Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

Mkuu nilijua shabiki wa kuugua kwa wenge BCBG nipo peke yangu, kala eboing na hi ho ha pale waliuwa!
 
Theodor Ngiama Obiang
Adolph Muteba Chilamwina
Jose Kongolo
Hamed Bakayoko
Pedeshee Dariol Mulongo
Adam Bombole
Fabrice Wasepe
Patricke Bolonya
Mohamed Munuo
Monsieur De Congolaise
Mabanga pambapamba
Tchacho Ombara
Paul Mukoko
Roger Nsunga
Boria Bondo bebe Ramasani
 
JB Mpiana hatokuja kufanya tena show kama hii
Si kweli kuna Mbili alizifanya nchini Ubelgiji na nyingine eneo la FIKIN huko Congo DR ambako Kumbi na Uwanja ulijaa hadi Pomoni ( Ulifurika ) mpaka kupelekea Vifo vichache kutokana na 'Stampede' iliyotokea.
 
Hakuna vibao vinavyonikosha vya hawa mabwana kama Feux de I’amour na Masuwa vyote wameimba na Papa Wemba….

Nikiwa nimekaa kiti kirefu nashusha bia nikikumbuka harakati za miaka ya tisini hakika nimezeeka sasa…
Nimeona jina lako nkakumbuka ngoma ya nina
 
Wenge Msison mere
Hakuna Bendi iitwayo Wenge Msison mere kama 'ulivyojitutumua' Kuandika bali kuna Bendi iitwayo Wenge Maison Mere ( MM ) yake Ngiama Makanda Werrason Noel ikimaanisha Wenge Nyumba ya Mama na Wenge Bon Chic Bon Genre ( BCBG ) yake Jean Bedele Tshituka Mpiana ikimaanisha Wenge Wazuri na Watanashati.
 
Nipo home namsikiliza Madilu System, Ya Jean napenda ku_replay sana hii ngoma
Tafadhali msinitafute Ubaya katika huu Uzi wangu na bahati nzuri unajieleza vizuri tu kuwa ni wa Kuihusu Bendi ya Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana hivyo kama nanyi mna Mapenzi na Wanamuziki wa Bendi zingine na Nyimbo zao anzisheni 'threads' zao ila sitaki mtumie huu Uzi wangu GENTAMYCINE kama Lifti yenu ya kusema Mahaba na hao mnaowapenda.

Mtanikwaza sasa hivi na niwajibu hovyo.
 
Sorry mkuu,nilikuwa naonesha heshima heshima kwa nyimbo za wenzetu.
 
Sorry mkuu,nilikuwa naonesha heshima heshima kwa nyimbo za wenzetu.
Umeshindwa kuanzisha Uzi wao Maalum hadi uje uwasifie na uwaonyeshe hiyo Heshima katika huu Uzi wangu Maalum wa kuihusu Bendi yangu pendwa na Tukuka ya Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…