Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

Kuna wimbo mmoja JB mpiana anawataja wanamuziki wote wa bendi yao ni nzuri sana,

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Mara nyingi JB Mpiana hupenda Kuwataja Wanamuziki wake wote katika nyimbo Mbili tu za taratibu ( Rhumba ) za Omba na Jeanette.

Na hakuna Wanamuziki ambao JB Mpiana huwa akiwataja kwa Kuwaimba hujikuta hata akitokwa na Machozi ya Kihisia kama aliyekuwa Mwanamuziki wake Kipenzi ndani ya Bendi Alain Mpela 'Afande' na Rapa ( Atalaku ) wake Kipenzi Tutu Calugi bila Kumsahau aliyekuwa Mpiga Gitaa wake wa Bass ( Besi ) na Mmoja wa Waanzilishi wa iliyokuwa Bendi Mama ya Wenge Musica BCBG 4 X 4 iliyokuwa imesheheni 'Mafundi' watupu kama JB Mpiana mwenyewe aliyebaki na Wenge BCBG, Ngiama Makanda Werrason aliyebaki na Wenge Maison Mere, Blaise Bula ( ambaye ni Msomi sana na Kitaaluma ni Injinia wa Ndege ) aliyebaki na Bendi ya Wenge Ponderation na Adolphe Dominguez aliyebaki na Wenge Affaire Tonya Tonya bila Kuwasahau akina Alain Mpela, Aimelia Byakodile, Suzuki na Ferre Gola ambaye amefundishwa Mziki na JB Mpiana japo Werrason baadae akampika zaidi Kimuziki na leo nae anajitegemea.
 
Daaa ile shughuli si ya kitoto ndio Mana hadi makoo huwa yanaleta shida. Mungu amtendee vema!
Ni kweli ile aina ya Kurapu ( Kughani ) ya Roberto Wunda Enkokota inasababisha Kuugua Koo kwani unatumia Nguvu nyingi na ndiyo maana Tutu Calugi akaja na Rapu ( Atalaku ) yake isiyotumia Nguvu nyingi na yenye Sauti ya Juu ambayo ndiyo imekuja Kuigwa karibia na Marapa ( Atalakus ) wengi wa Congo DR kwa sasa.

Marapa ( Atalakus ) waliomuiga Roberto Wunda Enkokota na ambao nao wako ( walikuwa ) hatarini Kuugua Saratani ( Cancer ) ya Koo ni kama Wafuatao..

1. Mukeba Kalondji ( BILL CLINTON )
2. Faustine Nzinga Yankobo CELLULAIRE ( Marehemu ) sasa
3. Gesac
4. Eyale Kalondji ( KEROZENE )
 
Mara nyingi JB Mpiana hupenda Kuwataja Wanamuziki wake wote katika nyimbo Mbili tu za taratibu ( Rhumba ) za Omba na Jeanette.
Pia, kuna ule wimbo uitwao DADDET, kule mwishoni ametaja baadhi ya majina. Huo wimbo, nao huwa naupenda sana. Pia, huwa sichoki kuangalia ile video maarufu kwa jina la "Hi ho ha"!
 
Pia, kuna ule wimbo uitwao DADDET, kule mwishoni ametaja baadhi ya majina. Huo wimbo, nao huwa naupenda sana. Pia, huwa sichoki kuangalia ile video maarufu kwa jina la "Hi ho ha"!
Ni kweli Mkuu mwishoni mwa huo Wimbo aliwataja akina Didier Masela, Werrason, akajitaja JB Mpiana, Alain Makaba na akammalizia Injinia wa Ndege na Mwanamuziki Msomi Blaise Bula.
 
BCBG for life, taja nyimbo zote lakini Kama hakuna Kalayi Boeing hiyo siyo Wenge ni Mawenge.
Aisee nimeenda youtube nimekutana na mwanya ulio katikati ya meno meupe masafi ya mtoto mzuri na sauti nzito za vidume zilisho shiba hakika vijana wa enzi hizo walifurahia muziki halisi wa kiafrika.
 
Aisee nimeenda youtube nimekutana na mwanya ulio katikati ya meno meupe masafi ya mtoto mzuri na sauti nzito za vidume zilisho shiba hakika vijana wa enzi hizo walifurahia muziki halisi wa kiafrika.
Mkuu, kile kizazi, we acha tu! Wale jamaa kabla hawajatawanyika, ilikuwa balaa! Kama alivyosema Genta, miaka ile, ile Bendi haikuwa ya Taifa huko kwao tu, bali ilikuwa inapendwa sana na Vijana sehemu mbali mbali, hata hapa Tanzania. Vijana wa wakati huo, walikuwa wanawaiga mpaka mpaka mavazi!
 
Vijana wa sasa wapo na amapiano na kamserereko ya baba levo😑
 
Alikuwa akiitwa Roberto Wunda Enkokota ila sasa anaumwa Saratani ( Cancer ) ya Koo na yuko nchini Ufaransa.

