sana waliowahi kuzishika chati lakini leo hii wamepotea kabisa

Babu anaujua vema muziki wa hapa Bongo, ameona kabisa mwanae hajui muziki wala hana ujanja kwenye muziki ndio maana kaona bora asome.
 
Kipigo itasaidia nini na kwa kumdhalilisha kwa wenzake?

Kumchukua wakakaa chini wawili tu.. akaeleza sababu za kuwa pale na mengine mengi ya mtoto wake angeyajua na kupanga ushauri hata hiyo iwe part time au kama hobby

Ila mmmh mzazi kupanga ya career ya mtoto wengine yanawatokea puani
 
Bongo movie hiyo. Hakuna kitu hapo
 
Bongo sahv kila mtoto anataka kuwa msanii mkata uno

Ova
 
Back
Top Bottom