Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

Tafadhali naomba ukiwa kama mwana Wenge BCBG yake JB Mpiana uniambie ni kwanini Nyimbo hizi Nne zifuatazo haziishi Utamu na wala hazichuji miaka nenda rudi?

1. Champion Kapangala ( Sebene )
2. Omba ( Rhumba )
3. Wallah Danico ( Sebene )
4. Sans te Toucher ( Rhumba )

Kama una 'updates' zozote za kuihusu Bendi hii yetu pendwa ya Wenge BCBG yake JB Mpiana tafadhali karibu utupatie kwani hii Bendi ambayo Mbinguni kwa Mungu Baba inapendwa na imebarikiwa kabisa.

Wenge BCBG ni Mashine ya Muziki hasa!
Mkuu nilijua shabiki wa kuugua kwa wenge BCBG nipo peke yangu, kala eboing na hi ho ha pale waliuwa!
 
Theodor Ngiama Obiang
Adolph Muteba Chilamwina
Jose Kongolo
Hamed Bakayoko
Pedeshee Dariol Mulongo
Adam Bombole
Fabrice Wasepe
Patricke Bolonya
Mohamed Munuo
Monsieur De Congolaise
Mabanga pambapamba
Tchacho Ombara
Paul Mukoko
Roger Nsunga
Boria Bondo bebe Ramasani
 
JB Mpiana hatokuja kufanya tena show kama hii

Si kweli kuna Mbili alizifanya nchini Ubelgiji na nyingine eneo la FIKIN huko Congo DR ambako Kumbi na Uwanja ulijaa hadi Pomoni ( Ulifurika ) mpaka kupelekea Vifo vichache kutokana na 'Stampede' iliyotokea.
 
Hakuna vibao vinavyonikosha vya hawa mabwana kama Feux de I’amour na Masuwa vyote wameimba na Papa Wemba….

Nikiwa nimekaa kiti kirefu nashusha bia nikikumbuka harakati za miaka ya tisini hakika nimezeeka sasa…
Nimeona jina lako nkakumbuka ngoma ya nina
 
Wenge Msison mere
Hakuna Bendi iitwayo Wenge Msison mere kama 'ulivyojitutumua' Kuandika bali kuna Bendi iitwayo Wenge Maison Mere ( MM ) yake Ngiama Makanda Werrason Noel ikimaanisha Wenge Nyumba ya Mama na Wenge Bon Chic Bon Genre ( BCBG ) yake Jean Bedele Tshituka Mpiana ikimaanisha Wenge Wazuri na Watanashati.
 
Nipo home namsikiliza Madilu System, Ya Jean napenda ku_replay sana hii ngoma
Tafadhali msinitafute Ubaya katika huu Uzi wangu na bahati nzuri unajieleza vizuri tu kuwa ni wa Kuihusu Bendi ya Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana hivyo kama nanyi mna Mapenzi na Wanamuziki wa Bendi zingine na Nyimbo zao anzisheni 'threads' zao ila sitaki mtumie huu Uzi wangu GENTAMYCINE kama Lifti yenu ya kusema Mahaba na hao mnaowapenda.

Mtanikwaza sasa hivi na niwajibu hovyo.
 
Sorry mkuu,nilikuwa naonesha heshima heshima kwa nyimbo za wenzetu.
 
Sorry mkuu,nilikuwa naonesha heshima heshima kwa nyimbo za wenzetu.
Umeshindwa kuanzisha Uzi wao Maalum hadi uje uwasifie na uwaonyeshe hiyo Heshima katika huu Uzi wangu Maalum wa kuihusu Bendi yangu pendwa na Tukuka ya Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana?
 
Back
Top Bottom