Baada ya tatizo lake hilo nafasi yake ndiyo ilikuja Kuzibwa vyema na Tutu Calugi ( Yombo Lumbu ) ambaye ndiyo Mwalimu wa Marapa ( Atalakus ) wengi wa Bendi za Congo DR kama vile Theo Mbala ( aliyerapu kwa Aurlus Mabele, Madilu System na Bozi Boziana ), Celeo Mozami Muviu ( aliyerapu na Werrason katika Bendi yake ya Wenge Maison Mere ) na Fusee De Gaire ambaye sasa anarapu na JB Mpiana katika Bendi yake ya Wenge BCBG akichukua nafasi ya Rapa ( Atalaku ) Marehemu Cellulaire ( Faustin Nzinga Yankobo ) akisaidiana na Atalaku ( Rapa ) Mkuu wa Wenge BCBG aitwae GENTAMYCINE ( Pitshou Lisimo ) pamoja na akina Pajo na Bin Laden.
Kumbe mkuu jina lako ulilibandua kutoka kwa huyu jamaaa.Saaafiii sana endelea kuipenda Wenge BCBG
 
Tafadhali naomba ukiwa kama mwana Wenge BCBG yake JB Mpiana uniambie ni kwanini Nyimbo hizi Nne zifuatazo haziishi Utamu na wala hazichuji miaka nenda rudi?

1. Champion Kapangala ( Sebene )
2. Omba ( Rhumba )
3. Wallah Danico ( Sebene )
4. Sans te Toucher ( Rhumba )

Kama una 'updates' zozote za kuihusu Bendi hii yetu pendwa ya Wenge BCBG yake JB Mpiana tafadhali karibu utupatie kwani hii Bendi ambayo Mbinguni kwa Mungu Baba inapendwa na imebarikiwa kabisa.

Wenge BCBG ni Mashine ya Muziki hasa!
Genta mambo natofautiana na wewe kwenye mambo mengi hapa JF na mara kadhaa tunakwaruzana ila linapokuja suala la Wenge BCBG basi naamua kuwa kitu kimoja na wewe hapa nilipo nasikiliza goma tuliloruka nalo pale Leaders mwaka 2014 linaitwa GECOCO basi nkaamua kwenye searching area ya JF nitype neno "Mpiana" ahamadi!!! Kwenye search result ni thread yako mkuu..Hakika Wenge BCBG wamenipa raha sana maishani mwangu tangu 1998 ni shabiki wao kindakindaki...Naona umeitaja Omba hapo juu hiyo kwangu ndio the best ever ikifuatiwa na Jeannette na Masuwa bila kusahau Feux de'l amour ...ubarikiwe sana mkuu
 
Asante mno Mkuu. Kuhusu Mimi nawe Kutofautiana Kwetu hapa JamiiForums mara kwa mara wala Kusikuumize kwani huo ndiyo Ubinadamu na katika Mijadala ya Kihisia ni Jambo la Kawaida na Afya ya Akili pia.

Kumbe Siku ile December 2013 Wenge BCBG yake JB Mpiana walipopiga pale Leaders Club katika Tamasha Maalum la iliyokuwa Bendi ya Mashujaa tulikuwepo Wote?

Hakika Mkuu hakuna Siku ambayo GENTAMYCINE nilifurahi na nilicheza mno tena bila Kuchoka kuanzia Saa 5 Usiku walipopanda na Kupiga 'Non Stop' hadi Saa 12 Alfajiri.

Na Furaha yangu zaidi Siku ile ilikuwa ni Kukutana ana kwa ana na Mghani / Rapa ( kwa Kikongo wanaita Atalaku ) Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE Mwenyewe ) akiwa na Mwimbaji mwenzake Rio Biku a.k.a De Jeneiro na baadae nikapeana Mkono na Mnenguaji wa Kike Mrembo kuliko Wote ndani ya Bendi hiyo aitwae Igre Montra ( Jina halisi Yeti Munyeti )

Na nakumbuka nilipokutongoza nae Ataluku ( Mghani ) Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ) Mwenyewe nikamsalimie kwa Kumuita hivyo na akaongezea kwa kusema...Le Champione Animateur du Congo...akimaanisha Yeye si tu ni GENTAMYCINE bali pia ni Rapa ( Atalaku ) Bingwa Congo DR nzima. Kwa Lugha ya Kifaransa neno Rapa au Mghani linaitwa Animateur ila kwa Kilingala ndiyo wanaita Atalaku.

Kikubwa zaidi nilichojifunza Siku ile cha Kimuziki kutoka kwa Wenge BCBG na hata Bendi zote za Congo DR ni kwamba hawa Jamaa wanajua Kujipanga, kufanya Maandalizi na wanapenda mno Kuwafurahisha Mashabiki waliolipia Kiingilio Kuingia Kuwaona tofauti na Bendi nyingi za Kitanzania ( Bongo ) ambapo nyingi Masihara na Upuuzi vimekuwa Vipaumbele vyao.
 
Ndiyo Wimbo bora wa Rhumba ( Mziki wa taratibu ) ambao umemfanya JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG Kupendwa, Kukubalika na kuwa Tishio Congo DR nzima na huku Kwingineko.

Na huo Wimbo JB Mpiana aliuimba kwa 'Hisia' hizo za juu kwakuwa alikuwa akimuimbia aliyekuwa Mkewe ( Mpenziwe ) wa muda mrefu na aliyempenda sana Amida Shatur ambaye baadae alimsaliti kwa Tajiri ( Pedeshee ) Didi Kinuani ( kama sijakosea ) na baadae kutoka na aliyekuwa Rais wa Congo DR Joseph Kabila.

Ila kwa sasa inasemekana Wawili hawa wamesharudiana kwani walishazaa Watoto wao akina Junior Mpiana ( wa Kiume ) na Suraiya ( wa Kike ) ambao katika Album zote za JB Mpiana huwa anawataja ( anawafagilia ) kama ambavyo hata Koffi Olomide nae hupenda 'Kumfagilia' Mwanae katika Nyimbo zake aitwae Didistone.
Alirudiana naye baada ya Victor Kamerhe kufungwa? [emoji848]
 
Back
Top Bottom